Rais Magufuli, umewadhalilisha sana wanawake weusi nchini

Wewe ni cheusi kweli? Hebu weka picha yako tuuone weusi wako mataga wewe
Mimi hapa mweusi na sijaumia chochote
Labda Kama wee mtoa mada umeumia pole Sana mwanamke mwenzangu

Tena mwisho akasema i mnajua Tena wasukuma!!!!
Alimaanisha wasukuma wanapenda wanawake weupe na aalitania
 
Au huyu ndugu ana duka la mikorogo labda atuambie ili Tujue moja
 
Mzee baba anatania hivyo mbele ya halaiki ya watu wazima na watoto, vipi huyo cheupe akiingia ofisini kwake halafu wakae wawili tu hata mfanya kweli?

Eeeeeh Mungu walinde wake za watu dhidi ya mbwa mwitu wabaya
 
Watu tuko tofauti, tunatakiwa kuishi kwa kutumia standard code of conduct. Nimezaliwa porini, tunajisaidia vichakani, nikifika mjini nikianza kutafuta vichaka nitajinyea au kuloanisha nguo kwa mkojo.
Mtu wa miaka 61 huwezi kumbadilisha. Cha muhimu ni kumfahamu namna anavyobadilika kimaongezi.

Hakuna mkamilifu chini ya jua.
 
Yaaani watu mna shida nyie. Hivi Rais pale aliongea kwa utani tu tayari mmelibeba. Binadamu bhana ni shida sana

Au mnafikiri kwa vile ni Rais basi haruhusiwi kufanya utani?

Acheni ushamba kila kitu mnakishikia bango
Yeye atutanie sisi tusimtanie!
 
Kwahiyo tulia hawezi kusikilizwa mana sura yake anafanana na meko
 
Weka mpaka, sema kakufanyia mambo mengi mazuri. Wengi wananchi hakuna ambaye hajaguswa na rungu la Magufuli. Tumbuatumbua, timua wenye vyeti fake(akiwaacha majeshi, wabunge na wateuli kama kina Makonda), teuzi za ukabila, vunja nyumba za watu bila fidia, vurugu za korosho na tumbaku, pombe za viroba, kuingilia Sheria ya vileo (muda wa kufungua bar), kuingilia uhuru wa vyombo vya habari na mahakama, wasiojulikana kufanya yao, polisi kuruhusiwa kuchukua hela ya kiwi nk mk.
 
Wana DSM wanakula sementi,kokoto na nondo? Wana DSM si wana Kongwa.
 
Yaaani watu mna shida nyie. Hivi Rais pale aliongea kwa utani tu tayari mmelibeba. Binadamu bhana ni shida sana

Au mnafikiri kwa vile ni Rais basi haruhusiwi kufanya utani?

Acheni ushamba kila kitu mnakishikia bango
Utakuwa mwanamke mweupe wewe si bure....[emoji41]
 
Kwa kuwa kila mtu ana tabia yake basi ndio uishi na mwizi mtaani kisa tu watu hatufanani?
Uishi na mbakaji kisa tu kila mtu na tabia zake?
Uishi na mchawi kisa tu ni kila mtu na maisha yake?
Uishi na muuaji jirani kisa tu kila mtu kaumbwa na hulka zake?
Ikifikia hatua hiyo,wewe si mtu hai tena,bali ni maiti inayoishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…