Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Enginee kivipi, kupinga au kusapport? Au anacheza pande zote kuharibu na kupuliza?Hii clip sio ya leo!
Very old version ....
Angalia hata podium yenyewe ina bendera ya Tanu.
Kikwete hawezi kujitokeza kwa hili jambo sababu yeye ndie engineer mkuu wa hili jambo.
Ila wakristo wa Tanzania mmeweka mbele sana ukristo wenu kuliko chochoooote, hasa wakatoliki. Huo ni ujuha mwingine.Usitegemee TEC watakuja hapa kukujibu ama watatereka na waraka wao.. Hizo ni kelele za chura haziwezi kumzuia tembo kunywa maji
Kuna watu wamo humo walianza kutugawa kikanda huku wakisema chadema ni ya wachaga.Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka Watanzania kuwanyanyapaa na kuacha kuwasikiliza Viongozi wa dini au Viongozi wa siasa wanaotaka kuitumia dini kwa manufaa yao ya kisiasa kwa sababu ni kitu hatari kwa tunu ya amani na utulivu na iwapo tunu hiyo itavunjwa basi gharama yake itaonekana.
Mstaafu Kikwete ameyasema haya leo kwenye uzinduzi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Charya Kamageta Wilayani Rorya mkoani Mara na hizi ndio nukuu zake.
"Natumia nafasi hii kukumbusha kuhusu tunu nyingine muhimu nayo ni kutokuchanganya dini na siasa tukiivunja tunu hii gharama yake tutaiona, kama kuna Viongozi wa dini wanaotaka kutuelekeza kuitumia dini kwa manufaa ya kisiasa na kama kuna Viongozi wa siasa wanataka kuitumia dini kwa manufaa yao ya kisiasa nawaombeni tuwanyanyapae, siku ikifika Uanachama wa Chama cha siasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na Chama cha siasa anachokifuata ndio mwisho wa Nchi yetu”
"Mtakuwa na Vyama vya siasa vya Wakristo, Vyama vya siasa vya Waislamu, vya Walokole , Vyama vya siasa vya Watu gani, kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, utawala na kiserikali kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari, pia Watu kutazama masuala ya dini kwa mtazamo wa siasa za Vyama vyao sio jambo lenye afya kwa Taifa letu, yote mawili yataathiri umoja na kutishia amani na utulivu tunaoufaidi hivi sasa”
"Zanzibar walifika mahali Waislamu wanamuona Sheikh ambaye ni Mfuasi wa Chama ambacho sio chake sio Sheikh sawasawa kwahiyo wakienda kuswali kama Sheikh ni Mfuasi wa CUF wanangoja amalize kusalisha halafu anaingia Sheikh wa CCM na Wafuasi wake ndio maana nilipokuwa Rais nilipambana sana kupata ule mwafaka Zanzibar” #MillardAyoUPDATES
Kwani TEC wameongelea hayo wakiwa madhabahuni?Tukianza kuchanganya dini na siasa, tukageuza...madhabahu ndio mahali pa kuhubiri siasa za vyama vya siasa, kwishiria mbali nchi yetu...lakini Baba wa Taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa, nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni za jicho letu tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo vya aina hii iwe kwa siri au kwa dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya" Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Jakaya Kikwete wakati akizindua kanisa la SDA Rorya mkoani Mara, leo Agosti 20, 2023.
Kikwete si ni Mwanasiasa? Mbona kaenda kusimama kwenye Jukwaa la Dini na kumhubiri Mungu? Au hiyo siyo kuchanganya dini na siasa?Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka Watanzania kuwanyanyapaa na kuacha kuwasikiliza Viongozi wa dini au Viongozi wa siasa wanaotaka kuitumia dini kwa manufaa yao ya kisiasa kwa sababu ni kitu hatari kwa tunu ya amani na utulivu na iwapo tunu hiyo itavunjwa basi gharama yake itaonekana.
Mstaafu Kikwete ameyasema haya leo kwenye uzinduzi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Charya Kamageta Wilayani Rorya mkoani Mara na hizi ndio nukuu zake.
"Natumia nafasi hii kukumbusha kuhusu tunu nyingine muhimu nayo ni kutokuchanganya dini na siasa tukiivunja tunu hii gharama yake tutaiona, kama kuna Viongozi wa dini wanaotaka kutuelekeza kuitumia dini kwa manufaa ya kisiasa na kama kuna Viongozi wa siasa wanataka kuitumia dini kwa manufaa yao ya kisiasa nawaombeni tuwanyanyapae, siku ikifika Uanachama wa Chama cha siasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na Chama cha siasa anachokifuata ndio mwisho wa Nchi yetu”
"Mtakuwa na Vyama vya siasa vya Wakristo, Vyama vya siasa vya Waislamu, vya Walokole , Vyama vya siasa vya Watu gani, kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, utawala na kiserikali kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari, pia Watu kutazama masuala ya dini kwa mtazamo wa siasa za Vyama vyao sio jambo lenye afya kwa Taifa letu, yote mawili yataathiri umoja na kutishia amani na utulivu tunaoufaidi hivi sasa”
"Zanzibar walifika mahali Waislamu wanamuona Sheikh ambaye ni Mfuasi wa Chama ambacho sio chake sio Sheikh sawasawa kwahiyo wakienda kuswali kama Sheikh ni Mfuasi wa CUF wanangoja amalize kusalisha halafu anaingia Sheikh wa CCM na Wafuasi wake ndio maana nilipokuwa Rais nilipambana sana kupata ule mwafaka Zanzibar”
My Take
Tamko la Kikwete ni la kimkakati. Kupigania bandari yetu sio siasa. Amechochea kuni kwenye hizi harakati
Usimlishe maneno mzee wetu JK."Napenda kuchukua nafasi hii kukumbushana kuhusu tunu nyingine muhimu nayo ni kutokuchanganya dini na siasa. Tukiivunja tunu hii gharama yake tutaiona, na kama kuna viongozi wa dini wanataka kutuelekeza kuitumia dini kwa manufaa ya kisiasa, na kama kuna viongozi wa siasa wanataka kuitumia dini kwa manufa yao ya kisiasa, nawaombeni ndugu zangu tuwanyanyapae.
"Siku ikifika ambapo uwanachama wa chama cha siasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na chama cha siasa kinachofuata ndio mwisho wa nchi yetu, mtakuwa na vyama vya siasa vya wakristu, waislamu, walokole nk. Kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, kiserikali, utawala kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari, halkadhalika watu kuyatazama masuala ya dini kwa mtazamo wa siasa za vyama vyao si jambo lenye afya kwa taifa letu.
"Yote mawili yataathiri umoja na kutishia amani, usalama na utulivu tunaoufaidi hivi sasa. Mfano Zanzibar walifika mahali waisilamu wanamuona shehe ambaye ni mfuasi wa chama ambacho sio chake sio shehe sawa sawa, kwahiyo wakienda kusali kama shehe ni msuasi wa CUF wanangoja amalize kusalisha, halafu anaingia shehe wa waislamu na wafuasi wake.
"Nawaambia vitu halisi na ndio maana nilipokuwa Rais nilishughulika sana pale na kupata muafaka, niliahidi kwenye hotuba yangu ya kwanza ya Bunge 2005 Dec 30, kwamba nitafanya kila ninaloweza tujenge muafaka Zanzibar, haukuwa rahisi. Mkutano ule tuliufanyia Butiama NEC, ilikuwa moja ya kikao kigumu kwelikweli, lakini nikasema pamoja na ugumu wote lazima hapa tuvuke. Tukafika mahali nilipoona mambo yamekuwa makali, nikasema twendeni kwanza tukale, tulipokuwa tunakula ndio tukawa tunaweka mikakati ya namna gani tunalimaliza hili jambo. Tukajipanga nani ataanza kuzungumza, tukakubaliana kwamba tutakwenda Zanzibar kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na ndio imetusaidia Zanzibar tuna mazingira ya utulivu mpaka sasa, tungekwenda na utaratibu ule ule wa zamani tusingefika.
"…Tukianza kuchanganya dini na siasa tukageuza mimbari za dini na madhabahu kuwa sehemu ya kuhubiri kwishilia mbali nchi yetu. Lakini baba wa taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa. Nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni ya jicho letu. Tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo wa aina hii iwe kwa siri au kwa Dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya."
Kikwete ameyasema hayo leo 20/8/2023 katika ufunguzi wa jengo Kanisa la Kiadventisti Wasabato Mara.
Hakika, Mama Abduli ni chambo tuWatatoka wote, trick ya kutumia wenye uwezo wa kutumia Podium za kitaifa kutupumbaza, HATUTATOKA kwenye mstari.
Yeye ni mnufaika wa uhuni wote, hana credibility hiyo!
Mkuu Mshana Jr chonde chonde!! Usichekelee chura mmoja anaekoroga maji, juwa ya kwamba maji yakija kugeuka vumbi hata wewe yatakushinda kuyanywa. Tuwe na kiasi na tudhibiti mihemko inayopita kwenye nafsi zetu!!!.Usitegemee TEC watakuja hapa kukujibu ama watatereka na waraka wao.. Hizo ni kelele za chura haziwezi kumzuia tembo kunywa maji
Ametoa Onyo Hilo wakati alipoalikwa kuwa mgeni Rasmi kwenye hafla ya ibada ya kuzindua Kanisa la SDA Rorya Mkoani Mara.
View: https://www.instagram.com/p/CwKssoZMTVG/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
My Take
TEC na wengine wanaomshabikia Udini wakemewe.