Rais Mstaafu Jakaya Kikwete: Msijaribu Kuchanganya Dini na Siasa Hata Kidogo
Rais Mwinyi ni rais tofauti na watangulizi wake, rais Mwinyi yeye amejikita sana kuendeleza uisilamu kwani hivi sasa amekuja na ajenda ya " mwaka wa kiisilamu" kuuingiza kwenye kalenda, huko nyuma aliwahi kuja na serikali kuanzisha mfuko wa mahujaji.

Je, ushauri wa Kikwete kuhusu kuchanganya siasa na dini unawezekana wakati viongozi wa CCM ndio wachanganyaji wakubwa?
Za kuambiwa changanya na zako.....
 
Hii ya mwaka wa kiislamu tu? Vipi waliokuja na sikukuu ya mwaka mpya wa Kikristo kuwa siku ya mapumziko? Na vipi kuhusu siku ya kupeana zawadi ya mwezi wa kikristo (26 Disembal) kuwa siku ya mapumziko? Haya hayakuwa ni kuchanganya dini na siasa? Jee uliwahi kuyasemea?

Usiwarushie watu mawe ukiwa kwenye nyumba ya vioo; ni hatari kwako.
Hayo unayohoji sina jibu labda tuwaulize wapalestina kwanini huwa wanasheherekea wakati wao ni waisilamu, shida sisi tulidandia gari kwa nyuma bila kujua liendako, wapalestina na waislaeri wanapigana lakini hawahusishi dini hata siku moja wakati huko ndiko zilikoanzia.
 
Rais Mwinyi ni rais tofauti na watangulizi wake, rais Mwinyi yeye amejikita sana kuendeleza uisilamu kwani hivi sasa amekuja na ajenda ya " mwaka wa kiisilamu" kuuingiza kwenye kalenda, huko nyuma aliwahi kuja na serikali kuanzisha mfuko wa mahujaji.

Je, ushauri wa Kikwete kuhusu kuchanganya siasa na dini unawezekana wakati viongozi wa CCM ndio wachanganyaji wakubwa?
Unawaambiaje watu wasichanganye siasa na dini wakati wewe uko kwenye jukwaa la dini.

Ilipaswa abatizwe kwanza awe mwinjilisti wa dini iliyomwalika ndipo aseme hivyo.
Afuate nyayo za mzee Agrey Mwanri ambaye sasa ni mwinjilisti wa kkkt baada ya kustaafu siasa. Na hatumsikii tena.
 
Marais wenyewe kutwa makanisani halafu wanadai tusichanganye dini na siasa. Waache kwenda makanisani na misikitini Kama kweli wanammanisha.
 
Huwezi kuwazuia Watu Kuchanganya Dini na Siasa iwapo hakuna sheria inayokataza jambo hilo

Labda upelekwe Muswada bungeni ikatungwe Sheria ya kuzuia Binadamu wa Tanzania wasichanganye Dini na Siasa

Nawasilisha 😄
Basi kama ndivyo upelekwe mswada wa kufuta nadheebu ya dini zote nchini, huwezi tenganisha hivi vitu , waumini ndo wanasiasa wenyewe, mpo na hoja nyepesi sana kwenye mambo serious
 
Unawaambiaje watu wasichanganye siasa na dini wakati wewe uko kwenye jukwaa la dini.

Ilipaswa abatizwe kwanza awe mwinjilisti wa dini iliyomwalika ndipo aseme hivyo.
Afuate nyayo za mzee Agrey Mwanri ambaye sasa ni mwinjilisti wa kkkt baada ya kustaafu siasa. Na hatumsikii tena.
Mwanri aliteuliwa kuwa balozi wa pamba.
 
Ni Tanganyika ipi ilikuwa na udini wala ukabila! Toka kabla ya uhuru shule za misheni(Katoliki) wakati huo zilichukua watoto wote bila kujali dini zao wala kulazimisha kuingia kanisa lao.
Kwa hiyo Nyerere alikuwa anakemea matatizo ambayo hayakuwepo ?

Wewe hujui kuwa Mgogoro na malalamiko ya udini na ukabila yapo dahri na dahri ?

Kuna Mijitu ina uelewa hafifu sana
 
Huwezi kuwazuia Watu Kuchanganya Dini na Siasa iwapo hakuna sheria inayokataza jambo hilo

Labda upelekwe Muswada bungeni ikatungwe Sheria ya kuzuia Binadamu wa Tanzania wasichanganye Dini na Siasa

Nawasilisha [emoji1]
Na ikiwa hivyo ujue hakuna kiongozi yeyote atakae apishwa kwa imani yoyote ile yaani akisha teuliwa ni ofisi moja kwa moja.
Maana kitendo cha kiapo tayari dini na siasa [emoji2][emoji2]
 
Huo muswaada wasisahau kuweka kipengele Cha wanasiasa wasiape kwa vitabu vya Dini.
Bali watumie katiba au ilani za vyama vyao.
 
Huwezi kuwazuia Watu Kuchanganya Dini na Siasa iwapo hakuna sheria inayokataza jambo hilo

Labda upelekwe Muswada bungeni ikatungwe Sheria ya kuzuia Binadamu wa Tanzania wasichanganye Dini na Siasa

Nawasilisha 😄
Nafikiri Tukiruhusu hili ipo siku tutatunga sheria mtu asiwaze tofauti na kiongozi 😂😂😂😂
 
Nchi yetu mambo mengi hayako straight......akifanya wa upande fulani akiwa na hoja nzito na wanaotakiwa kujibu wakakosa majibu......kurahisisha au kukimbia wajibu wao wanasingizia kukosokewa kwasababu ya imani fulani.......ni busara tukajifunza kujibu hoja Kwa hoja
Screenshot_20230821-151455.png
 
Bunge lenyewe linafunguliwa kwa dua na sala 🤣🤣🤣🤣🤣

Anayeombwa kwenye ile dua ni mungu wa akina nani kama kweli sisi ni secular state??

Tumeyataka wenyewe.
 
Hayo unayohoji sina jibu labda tuwaulize wapalestina kwanini huwa wanasheherekea wakati wao ni waisilamu, shida sisi tulidandia gari kwa nyuma bila kujua liendako, wapalestina na waislaeri wanapigana lakini hawahusishi dini hata siku moja wakati huko ndiko zilikoanzia.
Nilitarajia ujibu wewe kwani wewe ndo uloweka hoja ya Rais Mwinyi. Au ni kwasababu imekugusa wewe? Ndo pale nilipokuambia usirushie watu mawe ukiwa kwenye nyumba ya vioo. Nadhani sasa umeelewa.
 
Back
Top Bottom