pwilo
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 10,913
- 13,876
Zikiwa zimepita siku tatu baada ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia nchini Qatar huku sheria na maagizo mbali mbali yaliyokatazwa katika nchi zikizidi kuleta mshangao kwa wadau na mashabiki wa soka hiyo inakuja baada ya Qatar kuendelea kusimamia sheria za nchi yao ambapo:–
Ndege ya team ya taifa ya ujerumani kuzuiliwa kutua katika nchi hiyo baada ya kuwa na nembo inayoashiria kuunga mkono mapenzi ya jinsi moja katika ndege hiyo hivyo kulazimika kutua Oman na kubadilisha ndege na baadae kuruhusiwa kutua katika nchi hiyo huku baadhi ya mashabiki na wadau wakipinga vikali uamuzi huo.
Vile vile Qatar imekataza unywaji wa pombe hadharani na kuonyeshana mapenzi hadharani kwa watu wa jinsia moja au tofauti kwani nchi hiyo hairuhusu swala hilo hivyo wameonywa kuzingatia hilo kwa mwezi mmoja watakaokuwa hapo na kusisitiza kwamba qatar hawatabadilsha dini kwa siku 30 za kombe la dunia asante sana Qatar.
Wakati hali hiyo ikijitokeza wachezaji na benchi la ufundi la Belgium wameonywa na kukatazwa kutumia jezi zenye nembo ya kuashiria kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja huku manahodha wa team zote zinazoshiriki katika fainali hizo wamekatazwa kuvaa nembo inayoashiria au kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja kwenye vitambaa wanavyotumia kuvaa manahodha wakiwa uwanjani asante sana Qatar.
Kwa yote hayo mimi naungana na Qatar kwa hatua hiyo kwani haki za binadamu sio kukubali kila kitu hata kukataa pia baadhi ya vitu visivyoendana na tamaduni ya nchi au jamii husika pia ni haki za binadamu ikumbukwe Qatar hawajakataza harakati za mapenzi ya jinsia moja bali hawataki hizo harakati katika nchi yao wakitoka Qatar waende nchi zinazoruhusu, mambo hayo nje ya Qatar kumbuka kila nchi ina sheria na kanuni zake wao Qatar wamekataa kuunga mkono kwenye suala hilo naona wadau wanalalamika sana wakati huo raisi wa shirikisho la mpira duniani akiwaonya pombe na vyote wanavyolalamika sio sehemu ya mpira asante sana Qatar.
NB:HATA KUKATAA VITU VISIVYOENDANA NA TAMADUNI ZA NCHI YAKO PIA NI HAKI ZA BINADAMU ASANTE SANA QATAR MUNGU AWE NANYI SIKU ZOTE.