Rais Mstaafu Jakaya Kikwete: Msijaribu Kuchanganya Dini na Siasa Hata Kidogo
Alikuwa aliongea Leo huko Mara alikoalikwa kama mgeni Rasmi kwenye sherehe ya ufunguzi wa jengo la ibada la Kanisa.

My Take
Naunga mkono hoja,TEC na wachochezi wengine wakemewe na waonywe.

=====

"Tukianza kuchanganya dini na siasa, tukageuza...madhabahu ndio mahali pa kuhubiri siasa za vyama vya siasa, kwishiria mbali nchi yetu...lakini Baba wa Taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa, nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni za jicho letu tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo vya aina hii iwe kwa siri au kwa dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya" Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Jakaya Kikwete wakati akizindua kanisa la SDA Rorya mkoani Mara, leo Agosti 20, 2023.

View attachment 2722951
1 - Suala la bandari si suala la siasa ni uchumi na ustawi wa watu. ndiyo sababu watu wanaishutumu serikali kuingia mkataba mbovu. hawashutumu chama cha mapinduzi. Na uchumi na ustawi wa watu huwezi ukamzuia mtu yeyote.

2-Yeye Kikwete, alikwenda hapo kwenye jukwaa la dini kama nani, mwanasiasa au mwinjilisti? kwa nini yeye kama mwanasiasa anakubali kuingia kwenye masuala ya dini, kwa ni ukialikwa lazima uende?
 
Huyo mzee Mkwere anazingua.
Na alipaswa kuwakemea mkewe na kijana wake waache tamaa ya uongozi wa kisiasa maana hawana sifa hata moja zaidi ya kuhonga ili wawe viongozi kama alivyohonga yeye awe rais.

Nyerere alimkemea huyo mkwere akimuita mhuni anayetamani kuingia ikulu 😂😂
 
Tufanye uchaguzi haraka kwa amani ya nchi.
Kwako amani inakwepo akiongoza nani?Kwangu nina amani kubwa sana nchi kuongozwa na mtu kama Samia.Huko tulikotoka msemaji alikuwa moja tu nchi nzima,mauaji kila kona!Sasa hivi mambo safi.Watu wanajadili mkataba wa DP WORLD kwa starehe zote
 
Hawajui kuwa serikali ni utumishi WA Mungu. Mungu ni utu, haki, kweli, n.k. JE KUNA SERIKALI INAYOINGIA MADARAKANI KWA AJILI YA KUFANYA UOVU? NA IKAWAAHIDI WANANCHI KUWA WATAFANYA UOVU ILI WACHAGULIWE? NA WANANCHI WAKAKUBALI KUWACHAGUA KWA UOVU ULIOAHIDIWA? KAMA SIVYO BASI KUTENGANISHA MAKANISA/DINI NA SIASA NI KUFICHA UDHALIMU NA WACHACHE WAENDELEE KUNEEMEKA KWA MTAJI WA DINI ISIHUSIKE NA SIASA. SIASA NI UTARATIBU WA MAISHA YA NCHI. KWA NINI WATU WAJITENGE NAO? SIASA IWE YA WATU WOTE. ILA SERIKALI NDIYO HAINA DINI/ MAKANISA. ILA WATU NDIWO WENYE DINI/ MAKANISA.
 
RAI! RAI! RAI!
Nadhani serikali kwa njia ya wataalamu wa magonjwa ya akili waweke mpango wa kitaifa wa kupima watu magonjwa ya akili. Na watu wote tupimwe. Kuna dalili kwamba kuna wagonjwa wengi wa akili kuliko tunavyodhani na wengine si ajabu wako kwenye nafasi nyeti. Naona tukiongea hatuelewani hata katika mambo madogo ya wazi na ya kawaida. Tena lugha chafu, uongo, na za matusi zimeongezeka hadharani.
 
Askofu Gwajima alishiriki vikao viwili kupitisha Mkataba wa Bandari - Bunge na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. Pia, ameshiriki mikutano ya hadhara na kampeni kadhaa za CCM kuunga mkono mkataba. Wakati anashiriki vikao hivyo, hawakuona kuwa anachanganya dini na siasa.

Lakini sisi tunapotoa hoja na matamko kupinga na kutahadharisha juu ya mkataba wa bandari, lakini vigogo wa CCM wanakuja juu na kuanza kutupiga madongo majukwaani kutuonya kuwa tunachanganya dini na siasa.

Hakuna utawala uliowahi kudumu duniani hasa kama viongozi wameanza kuwa wanafiki kwa kuwa wanafiki huukataa na kuuchukia ushauri hata ule ambao una lengo la kuuokoa utawala huo usianguke.

Waache waendelee kutumia majukwaa kupiga madongo maaskofu wanaoonya, wanaoshauri na kukemea kwani CCM walio wengi hawajui kuwa meli yao imeanza kutoboka. Wanadharau boti za wokozi zinazopita kandokando ya meli yao kubwa ya kifahali iliyoanza kutoboka. Muda wa kuzama ukitimu watapiga kelele ili kutafuta msaada wasiweze kupata watu wa kuwaokoa.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 21 Agosti 2023; 02:38 Asubuhi
 
Rais Mwinyi ni rais tofauti na watangulizi wake, rais Mwinyi yeye amejikita sana kuendeleza uisilamu kwani hivi sasa amekuja na ajenda ya " mwaka wa kiisilamu" kuuingiza kwenye kalenda, huko nyuma aliwahi kuja na serikali kuanzisha mfuko wa mahujaji.

Je, ushauri wa Kikwete kuhusu kuchanganya siasa na dini unawezekana wakati viongozi wa CCM ndio wachanganyaji wakubwa?
 
B

Je, ushauri wa mhe. Kikwete kuhusu kuchanganya siasa na dini unawezekana wakati viongozi wa CCM ndio wachanganyaji wakubwa?
Baelezee Mwamba
 
Hawajui kuwa serikali ni utumishi WA Mungu. Mungu ni utu, haki, kweli, n.k. JE KUNA SERIKALI INAYOINGIA MADARAKANI KWA AJILI YA KUFANYA UOVU? NA IKAWAAHIDI WANANCHI KUWA WATAFANYA UOVU ILI WACHAGULIWE? NA WANANCHI WAKAKUBALI KUWACHAGUA KWA UOVU ULIOAHIDIWA? KAMA SIVYO BASI KUTENGANISHA MAKANISA/DINI NA SIASA NI KUFICHA UDHALIMU NA WACHACHE WAENDELEE KUNEEMEKA KWA MTAJI WA DINI ISIHUSIKE NA SIASA. SIASA NI UTARATIBU WA MAISHA YA NCHI. KWA NINI WATU WAJITENGE NAO? SIASA IWE YA WATU WOTE. ILA SERIKALI NDIYO HAINA DINI/ MAKANISA. ILA WATU NDIWO WENYE DINI/ MAKANISA.
Kwa kuongezea Viongozi wengi wakichaguliwa wanaapa Kwa kumtumia katiba na vitabu vya dini
 
Rais Mwinyi ni rais tofauti na watangulizi wake, rais Mwinyi yeye amejikita sana kuendeleza uisilamu kwani hivi sasa amekuja na ajenda ya " mwaka wa kiisilamu" kuuingiza kwenye kalenda, huko nyuma aliwahi kuja na serikali kuanzisha mfuko wa mahujaji.
Je, ushauri wa mhe. Kikwete kuhusu kuchanganya siasa na dini unawezekana wakati viongozi wa CCM ndio wachanganyaji wakubwa?
Okay, imekaaje hii. Kwani kwa Sasa Mwaka wa Kiislaamu haupo kwenye kalenda?
 
... watakuambia Zanzibar 99% ni watu wa dini hivyo kuanzisha mfuko maalumu wa kuwasaidia kwenda kutekeleza ibada ni jukumu la serikali. Tena ukizingatia rais ni wa dini hiyo hiyo huko hakuna uhusiano wowote wa kuchanganya dini na siasa.
 
Rais Mwinyi ni rais tofauti na watangulizi wake, rais Mwinyi yeye amejikita sana kuendeleza uisilamu kwani hivi sasa amekuja na ajenda ya " mwaka wa kiisilamu" kuuingiza kwenye kalenda, huko nyuma aliwahi kuja na serikali kuanzisha mfuko wa mahujaji.

Je, ushauri wa Kikwete kuhusu kuchanganya siasa na dini unawezekana wakati viongozi wa CCM ndio wachanganyaji wakubwa?
Hiyo kauli ya kikwete itakuwa imelenga upande wa tanganyika
 
Back
Top Bottom