Rais Mstaafu Jakaya Kikwete: Msijaribu Kuchanganya Dini na Siasa Hata Kidogo
shida inakuja, wanasiasa wanasema tusichanganye siasa na dini ili kutunyamazisha wao wapate uchochoro wa kupiga pesa, ndio maana ni matajiri kweli kweli. wanawanyamazisha, ukijaribu kuongea wanasema unaleta udini na wao wanapitia uchochoro huohuo. TEC wamekuja mazima kutetea maslahi ya Taifa baada ya kuona upande mwingine umesherehekea kwasababu mwarabu ndio anakuja kuwekeza hivyo hata kama mwarabu atatunyonya haina shida kwasababu ni mwenzao. ndugu wa mwislam ni mwislam hata kama anafanya makosa.
Kitu Cha Ajabu Wakiristo wao huangalia issue bila kujali Rais ni wa dini Gani ONA HII TAARIFA HAPA CHINI

Tarehe 25 December 2017, Askofu Zakaria Kakobe akiwa kanisani kwenye ibada ya Christmas, katika kanisa la FGBF Mwenge jijini Dar es Salaam, alinukuliwa akituma salamu kwa Rais wa JMT, Dkt. John P. Magufuli.

"Rais John Pombe Magufuli, nawe unatakiwa kutubu leo. Unaposherekea sikukuu ya Christmas, ili uridhiwe na Mungu unatakiwa nawe utubu".

"Leo ni siku ya watawala wa Tanzania kutubu. Leo tumeanza kuona misingi ya amani ya nchi yetu ikitikiswa. Amani iliyojengwa kwa gharama kubwa na waasisi wetu. Tumeanza kuona nchi hii ni ya chama kimoja na huu ni uovu. Mungu mwenyewe anaheshimu sheria basi kama na sisi tumeweka sheria tunapaswa kuheshimu sheria tulizojiwekea wenyewe. Hii si nchi ya chama kimoja. Kama mnataka kubadilisha si mbadilishe tu mara moja kupitia wabunge wenu wa CCM, si mko wengi?".

"Sheria ni lazima zizingatiwe! Na kwa hili nitapiga kelele mpaka Mlima Kilimanjaro. Huwezi kusema wewe huwezi kusemwa, wewe ni nani? Mungu anasemwa vibaya sembuse wewe?".

"Mungu mwenye nguvu kuliko Magufuli, ana nguvu kuliko majeshi yote ya nchi, lakini anatukanwa na bado hatumii majeshi yake. Hata wewe unaweza ukawa mvumilivu"

Baada ya kauli hii, Askofu Kakobe alipokonywa passport yake, alihojiwa uraia wake na aliandamwa na TRA kwa madai ya kodi.

Huyu alikuwa ni kiongozi wa dini ya Kikistro na alimkosoa Mkristo Magufuri

Huu ulikuwa udini? Wa dini gani?

Askofu wa Catholic Jimbo la Rulenge (Severine Niwemugizi) alimkosoa mkatoliki mwenzake Magufuri juu ya haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano.

Aliishia kupokonywa passport na kuhojiwa uraia wake.

Alikuwa mdini? Akishabikia dini gani?

Nachukizwa sana na yeyote ambaye atataka kutugawa kwa misingi ya kidini.

Kukosoa haiwezi hata mara moja kuwa udini.

Kuwa kiongozi wa dini hakumnyimi haki kiongozi huyo kupata haki zake za kikatiba kutoa maoni juu ya mambo ya nchi yake kama anavyoweza kufanya Mwalimu, daktari, mkulima au mfugaji.

Tukemee wale wote wanaotaka kujificha kwenye udini pale tu wanapokosolewa kwa makosa waliyoyafanya wenyewe.
 
Kama vipi tuchapane tu, kila mtu arudi kijijini kwao.
Baada ya mnyukano tutaheshimiana zaidi na tutakuwa majirani wazuri.
Naiona project Tanganyika ikifeli kabla ya kuanza, waislam na watu wa mwambao wa pwani ya Tanganyika wakiwa na dola yao ya kiislam, jirani na jamhuri ya kidemokrasia ya kikiristo.
Nadhani wale ambao hatujakwenda vijijini kwetu ndio muda muafaka wa kuandaa mazingira ya kureja mazima.
Kitanuka muda si mrefu na wakukizima hakuna.
 
Waache kuapa kwa vitabu vya Dini bungeni
Niliweka Uzi hapa Leo kuwa tunakopelekwa na hizi dini zetu UTANZANIA WETU NA UMOJA UTAVUNJIKA. nikatoa maoni kuwa kwani kama tunavyosema Serikali Haina dini, tusianzie na VIONGOZI wetu wakati wanaapa badala ya KUTIMIA Biblia au Quran basi watumie Katiba kwani hiyo ndyo ya kwanza wanayotakiwa kuilinda. KUTIMIA hivyo vitabu unakuwa ndiyo MWANZO wa kuingia Dini kwenye siasa na hatimaye kutugawanya watanzania
 
Ni rahisirahisi sana kwa watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri kama huyo bwana kuishia kusema maneno kama hayo aliyoyasema, lakini ukimuuliza aeleze tuhuma anazoziwasilisha hana uwezo wa kueleza chochote.
Ni uwezo mdogo au ni amesema kwa sababu na yeye ni mnufaika tarajiwa wa li mkataba libovu?!
 
Ifikie mahali tutambue kuwa DINI ni imani na kila mmoja ana yake....

Watanzania wanahitaji kilimo...hakuhusiani na dini!

Watanzania wanahitaji amani na usalama.... hakuhusiani na dini!

Watanzania wanahitaji maji safi... hakuhusiani na dini!

Watanzania wanahitaji afya bora.... hakuhusiani na dini!

Watanzania wanahitaji barabara na miundombinu ya mawasiliano.... hakuhusiani na dini!!

Watanzania wanahitaji mazingira bora ya biashara.....hakuhusiani na dini!!

Watanzania wanahitaji michezo.... hakuhusiani na dini!!

Watanzania wanazipenda Simba na Yanga.... hakuhusiani na dini!!

Wasomi wanahitaji GRANTS na mikopo ya HESLB.... hakuhusiani na dini!!!

Ni kiburi tu cha baadhi ya watu kujifanya kuwa wako juu ya wengine kwa kuwa wanaamini dini zao.....

Ni dharau tu kuwabagua wasiokuwa na dini na kuwafanya daraja la pili la kiraia....UJINGA+KIBURI+UPUMBAVU+BRAINWASHING

Tanzania haisimami kwa sababu ya dini za watu .....

Dunia inakwenda kasi mno....ni kwanini baadhi yetu wanadini tunaufufua ujinga wa karne 20 zilizopita ?!!! [emoji15][emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Wenye akili husema "NEVER GIVE WISDOM TO UNWORTHY BECAUSE ITS UNJUST TO THE KNOWLEDGEABLE"

Kipenzi rais wetu mh.SSH hakuchaguliwa KIDINI....hayuko kwa ajili ya DINI.....dini amewaachia MASHEIKH na MAASKOFU.......

Tanzania tunahitaji wawekezaji....

Wawekezaji hao wawe waarabu ,wahindi ,wachina ama wazungu....

TEC wasitucheze NGOMA wanazozijua wao ndani ya kuta zao......


#TanzaniaTaifaLaKijamaa[emoji120]

#TanzaniaHatutakiUdini[emoji120]

#MwenyeKutakaKutugawaKidiniAshughulikiweVyemaTu[emoji120]

[emoji120] Tanzania DaimaDumu[emoji120][emoji120]
Pumba!
 
"Napenda kuchukua nafasi hii kukumbushana kuhusu tunu nyingine muhimu nayo ni kutokuchanganya dini na siasa. Tukiivunja tunu hii gharama yake tutaiona, na kama kuna viongozi wa dini wanataka kutuelekeza kuitumia dini kwa manufaa ya kisiasa, na kama kuna viongozi wa siasa wanataka kuitumia dini kwa manufa yao ya kisiasa, nawaombeni ndugu zangu tuwanyanyapae.

"Siku ikifika ambapo uwanachama wa chama cha siasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na chama cha siasa kinachofuata ndio mwisho wa nchi yetu, mtakuwa na vyama vya siasa vya wakristu, waislamu, walokole nk. Kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, kiserikali, utawala kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari, halkadhalika watu kuyatazama masuala ya dini kwa mtazamo wa siasa za vyama vyao si jambo lenye afya kwa taifa letu.

"Yote mawili yataathiri umoja na kutishia amani, usalama na utulivu tunaoufaidi hivi sasa. Mfano Zanzibar walifika mahali waisilamu wanamuona shehe ambaye ni mfuasi wa chama ambacho sio chake sio shehe sawa sawa, kwahiyo wakienda kusali kama shehe ni msuasi wa CUF wanangoja amalize kusalisha, halafu anaingia shehe wa waislamu na wafuasi wake.

"Nawaambia vitu halisi na ndio maana nilipokuwa Rais nilishughulika sana pale na kupata muafaka, niliahidi kwenye hotuba yangu ya kwanza ya Bunge 2005 Dec 30, kwamba nitafanya kila ninaloweza tujenge muafaka Zanzibar, haukuwa rahisi. Mkutano ule tuliufanyia Butiama NEC, ilikuwa moja ya kikao kigumu kwelikweli, lakini nikasema pamoja na ugumu wote lazima hapa tuvuke. Tukafika mahali nilipoona mambo yamekuwa makali, nikasema twendeni kwanza tukale, tulipokuwa tunakula ndio tukawa tunaweka mikakati ya namna gani tunalimaliza hili jambo. Tukajipanga nani ataanza kuzungumza, tukakubaliana kwamba tutakwenda Zanzibar kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na ndio imetusaidia Zanzibar tuna mazingira ya utulivu mpaka sasa, tungekwenda na utaratibu ule ule wa zamani tusingefika.

"…Tukianza kuchanganya dini na siasa tukageuza mimbari za dini na madhabahu kuwa sehemu ya kuhubiri kwishilia mbali nchi yetu. Lakini baba wa taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa. Nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni ya jicho letu. Tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo wa aina hii iwe kwa siri au kwa Dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya."


Kikwete ameyasema hayo leo 20/8/2023 katika ufunguzi wa jengo Kanisa la Kiadventisti Wasabato Mara.
Huyu mzee ndio mwizi, namba moja kwa sasa, aulizwe gesi yetu ya mtwara iliishia wapi
 
Hiki kizee kinafiq sana amesahau alivyopigiwa kampeni misikitini 2010 mbona hakukemea? Mbona Pengo na Kilaini walipompigia debe kuwa ni chaguo la Mungu hakusema kitu? Mbona taasisi za kiisllam zilipoupigia debe mkataba wa DP World na kuisakama Chadema kwa kukosoa mkataba huo alipiga kimya? Ufisadi mwingi na wa kutisha ulifanyika kipindi chake cha utawala hadi wanaccm walikuwa wanazomewa mitaani kama wezi? Mzee kaa kimya umetukosea mengi sana Watanzania.
 
Alikuwa aliongea Leo huko Mara alikoalikwa kama mgeni Rasmi kwenye sherehe ya ufunguzi wa jengo la ibada la Kanisa.

My Take
Naunga mkono hoja,TEC na wachochezi wengine wakemewe na waonywe.

=====

"Tukianza kuchanganya dini na siasa, tukageuza...madhabahu ndio mahali pa kuhubiri siasa za vyama vya siasa, kwishiria mbali nchi yetu...lakini Baba wa Taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa, nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni za jicho letu tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo vya aina hii iwe kwa siri au kwa dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya" Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Jakaya Kikwete wakati akizindua kanisa la SDA Rorya mkoani Mara, leo Agosti 20, 2023.

View attachment 2722951
Kwani kikwete ni nani, mbona twiga waliuzwa akiwa Rais, escrow, richmond nk.
Anataka uuzaji wa rasilimali za nchi watu wakae kimya.
Hata hivyo katika waraka wa TEC hakuna siasa zaidi ya viongozi kuonya uuzaji wa rasilimali za nchi.
Ni haki yao kama raia kulingana na katiba.
Hawakusema masuala ya kisiasa. Syo wafuasi wa chama chochote, hawakupiga kampeni.tatizo liko wapi
 
Kwani kikwete ni nani, mbona twiga waliuzwa akiwa rais,escrow richmond nk.

Anataka uuzaji wa rasilimali za nchi watu wakae kimya.
Hata hivyo katika waraka wa TEC hakuna siasa zaidi ya viongozi kuonya uuzaji wa rasilimali za nchi.
Ni haki yao kama raia kulingana na katiba.
Hawakusema masuala ya kisiasa. Syo wafuasi wa chama chochote, hawakupiga kampeni.tatizo liko wapi
Unajua hawa viongozi wanajiona kama wao ndiyo miungu ya duniani hapa.

Wanajiona kila maauzi wanayofanya ni sahihi kln ukweli ni kuwa kuna wananchi wana akili kuliko wao.
 
Hiki kizee kinafiq sana amesahau alivyopigiwa kampeni misikitini 2010 mbona hakukemea? Mbona Pengo na Kilaini walipompigia debe kuwa ni chaguo la Mungu hakusema kitu? Mbona taasisi za kiisllam zilipoupigia debe mkataba wa DP World na kuisakama Chadema kwa kukosoa mkataba huo alipiga kimya? Ufisadi mwingi na wa kutisha ulifanyika kipindi chake cha utawala hadi wanaccm walikuwa wanazomewa mitaani kama wezi? Mzee kaa kimya umetukosea mengi sana Watanzania.
Bado anatoa vitisho kwa wakatoliki kuwa wasijiingize kwenye siasa wakati wao ndiyo huwa wanageuza misikiti kuwa sehemu ya kufanyia mikutano.

Unafiki ni kitu kibaya sana katika maisha.
 
Back
Top Bottom