Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Gambo sikumfukuza Ukuu wa Mkoa bali aliniomba akagombee Ubunge baada ya kuona Arusha inakwama

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Gambo sikumfukuza Ukuu wa Mkoa bali aliniomba akagombee Ubunge baada ya kuona Arusha inakwama

Katika wasukuma nafikiri huyu jamaa ni muongo no.1
FB_IMG_1603457367241.jpg
 
2018" Sijawahi fika Uraya wara Marekani na sina mpango wa kwenda"

2020 "Masters nirifanyia uraya Salford pale na Marekani na Canada nirifika mpaka niripewa kuwa co-chairman"

Cc:Tanzania ya Viwonder& Matokeo Chanya
 
Mkuu we unashauri Nini kifanyike ili vyama vya upinzani viweze kuishinda CCM pamoja na vikwazo vingi vilivyopo?
1. Elimu iongezeke, hususan elimu ya uraia kwa watu wengi zaidi. Mtaji wa CCM ni ujinga wa Watanzania wengi.

2.Watu waache utamaduni wa "hewala, hewala". Hata ukiwa na elimu, ukiwa mwoga hutaweza kuuondoa mfumo dhalimu.

3.Wanaotaka mabadiliko wamaanishe hilo kwa kweli. Wao wenyewe waanze kuishi kwa utamaduni wa kidemokrasia na kupenda mawazo mbadala. Siyo mtu analalamikia udhalimu wa CCM isivyo na demokrasia, wakati nyumbani yeye baba akishasema jambo halina mjadala. Au chama cha upinzani anakiendesha kama familia yake binafsi.

4. Vyama vya upinzani viache kuwa vyama vya msimu wa uchaguzi.Nimeshangaa sana upinzani umekubali kunyamazishwa na Magufuli miaka yote hii.Hususan katazo la kufanya mikutano ya hadhara ambalo liko kinyume na katiba. Kama wapinzani wameshindwa kupinga hili, nawaona bado sana hawajajizatiti kuiondoa CCM.

5. Tuandae watoto na vijana wanaokua sasa kukua katika utamaduni wa kuukataa ujinga bila tahayari.Kwa sasa naona kama na wao tayari wanaondolewa kutoka kwenye "kizazi cha kuhoji" na kupelekwa kwenye "kizazi cha hewala hewala".

6. Vyama vya upinzani vijizatiti zaidi kimataifa kuchukua uzoefu sehemu nyingine na kutengeneza urafiki na network kubwa za kimataifa zitakazosaidia kuleta maendeleo chanya bila kuleta hofu ya siasa zetu kutawaliwa na watu wa nje. Kuna mitandao inayojulikana na kuheshimika kama vile Amnesty International, The Committee To Protect Journalists, Human Rights Watch etc inafanya kazi kubwa na nzuri kumulika serikali dhalimu, lakini sioni kama wapinzani wetu wanazitumia hizi taasisi vizuri.

7. Vyama vya upinzani bado sana havijatumia mitandao ya kijamii kujitangaza. Presence ya chama kama CHADEMA Youtube, Twitter, au hata JF ni ndogo sana kulinganisha na ukubwa wa chama. Mitandao inasaidia sana kupasha habari watu wengi kwa wakati mfupi sana. Upinzani bado unacheza kwenye hili.

8.Vyama vya upinzani vinatakiwa kuonesha mifano ya shughuli za kiuchumi. Sio kupiga siasa za midomo tu.Yako wapi mashamba ya vyama vya upinzani? Yako wapi maduka yao? Iko wapi miradi ya kusaidia ajira kwa vijana? Wapinzani wakianzisha vitu hivi, humo humo kwenye miradi kuna nafasi ya kuongeza wanachama na kutanua wigo wa kueneza sera kwa wananchi, tena kwa kuonesha mifano, si maneno tu.Waswahili wanasema "Maneno matupu hayavunji mfupa". Waingereza wanasema "Action speaks louder than words".

9. Wapinzani wanatakiwa kuwashawishi watumishi wa umma, hususan vyombo vya dola, kwamba wao hawana ugomvi nao, wanataka kuitoa serikali ya CCM tu. Vyombo vya dola vinatakiwa kufanya kazi pamoja na wapinzani, si kudhibiti wapinzani. Vikidhibiti wapinzani ushahidi uchukuliwe na washitakiwe.

10.Vyama vya upinzani vijizatiti zaidi kupanga mkakati wa kisheria kuhakikisha haviibiwi kura. Hii ni pamoja na mabadiliko ya katiba, kuongeza teknolojia, kuongeza waangalizi wanaoheshimika kutoka nje, na kuongeza kujitambua miongoni mwa wananchi.

Kuna mengi sana, ila kwa leo niishie hapa.
 
Mwanasiasa ni mwanasiasa ...
 
Ukiachana na uongo wa Meko wa mchana kweupe, hivi huyo Gambo aliyeshindwa kuiokoa Arusha akiwa mkuu wa mkoa mzima leo aweze akiwa mbunge wa kajimbo kamoja?
Nikajuaa arusha nzima ni jimbo moja
 
Back
Top Bottom