Rais Magufuli: Kibamba mmejicheleweshea wenyewe maendeleo kwa kukosa mbunge sahihi huko nyuma ila sasa Mtemvu atawavusha!

CHADEMA kujitoa madarakani vifo vya kuugua kwa muda mfupi vimekuwa vingi sana ivi kwann. Warudisheni CHADEMA kwenye nyadhifa zao ili hili wimbi la vifo vya kuugua kwa muda mfupi vipungue mnasikia MATAGA?
 
Namaanisha Mwanga haijawahi kuwa na mbunge wa upinzani lakini inaongoza kwa maendeleo mkoa wa Kilimanjaro!
Haha kongwa imekuwa na mbunge ambae ni speaker. kwa muda mrefu sasa.

Ukiwa speaker inakuwa rahis kupelekea matatizo ya jimbo lako kwa rais.

Miaka yote hii ameshindwa kurekebisha jimbo lake why?
 
Reactions: BAK
Huyu ana matatizo zaidi ya corona
 
ili nibidi nicheke sana
 
Siri za kupata kura zote kumbe ulikuwa ni mtindo wa kukomba chungu cha mboga! Amewaumbua aliowapa udiwani kuwa hawakuchaguliwa na wananchi, msema ukweli ni kipenzi cha Mungu na ndugu zangu ukweli utabaki kuwa ukweli.
 
Namaanisha Mwanga haijawahi kuwa na mbunge wa upinzani lakini inaongoza kwa maendeleo mkoa wa Kilimanjaro!
Acha uongo ndugu yangu.
Jimbo la Mwanga huenda ndio jimbo duni zaidi kimaendeleo katika mkoa wa Kilimanjaro.

Jaribu kutembelea mkoa wa Kilimanjaro ndio utaelewa vizuri.
Mimi nilitembelea mwishoni mwa 2020 kuingia 2021, nilichokiona Kilimanjaro ni kitu tofauti sana, spirit ya maendeleo wanayo kabla hata ya kupata uhuru, na kuna mahali pengi huko kwao nilikutana na wenyeji wanaoamini kuwa kupata Uhuru kwa Tanganyika kulipunguza sana kasi ya maendeleo ya Kilimanjaro, na CCM ndio kongwa la umaskini.

Hao jamaa wa Kilimanjaro wanaichukia CCM kuliko hata shetani.
 
Sasa mbona wabunge wote ni CCM?

Au wanachukia nini?!!!
 
..huyu Mzee ni MUONGO.

..kuna majimbo kibao hajawahi kuchagua wabunge wa chadema lakini yako hoi bin taabani.

..inawezekana kipindi cha 2015 to 2020 serikali ilikuwa ikikwamisha maendeleo ya Kibamba ili ionekane mbunge aliyechaguliwa hafai.
 
Rais Magufuli amesema Kibamba wamejicheweshea wenyewe maendeleo kwa kushindwa kuchagua mbunge sahihi huko nyuma ambaye kwa muda wote amefanikisha kujenga km 5 tu za barabara ya lami.
Kwani ni kazi ya mbunge kujenga barabara. Kama ndivyo mbona hamuachii huyu mbunge wake wa sasa akajenga hizo barabara za lami. Lugha hii ya kibaguzi ningemshauri rais ajirekebishe.
 
Hatari sana... msemo wa maendelea hayana chama ni wa kinafiki sana...
 

John Pombe Joseph Magufuli πŸ’£πŸ’£πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Huwa nashindwa kuelewa kichwa cha Rais Magufuli huwa kinafanyaje kazi! Mbona kuna majimbo hawajawahi kuchagua mbu mbunge kutoka upinzani lakini ni maskini wa kutupwa?
 
Mbunge ana Budget ya maendeleo??
 
Ubaguzi wa dhahiri unaonyeshwa na baba mwenye nyumba.

Inaonekana pia majukumu ya mbunge hayafahamiki sawa sawa kwa baba mwenye nyumba.

SUALA la maendeleo nalo linaonekana ni hisani ya baba mkubwa na siyo jukumu lake kwa mujibu wa katiba.

Baba anapaswa kuwaunganisha watz na siyo kuwagawa kwa misingi ya KIIMANI, KISIASA, KIUCHUMI nk kama anavyofanya.

Hapa napata majawabu kwa nn watz WENGI walifurahia kuzuiwa kwa NDEGE yao kule AFRIKA KUSINI na CANADA

Very disappointed with these kinds of words from our beloved father
 

Attachments

  • IMG-20200630-WA0001.jpg
    37.8 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…