Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Kama aliumizwa na tozo ya tsh100 aliyokuwa ameiondoa kwa kutupunguzia ukali wa maisha, hakuna jipya atakalokuja nalo.
 
Dah uyu mama hana msaada kabisa na watanzania kwa ujumla.
 
Hii nchi inaongozwa na vibwengo Kama nane hivi...Yani system iko corrupt kiasi kwamba haifanyi kazi...ka nchi kapo kwenye auto pilot...
 
Kwa hiyo elimu yako hii ya uchumi lazima uwe waziri wa fedha even governor of BoT
Sijawahi kiwa mumwa wa serikalini. Hizo fikra za kitumwa ni zako wewe, sijaingoja serikali kunifanyia mambo yangu ya kimaisha hata siku moja, kwa sababu nafahamu "serikali" ni jina tu na waliopo huko ni binaadam kama wewe au mimi na wapo pale kwa ajili ya matumbo yao kwanza wakitimiza majukumu yao.

Mtu unalalamika kuku ghali, sili kuku. Wakati una fursa ya kujifugia kuku wako, ni ujinga huo.
 
Mi nadhani iyo paragraph yako ya pili uyo jamaa angestep out kidogo atuachie wizara
 
ivi yale mafuta ya Zanzibar waliyanunulia wapi mbona bei kitonga sana, au Zanzibar sio sehem ya Tanzania
 
Si bora wangesubiri kukuche tu maana sio ishu ya leo jana wala juzi, hizi gafla gafla sina imani kama zinakuja na majibu mazuri.
Huenda wamepata clues za kuweza kututoa hapa tulipo kwenye suala la mafuta ambazo zina deadline ya muda mfupi sana. So, hawataki kupoteza point!
 
Hii nchi inaongozwa na vibwengo Kama nane hivi...Yani system iko corrupt kiasi kwamba haifanyi kazi...ka nchi kapo kwenye auto pilot...
Aisee kweli kabisa juzi nimeshuhudia hawa wazee wa suluali nyeuoe na kofia wamekuja barabara ya vumbi kukamata bajaji wakawa na kula buku mbilimbili zao pamoja na magari walivyomaliza wakaingia kichakani wakabadilisha nguo wakavaa kiraia wakasepa sasa sijui ni kweli ni wenyewe au ni wamchongo
 
Waafrika tunapenda sana kula imagine kikao serious kama hicho kimejaa machupa na majuisi sijui makorosho kwani wangekula baada ya kumaliza ingekuwaje? Hatuko serious kabisa kila sehemu tunawaza kula kula hovyo tu.
Mataifa ya wenzetu kwa vikao serious kama ivyo utakuta wameweka maji tu bas. na mambo yanapangiliwa na kukamilika, kwetu wanawawekea adi wali maharage lakin kikao kinaishia kiutopolo
 
Waishushe Diesel kwa sababu ndio inayoleta mfumuko wa bei.
 
Huku sisi mikate inapanda kila siku!, wanapandisha mia 200 kila wiki!, wanasingizia mafuta ya kula na petrol kupanda
 
Anawaagiza kina nani sasa!!

Kumbe hana akili kiasi hiki
Ilitakiwa waumize vichwa mlemle barazani.
Ikiwa urais kazi yake ni kutoa maagizo tu kwa waliochini yake basi nchi hii tunamatatizo makubwa kuliko tunavyofikiri!
 
Iko wazi tu ni wapi pa kuondoa mafuta yashuke...kuna tozo kibao ni suala kuamua ipi iondoke na ipi ibaki
 
Amewaagiza tena kikao hicho kina maana gani ilibidi waje na maazimio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…