Kwa mara ya kwanza nimeamini CCM safari hii imekutana na mpini mgumu muno na isiposhtuka 2025 inaweza kuondolewa madarakani, kosa kubwa walilolifanya ni kuingiza vyombo vya ulimzi na usalama kwenye siasa wakiamini kwamba vitawalinda.

Waraka wa TEC unataka kuleta sura mpya ya siasa na utawala Tanzania.

Kitendo cha JK kutoka na kutoa hotuba Kali tena akiwa siriasi kuhusu kutenganisha dini na siasa kimenipa wasiwasi mkubwa juu ya kile kinachoendelea kwa sasa ndani ya serikali.

Kumbukeni huyu Rais mstaafu, kwahiyo anafahamu mambo mengi ambayo hata sisi watu wa kawaida hatufahamu.

Je hotuba hii ilikuwa ni kujibu Waraka wa TEC uliosomwa leo katika misa zote za kanisa katoliki?

Kuna kitu nyuma ya pazia juu ya DP world ambacho sisi kama raia hatukifahamu, haiwezekani TEC wachukua uamuzi huu, uwekezaji huu si wa kawaida inawezekana bado kuna vitu vingi hatuvifahamu kuhusu ili suala la bandari.




View: https://twitter.com/Jambotv_/status/1693233897662714215?t=UO0XpE-6d2yEkAmoQFCkig&s=19
 
Leo ndio amekumbuka maneno ya baba wa taifa?

Kukemea rushwa iliyosababisha bandari zetu zikatolewa bure milele kwa mwarabu hakuwezi hata siku moja kuwa kuchanganya dini na siasa.

Hayo maneno kuchanganya dini na siasa hutumiwa na wanasiasa ili wapate uwanja mzuri wa kufanya michezo yao haramu kwa manufaa yao, na sio manufaa ya watanganyika.

Siasa inahusisha watu, na dini zinahusisha watu hao hao, hawa hawatenganishiki, tendeni mema kwa wananchi wenu mkae kwa amani, kinyume na hapo lazima muambiwe ukweli.
 
Maji yameanza kuwazidi watatoka wote sasa.
 
Wacha viumane. Maandamano na mabadililo makubwa ya uongozi nchini Tunisia zaidi ya miaka kumi iliyopita yalianza baada ya kijana mmoja muuza mbogamboga na matunda kwenye mkokoteni kuchoshwa na manyanyaso ya polisi na mgambo wa jiji na kuamua kujilipua moto hadharani.
 
Huyu angetumia hicho kichwa kututoa kwenye mkwamo wa DP world. Siyo kurukia ndinga kwa mbele baada kuona TEC wametimiza wajibu wao.
Jakaya tunakukumbuka sana miaka ya 80 ukiwa waziri wa Mwinyi ulihudhuria Abuja conference iliokuwa na agenda ya kusilimisha africa! Ukapigiwa kelele sana. Jakaya tunakumbuka matokeo ya Abuja conference ni kisehemu cha Zenj kutaka kujiunga na OIC.
Jakaya najua mmetumana na bi mkubwa wewe ukaenda SDA na Bi Mkubwa kwa mzee sarakikya kujaribu kushawishi KKKT wasitoke na wao na tamko. Kwa KKKT najua Bi Mkubwa atagonga mwamba sababu Dk shoo Askofu wa KKKT si wa kuyumbishwa.
SIjui utafanikiwa namna gani kwa SDA tungojelee.
Upande mwingine Geodavie yule anayejiita Nabii Mkuu amekaribishwa bungeni. Hakuna cha kusafisha uchafu wa kuharibu tanganyika tuliyopewa na Muumba wetu!. Zile faranga waambie wamrudishie Mwarabu. Msaidie Bi Mkubwa kaingia kichwa kichwa kuratibu rushwa. Mwenzake ulikuwa mjanja kula na kunawa na kutosa wazembe walio kuwa chini yako! mf. Lowasa, chenge, tibaijuka nk. Mpige skuli mazeri.
Mambo mengine ni ya kizembe sana mf mwekezaji anakuja na kusema nitasaidia kujenga misikiti! Na hili limewapumbaza waislamu karibu wote!
 
Rais mstaafu mzee Kikwete amefungua Kanisa la Waadventista Wasabato Rorya mkoani Mara

Mzee Kikwete amemshukuru askofu kwa kumualika japokuwa yeye ni Muislamu na Hii inadhihirisha Tanzania haina Dini

Kikwete amesema Watanzania ni Wamoja hawabaguani kwa Dini wala madhehebu yao Kwani Mungu wetu ni moja ila tunamuabudu kwa njia tofauti

Mzee Kikwete amesisitiza tusichanganye Dini na Siasa na wale wanaochanganya tuwanyanyapae

Source: Global tv
 
Tuliwambia wajikite kwenye vipengele vya mkatana wakakimbilia udini.
 
Wamemwalika wapate pesa ya Harambe tu.
 
TEC iwaache muendelee kuiba mali za umma? shame on you
 
Huwa anamtaja Nyerere kama Baba wa Taifa akihitaji huruma , ila amezoea kumuita Mzee Nyerere
 
Jambo ni moja tu: CCM iwasikilize wananchi. Wabunge wawe wawakilishi wa kweli wa wananchi. Sasa wananchi wakikosa uwakilishi wa kweli, unategemea nini?
 
 

Attachments

  • IMG_2047.MP4
    1.2 MB
shida inakuja, wanasiasa wanasema tusichanganye siasa na dini ili kutunyamazisha wao wapate uchochoro wa kupiga pesa, ndio maana ni matajiri kweli kweli. wanawanyamazisha, ukijaribu kuongea wanasema unaleta udini na wao wanapitia uchochoro huohuo. TEC wamekuja mazima kutetea maslahi ya Taifa baada ya kuona upande mwingine umesherehekea kwasababu mwarabu ndio anakuja kuwekeza hivyo hata kama mwarabu atatunyonya haina shida kwasababu ni mwenzao. ndugu wa mwislam ni mwislam hata kama anafanya makosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…