Kitu Cha Ajabu Wakiristo wao huangalia issue bila kujali Rais ni wa dini Gani ONA HII TAARIFA HAPA CHINI

Tarehe 25 December 2017, Askofu Zakaria Kakobe akiwa kanisani kwenye ibada ya Christmas, katika kanisa la FGBF Mwenge jijini Dar es Salaam, alinukuliwa akituma salamu kwa Rais wa JMT, Dkt. John P. Magufuli.

"Rais John Pombe Magufuli, nawe unatakiwa kutubu leo. Unaposherekea sikukuu ya Christmas, ili uridhiwe na Mungu unatakiwa nawe utubu".

"Leo ni siku ya watawala wa Tanzania kutubu. Leo tumeanza kuona misingi ya amani ya nchi yetu ikitikiswa. Amani iliyojengwa kwa gharama kubwa na waasisi wetu. Tumeanza kuona nchi hii ni ya chama kimoja na huu ni uovu. Mungu mwenyewe anaheshimu sheria basi kama na sisi tumeweka sheria tunapaswa kuheshimu sheria tulizojiwekea wenyewe. Hii si nchi ya chama kimoja. Kama mnataka kubadilisha si mbadilishe tu mara moja kupitia wabunge wenu wa CCM, si mko wengi?".

"Sheria ni lazima zizingatiwe! Na kwa hili nitapiga kelele mpaka Mlima Kilimanjaro. Huwezi kusema wewe huwezi kusemwa, wewe ni nani? Mungu anasemwa vibaya sembuse wewe?".

"Mungu mwenye nguvu kuliko Magufuli, ana nguvu kuliko majeshi yote ya nchi, lakini anatukanwa na bado hatumii majeshi yake. Hata wewe unaweza ukawa mvumilivu"

Baada ya kauli hii, Askofu Kakobe alipokonywa passport yake, alihojiwa uraia wake na aliandamwa na TRA kwa madai ya kodi.

Huyu alikuwa ni kiongozi wa dini ya Kikistro na alimkosoa Mkristo Magufuri

Huu ulikuwa udini? Wa dini gani?

Askofu wa Catholic Jimbo la Rulenge (Severine Niwemugizi) alimkosoa mkatoliki mwenzake Magufuri juu ya haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano.

Aliishia kupokonywa passport na kuhojiwa uraia wake.

Alikuwa mdini? Akishabikia dini gani?

Nachukizwa sana na yeyote ambaye atataka kutugawa kwa misingi ya kidini.

Kukosoa haiwezi hata mara moja kuwa udini.

Kuwa kiongozi wa dini hakumnyimi haki kiongozi huyo kupata haki zake za kikatiba kutoa maoni juu ya mambo ya nchi yake kama anavyoweza kufanya Mwalimu, daktari, mkulima au mfugaji.

Tukemee wale wote wanaotaka kujificha kwenye udini pale tu wanapokosolewa kwa makosa waliyoyafanya wenyewe.
 
Kama vipi tuchapane tu, kila mtu arudi kijijini kwao.
Baada ya mnyukano tutaheshimiana zaidi na tutakuwa majirani wazuri.
Naiona project Tanganyika ikifeli kabla ya kuanza, waislam na watu wa mwambao wa pwani ya Tanganyika wakiwa na dola yao ya kiislam, jirani na jamhuri ya kidemokrasia ya kikiristo.
Nadhani wale ambao hatujakwenda vijijini kwetu ndio muda muafaka wa kuandaa mazingira ya kureja mazima.
Kitanuka muda si mrefu na wakukizima hakuna.
 
Waache kuapa kwa vitabu vya Dini bungeni
Niliweka Uzi hapa Leo kuwa tunakopelekwa na hizi dini zetu UTANZANIA WETU NA UMOJA UTAVUNJIKA. nikatoa maoni kuwa kwani kama tunavyosema Serikali Haina dini, tusianzie na VIONGOZI wetu wakati wanaapa badala ya KUTIMIA Biblia au Quran basi watumie Katiba kwani hiyo ndyo ya kwanza wanayotakiwa kuilinda. KUTIMIA hivyo vitabu unakuwa ndiyo MWANZO wa kuingia Dini kwenye siasa na hatimaye kutugawanya watanzania
 
Ni rahisirahisi sana kwa watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri kama huyo bwana kuishia kusema maneno kama hayo aliyoyasema, lakini ukimuuliza aeleze tuhuma anazoziwasilisha hana uwezo wa kueleza chochote.
Ni uwezo mdogo au ni amesema kwa sababu na yeye ni mnufaika tarajiwa wa li mkataba libovu?!
 
Pumba!
 
Huyu mzee ndio mwizi, namba moja kwa sasa, aulizwe gesi yetu ya mtwara iliishia wapi
 
Hiki kizee kinafiq sana amesahau alivyopigiwa kampeni misikitini 2010 mbona hakukemea? Mbona Pengo na Kilaini walipompigia debe kuwa ni chaguo la Mungu hakusema kitu? Mbona taasisi za kiisllam zilipoupigia debe mkataba wa DP World na kuisakama Chadema kwa kukosoa mkataba huo alipiga kimya? Ufisadi mwingi na wa kutisha ulifanyika kipindi chake cha utawala hadi wanaccm walikuwa wanazomewa mitaani kama wezi? Mzee kaa kimya umetukosea mengi sana Watanzania.
 
Kwani kikwete ni nani, mbona twiga waliuzwa akiwa Rais, escrow, richmond nk.
Anataka uuzaji wa rasilimali za nchi watu wakae kimya.
Hata hivyo katika waraka wa TEC hakuna siasa zaidi ya viongozi kuonya uuzaji wa rasilimali za nchi.
Ni haki yao kama raia kulingana na katiba.
Hawakusema masuala ya kisiasa. Syo wafuasi wa chama chochote, hawakupiga kampeni.tatizo liko wapi
 
Unajua hawa viongozi wanajiona kama wao ndiyo miungu ya duniani hapa.

Wanajiona kila maauzi wanayofanya ni sahihi kln ukweli ni kuwa kuna wananchi wana akili kuliko wao.
 
Bado anatoa vitisho kwa wakatoliki kuwa wasijiingize kwenye siasa wakati wao ndiyo huwa wanageuza misikiti kuwa sehemu ya kufanyia mikutano.

Unafiki ni kitu kibaya sana katika maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…