Putin asaini waraka wa kuamuru Majeshi ya Urusi kuingia Ukraine kulinda amani majimboni

Putin asaini waraka wa kuamuru Majeshi ya Urusi kuingia Ukraine kulinda amani majimboni

Rais Putin asaini waraka wa kuamuru majeshi ya Russia kuingia Ukraine kulinda amani ktk majimbo-yenye-uasi ya Luhansk na Donetsk

Rais Vladimir Vladimirovich Putin Putin wa Russia amesaini tamko rasmi/ decree kuamrisha majeshi ya Russia kuingia nchi Ukraine katika majimbo Luhansk na Donetsk, ambayo Russia inadai ni majimbo asili kwa karne nyingi ingawa yapo nchini Ukraine lakini yanayoiunga mkono Russia, hati hiyo aliyosaini rais Vladimir Putin ni ili kulinda amani toka tishio la majeshi ya Ukraine ambayo bado ni tiifu kwa utawala wa rais wa Ukraine ktk mji mkuu wa Ukraine Kiev / Kyiv .

Rais Putin ametoa tamko hili mubashara ktk televisheni na kusema hatua hiyo ni muhimu ili kulinda majimbo hayo mawili yaliyoamua kujitenga toka Ukraine.

Rais Vladimir Putin ameyatambua majimbo hayo ya Ukraine kuwa ni Jamhuri ya Luhansk na Jamhuri Donetsk ikimaanisha siyo tena majimbo ya Ukraine na hivyo kupeleka msaada wa majeshi ya Russia kutekeleza majukumu aliyoyaita kulinda amani.

Ikulu ya White House Marekani imetangaza kuiwekea vikwazo Jamhuri ya Luhansk na Jamhuri Donetsk ya nchini Ukraine huko Umoja wa Ulaya UE nayo imeitisha kikao cha dharura kufuatia hali hiyo mpya huku nchi zingine za Ulaya zikitoa matamko ya kulaani ubeberu wa Russia dhidi ya Ukraine.

Toka mji wake mkuu wa Kyiv, Ukraine imetaka Umoja wa Mataifa / UN kuitisha kikao cha dharura kufuatia hali hiyo.

Source: Russia MoD

Kwa wiki kadhaa majeshi ya Russia yalionekana kujikusanya karibu ya mipaka ya Ukraine pande za nchi za Russia yenyewe, Belarus, Crimea na bahari ya Black Sea kwa kile Russia ilichosema ni mazoezi ya kawaida ya utayari ya majeshi yake. Lakini majeshi ya utambuzi / intelligence ya nchi za umoja wa majeshi ya Ulaya Magharibi na Marekani wa NATO yalitia shaka hicho kilichoitwa mazoezi ya utayari ya Russia kwa wingi wa majeshi, vifaa vya kivita vya ulinzi wa anga, manowari za kivita, ndege za kijeshi, askari wa miguu, logistics, propaganda kupitia media mbalimbali za habari na mpangilio wa formation ilionesha wazi ni mpangilio wa kuweza kufanya uvamizi wa spidi kubwa na kuwapiga butwaa nchi marafiki za Ukraine.


Source : PBS Newshour

Ikumbukwe nchi ya Russia pia inaikalia asilimia 20% ya nchi ya Georgia toka mwaka 2008 na pia iligema eneo la Ukraine la Crimea mwaka 2014 katika bahari ya Black Sea toka Ukraine kupitia pia kuvamia maeneo ya nchi hizo kijeshi kwa sababu hizo hizo za kulinda amani na kuleta amani. Nchi za magharibi hazikuchukua hatua zozote za kijeshi zaidi ya kulaani hatua hizo za miaka iliyopita ktk nchi za Georgia na Ukraine.

Putin orders Russian troops into Ukraine separatist regions | DW News


Russian President Vladimir Putin has signed a decree to send what he is describing as "peacekeeping troops" into the separatist regions of Luhansk and Donetsk. The decision comes after Putin recognized both regions as independent states and described Ukraine as ancient Russian territory. The move could mark a significant escalation amid fears Russia could soon launch a full-scale invasion of Ukraine.

Source : DW News

Mbona kelele nyingi hayo majimbo yanajulikana ni ngome ya Russia mbona hawakuchukua na Kiev yenyewe?
 
Tokea awali Marekani alisema atatoa msaada wa silaha na siyo kuingiza wanajeshi wake vitani, pia labda mtu iwe akili zake haziko sawa kuamini Marekani anaweza kuingia vitani na Urusi kisa ni jimbo lililo huko Ukraine. Nchi za NATO nazo zimetoa baadhi ya msaada kwa Ukraine kama rafiki tu na siyo mwanachama. Ukitaka kuona kile NATO wanaweza kukifanya, Putin ajichanganye kuchukua eneo la nchi mwanachama wa NATO.
Kwa hiyo anaogopa kifiro cha kwenye mabarafu
 
Hao mabeberu siku zao zinahesabika ,, safi sana putin.

Hao mabeberu waendelee huku africa kufanya ubeberu wao wa kipuuzi
Huu msemo kama ulishapoteza maana, Kange alituambia siku za Kigogo zinahesabika, mpaka leo hakuna kitu.
 
Wewe tiliza kitushulio NATO hawana cha kufanya zaidi ya biti za kaboka mchizi
Kuna mtu alisema ugali hudumaza akili, NATO wala USA hawakuwahi kusema watapigana vita kuilinda Ukraine. Ukraine siyo mwanachama wa NATO, sasa mnataka NATO wapigane kwa lipi? NATO walisema watatoa msaada wa silaha na kuiwekea vikwazo Urusi ikiwa itaivamia Ukraine, mlitaka kipi cha zaidi?
 
Kuna mtu alisema ugali hudumaza akili, NATO wala USA hawakuwahi kusema watapigana vita kuilinda Ukraine. Ukraine siyo mwanachama wa NATO, sasa mnataka NATO wapigane kwa lipi? NATO walisema watatoa msaada wa silaha na kuiwekea vikwazo Urusi ikiwa itaivamia Ukraine, mlitaka kipi cha zaidi?
NATO na USA wamepigwa na kitu kizito wanauguliwa maumivu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635]
 
Katika iliyotarajiwa na wengi hatimaye Umoja wa Ulaya unatafakari kuiwekea vikwazo vya kifedha Russia na tayari Kansela wa Ujerumani ameshasimamisha ujenzi wa Nord Stream 2 hii ni baada ya kupigwa na kitu kizito toka kwaJasusi wa zamani wa KGB Rais Vladimir Putin baada ya kutangaza kuyatambua majimbo ya Luhansk Donenst na kuingiza majeshi ya Russia kutoa ulinzi kwa Mataifa hayo.
 
Chechnya ,Georgia, Syria na hatimaye Ukraine muendelezo wa umwagaji damu ya wasio na hatia. Putin siyo wa kuchekewa. Civilized world must come together as one and teach Vladmir Putin a lesson or two on civility and peaceful co-existence.
 
US na NATO walisema wao wataweka vikwazo na si vinginevyo.

Ni ngumu kupambana kijeshi kuisaidia Ukraine directy kwa sababu sio member wa NATO ndio maana walimpa vifaa vya kijeshi,ni wajibu wake kupambana.
Hakuna awezaye kutia mguu mahali Putin atakapokuwa ametia mguu. Saa hii mzee mzima biden anajichanganya!! walitishia vikwazo putin akasema we are immune to sunctions!!
 
Katika iliyotarajiwa na wengi hatimaye Umoja wa Ulaya unatafakari kuiwekea vikwazo vya kifedha Russia na tayari Kansela wa Ujerumani ameshasimamisha ujenzi wa Nord Stream 2 hii ni baada ya kupigwa na kitu kizito toka kwaJasusi wa zamani wa KGB Rais Vladimir Putin baada ya kutangaza kuyatambua majimbo ya Luhansk Donenst na kuingiza majeshi ya Russia kutoa ulinzi kwa Mataifa hayo.
Hilo bomba la Nord stream 2 halikuwa linafanya kazi hivyo huwezi kusema amesimamisha. Ujenzi ulishaisha wakagoma kulifungua. Kwa hiyo hakuna jipya!
 
Huu msemo kama ulishapoteza maana, Kange alituambia siku za Kigogo zinahesabika, mpaka leo hakuna kitu.
Mbona siku zake zilishafika muda tu. Hebu muangalie Kigogo Huyu wa sasa kama ni Yule uliyemjua
 
Natumefurahiiiii sisi wa Russian na kwa taarifa nilizozipata kutoka Moscow putin kalala salama kabsaa na Kala kashiba na kunywa vodka ya Bambuu wale wamarekani wa uyowa mlokuwa mnatoa takwimu za ndege zenu kuwa ni hatari wapuuzi nyinyi mlinichukiza Sana na uchambuzi wenu njooni hapa CNN na BBC wakubwa nyinyi mjomba kaingia mjini mtafanya nn tulishawaambia put in hakuzaliwa kuogopa mashoga haya mmeumbka bango limewaka taa show show mtazificha wapi sura zenu hii iwe fundisho kwenu

axxxxbhfdcvvgsd upuuzi edssdgggdadg bora aasftghbb mkatuliza seffsfgfdg vijambio dsdgvbb

Putin yavlyatetsya luchshim prezidentom vetoy vselennoy.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji119]
 
Back
Top Bottom