Kauli hii kabambe imetolewa na Mh Rais Samia Suluhu Hassan huko Tanga, wakati akifunga mafunzo ya awali ya askari wa Uhamiaji kwenye Chuo cha Boma Kichaka Miba Mkoani humo .
Mh Rais amesema kwamba ili kurejesha Ukakamavu kwa Askari wa Uhamiaji inapaswa wote wenye vitambi kurejeshwa kuhenya ili kupukutisha Vitambi na kurejesha Ukakamavu.
Chanzo: SwahilTimes
Toa Maoni yako
Kitambi kinakuja kutokana na mtindo wa maisha na hakitoki kwa kufanya kwata. Hata akifanyishwa 'Extra drill' maisha yote ya skari utatokea uasi............kupenda maisha ya fahari, kula vitu vitamu bila uwiano, kujipatia kipato bila kuitolea jasho halali na kupotoshwa na pesa zinazoingia mfukoni kila siku hivyo kuacha kufikiri kesho haina rangi sawia na ya leo ndio chanzo.
Hata hivyo mkuu wa kaya ajiandae na changamoto za chini kwa chini kutoka kwao hao the so called 'cops'
AINA KUU ZA TUMBO KUFURA
1.
KITAMBI MVIRINGO – The tumbo hili limekaa kama herufi 'O' linapatikana kwa kula protini nyingi (kimito)
2.
KITAMBI MCHUCHUMIO – tumbo la aina hii limekaa kama herufi 'D' na husababishwa na kula juisi nyingi na bia maalumu
3.
KITAMBI MBONYEO – uvimbe wa tumbo huatamia kitovu kwa kiwango ambacho hufanya kisichoonekana. Hivi ndivyo mafisadi wanavyokuwa, lakini mtu huyo akisimamishwa kazi au kujihusisha na mazoezi ya muda mrefu ya kazi, huisha haraka sana.
4.
KITAMBI MTEPETO – Uvimbe wa tumbo hauonekani kama nguo pana zinavaliwa, husababishwa na kula kupita kiasi
5.
KITAMBI MFUMANIO - Huyu ni mtu ambaye hana pesa, lakini tatizo linatokana na minyoo na utapiamlo mkali
6.
KITAMBI MTUNGUO – aina hii ya uvimbe wa tumbo ni maarufu kwa akina dada na wanawake; tumbo linakuwa na umbo la mayai linalosababishwa na chakula kisicho na uwiano.
Kwa kawaida mwili wa binadamu una seli za mafuta kati ya bilioni 50 na 200 zinazosambazwa katika sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.
Kwa wanawake, seli hizi zipo zaidi katika maeneo ya matiti, makalio, kiuno na nyonga.
Kwa upande wa wanaume, seli hizi hupatikana sana kifuani, tumboni, na nyonga pia.
Mafuta ya tumbo hujilimbikiza kwa njia kuu mbili:
i. Njia ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi
ii. Njia ya pili ni kutoka viungo vya ndani kama moyo, kongosho, n.k.
Uvimbe wa tumbo unaosababishwa na lishe ya chakula kisicho na uwiano lishe sawa
Chanzo kikuu cha unene kupita kiasi ni kukosekana kwa uwiano wa nishati (kalori) katika mwili wa binadamu, hali inayosababishwa na mtu kula vyakula vinavyotoa nguvu zaidi kuliko kile anachoweza kutumia na kuachia kama taka.
Vyakula vinavyochangia kuvimbiwa ni pamoja na :
i. Vyakula vyenye mafuta mengi kama vile nyama nyekundu (iwe imechemshwa, kukaangwa, au kuchomwa), nyama nyeupe ya kuku (iwe ya kuchemshwa, kukaangwa, au kuchomwa), mafuta ya kupikia , (hasa yale yanayotokana na bidhaa za wanyama, kama vile
siagi, na jibini ),
viazi vya kukaanga (
chips) na
pizza.
ii. Vyakula vyenye wanga mwingi kama vile wanga wa mahindi, mihogo, wali, mkate mweupe.
iii. Vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi iliyoongezwa
kama vile soda na keki.
iv. Vyakula vilivyotengenezwa kwa ngano na sukari kama vile keki, vidakuzi, chapatti, pastries, mkate mweupe n.k.
v. Pamoja na vinywaji vinavyotengenezwa kwa kutumia ngano kama vile bia za aina mbalimbali na n.k.
Vyakula vilivyotajwa hapo juu, vikitumika bila kuzingatia kanuni za mlo kamili, huchangia tatizo la kuvimbiwa.
vi. Sababu nyingine ni kutofanya mazoezi ya mwili na viungo kwa muda mrefu ambavyo huongeza kasi ya kuweka mafuta karibu na tumbo au moyo unaoathiri hatari ya saratani au upanuzi wa moyo au ujenzi.
vii. Msongo wa mawazo
viii. Kuongea sana bila kipimo
Kitambi ni mafuta ambayo yanaweza kuwa chini ya ngozi yako au ndani kabisa kuzunguka moyo,, mapafu, maini na viungo vingine. Mafuta haya ya ndani (visceral fat) ndiyo yanayoweza kuwa tatizo kubwa kwa afya yako hata kama mwili wako ni mwembamba kiasi gani. Mwili huhitaji mafuta haya ndani kwa ajili ya kutenganisha viungo vya ndani ya mwili visigusane na kusuguana, lakini yakizidi huleta matatizo ya kiafya. Ukiwa na mafuta mengi yaliyopitiliza kipimo cha uhitaji utakuwa kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa kama ya ‘Shinikizo la damu, Kisukari (Kisukari hatua ya 2), magonjwa ya moyo, kansa (utumbo na maziwa) na mengineyo.
Kuacha mwili kunenepeana na kuongeza uzito kunasababisha mwili ushindwe kupata sehemu ya kutosha ya kuhifadhi mafuta ya ziada na mengine kuyachoma kuongeza joto hivyo kusababisha mwili kutafuta sehemu nyingine za kutunzia kama kuzunguka moyo ambapo ndipo matatizo yanapoanzia kukusumbua.
Kumbuka uzito wa mtu mwenye siha safi unatakiwa uwe sio zaidi ya nusu ya urefu wake wa kimo akiwa amesimama wima. Upana wa moyo wa mtu mwenye sifa njema unatakiwa usiwe zaidi ya kipimo cha kukunja ngumi mkono wake mwenyewe.