Rais Samia afupisha ziara yake Dubai kurejea nchini haraka iwezekanavyo, Serikali kugharamia mazishi na matibabu ya majeruhi wa mafuriko ya Hanang

Uzuri wa Serikali ya CCM ikipewa ushauri na vyombo vinavyo husika vya maafa kabla ya tukio halija tokea. Inaweka pamba masikioni mpaka kukitokea majangaa ndio inakuwa mstari wa mbele katika kushughulikia waliopatwa na hayo majangaa hiyo ndio Serikali ya CCM inavyofanya kazi.
Katika hili serikali ingefanyaje?
 
Kama amekatisha ziara fedha za kujikiku zirudishwe serikalini yeye na watu wake wote warudishe hazina
Hii haiwezekani baba, baadhi ya pesa tulizopewa ni stahiki yetu, sisi hatukuleta hayo mafuriko, mwambieni sir god awapeni, lakini sisi bado tunaendelea na mkutano, hayo yanamuhusu yeye tu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuwa serikali igharamie mazishi ya wote waliopoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyotokea na mafuriko katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.

Rais Samia pia ametaka majeruhi wote ambao wapo kwenye hospitali mbalimbali wapate matibabu yote yanayostahili kwa gharama za Serikali, huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kutoa msaada wa dharura na uokoaji.

Aidha Rais Samia ameelekeza Serikali ya Mkoa na Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha wananchi wote ambao makazi yao yamesombwa na maji wapate makazi ya muda kwa ajili ya kuwastiri wananchi hao.

Maafa haya yameathiri mji wa Katesh hususan vijiji vya Jorodom, Ganana, Katesh na Dumbeta na pia vijiji vya Gendabi, Sarijandu, Arukushay, na Sebasi.

Kwa taarifa za awali nyumba na mifugo imeathirika sana huku idadi za kaya zilizoathirika ni 1,150, idadi ya watu walioathirika hadi sasa ni 5,600 na pia ikikadiriwa takriban ekari 750 za mashamba zimeharibika.

Licha ya changamoto kadhaa zilizokuwepo uokoaji unavyoendelea ikiwemo barabara kuharibika huku tope na magogo kujaa barabara kuu na mitaani na kusababisha mawasiliano kukatika, serikali inajitahidi kukabiliana nazo.

Idadi ya vifo hadi sasa ni zaidi ya watu 50 huku majeruhi waliopelekewa katika hospitali mbalimbali za wilaya, mkoa na vituo vya afya ni zaidi ya 80.

Wakati huo huo Rais Samia ameelekeza tathmini ya kina ifanyike juu ya maafa hayo na vitengo na taasisi zote za Serikali zinazohusika kuwepo eneo la tukio na kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali inarejea kawaida.

Rais Samia anatoa pole kwa wafiwa wote kutokana na msiba mkubwa uliowakumba na pia anawahakikishia wananchi walioathirika kuwa serikali iko pamoja nao na itahakikisha inashughulikia masuala yote yaliotokana na janga hili.

Rais Samia ambaye amekuwepo Dubai kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) ameamua kufupisha safari hiyo na kurejea nchini haraka iwezekanavyo ili kushughulikia kwa karibu janga hilo.

View attachment 2832970
View attachment 2832974
Kwani Makamu wa Rais Hayupo 🤔🤔🤔🤔🤔
 
Uzuri wa Serikali ya CCM ikipewa ushauri na vyombo vinavyo husika vya maafa kabla ya tukio halija tokea. Inaweka pamba masikioni mpaka kukitokea majangaa ndio inakuwa mstari wa mbele katika kushughulikia waliopatwa na hayo majangaa hiyo ndio Serikali ya CCM inavyofanya kazi.
Haya majanga ni faida kwa CCM kupiga pesa za umma, hizi hazina audit query mzee
 
Kumbe kukitokea Majangaa Baadhi ya Viongozi wa Serikali wanakula pesa za Michango ya kodi za Wananchi walala hoi? kweli tutafika kuupanda Mlima kilimanjaro kufika kileleni? tuna safari ndefu kweli kufika huko killeleni haya waache wale tu Mungu anawaona wanayoyafanya.
 
Hujasikia jana kuwa VP yuko ngambo kwa ziara ya kikazi!?
But VP angesolve kwa Mujibu wa katiba Why Majukumu haachiwi Vice naona majukumu yote amafanya yeye hata yale ya Vice..

Imagine Yeye angekuwa vice na Rais angekuwa wa Kiume watu wangesemaje
 
Kumbe kukitokea Majangaa Baadhi ya Viongozi wa Serikali wanakula pesa za Michango ya kodi za Wananchi walala hoi? kweli tutafika kuupanda Mlima kilimanjaro kufika kileleni? tuna safari ndefu kweli kufika huko killeleni haya waache wale tu Mungu anawaona wanayoyafanya.
Bahati nzuri haya majangili yakiiba yanaenda kutubu kwa MUNGU na kutoa michango Msikitini na Makanisani mambo yanakaa sawa chap
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuwa serikali igharamie mazishi ya wote waliopoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyotokea na mafuriko katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.

Rais Samia pia ametaka majeruhi wote ambao wapo kwenye hospitali mbalimbali wapate matibabu yote yanayostahili kwa gharama za Serikali, huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kutoa msaada wa dharura na uokoaji.

Aidha Rais Samia ameelekeza Serikali ya Mkoa na Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha wananchi wote ambao makazi yao yamesombwa na maji wapate makazi ya muda kwa ajili ya kuwastiri wananchi hao.

Maafa haya yameathiri mji wa Katesh hususan vijiji vya Jorodom, Ganana, Katesh na Dumbeta na pia vijiji vya Gendabi, Sarijandu, Arukushay, na Sebasi.

Kwa taarifa za awali nyumba na mifugo imeathirika sana huku idadi za kaya zilizoathirika ni 1,150, idadi ya watu walioathirika hadi sasa ni 5,600 na pia ikikadiriwa takriban ekari 750 za mashamba zimeharibika.

Licha ya changamoto kadhaa zilizokuwepo uokoaji unavyoendelea ikiwemo barabara kuharibika huku tope na magogo kujaa barabara kuu na mitaani na kusababisha mawasiliano kukatika, serikali inajitahidi kukabiliana nazo.

Idadi ya vifo hadi sasa ni zaidi ya watu 50 huku majeruhi waliopelekewa katika hospitali mbalimbali za wilaya, mkoa na vituo vya afya ni zaidi ya 80.

Wakati huo huo Rais Samia ameelekeza tathmini ya kina ifanyike juu ya maafa hayo na vitengo na taasisi zote za Serikali zinazohusika kuwepo eneo la tukio na kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali inarejea kawaida.

Rais Samia anatoa pole kwa wafiwa wote kutokana na msiba mkubwa uliowakumba na pia anawahakikishia wananchi walioathirika kuwa serikali iko pamoja nao na itahakikisha inashughulikia masuala yote yaliotokana na janga hili.

Rais Samia ambaye amekuwepo Dubai kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) ameamua kufupisha safari hiyo na kurejea nchini haraka iwezekanavyo ili kushughulikia kwa karibu janga hilo.

View attachment 2832970
View attachment 2832974
1. Liko jambo

2. Jambo liko
 
Samia Rais mtenda wema haswa
 
Back
Top Bottom