Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Leo usiku wa manane Urusi walikuwa wanasheherekea ushindi so Cabinet inacheza na gap hilo
 
Hivi makamu yuko wapi mbona anakosa kwenye vikao muhimu Kama hichi..?
Isitoshe alishawahi kuwa waziri wa fedha,hivyo anaufahamu mzuri sana juu ya uchumi Sasa anakosaje kwenye swala Kama hili!
Wanamtenga,hawampi ushirikiano
 
Siwezi kusema sana kuhusu jinsi serekali inavyofanya kazi lakin kwenye hicho kikao sidhani kama team imekamilika hao mawaziri ni wanasiasa tu inputs zao ndogo sana. Makatibu wakuu, EWURA, TPDC ..ndio wenye inputs kubwa kuliko wanasiasa. Hayo maoni yangu tu
 
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

View attachment 2217468

Yani Rais na serikali wamejua mafuta yamepanda usiku wa Leo? Hiki kikao kina maana gani ikiwa hakina wawakilishi wa wadau wa mafuta?

Inamaana serikali haijui sababu za kupanda kwa bei ya mafuta hadi waitishe kikao usiku? Hivi ni nani aliweka tozo kwenye mafuta? Hivi serikali haijui zile tozo karibu 20 kwa taasisi mbalimbali zilizopo kwenye mafuta?

Hivi atahari za kupanda kwa mafuta kwa sasa zitazuiwa vipi ikiwa kila kitu kimeshapanda ndio wanafanya kikao cha dharura? Au serikali ndio imejua leo kuwa mafuta yamepanda?

Huu nao ni usanii tuu!
Tuliambiwa kuwa kila kitu kitapanda na kweli kila kitu kimepanda sasa sijui maana ya kikao cha dharura ni nini? Huu ni ujinga tuuu!
 
Asante alkasusu hiyo kwenye chupa hapo mezani bei ya mafuta lazima ishuke na kazi iendelee
 
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

View attachment 2217468
Mbona rahisi hakuitajiki hata vikao, toa alfu 1500 kutoka kwenye diesel uza alfu 2 diesel na 5000 Petrol changamoto itakuja wale wazee wa fursa kutorosha nchi jirani lakini jukumu la polisi au 2500 diesel na 4500 petrol mwisho wa mchezo.
 
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

View attachment 2217468
Yaani hawa watu wanfurahisha! Mpaka wanaamua kupandisha mafuta walikuwa hawajtafakari kwa kina!!!!! Mbona mafuta kwa kipindi kifupi yamepanda sana!!!! Actually kila kitu kimepanda bei. Yaani usanii tu huu.
 
Sijui ni Ukosefu wa vision, au ushauri mbovu, au pengine ukosefu wa bunge lenye 'kelele'...

Few days back, same person alikuwa akiweka bayana kwamba mafuta yatapanda bei na vitu hivyo hivyo vitapanda bei kwa sababu ya conflict ya Ukraine vs Russia na kodi iliyoondolewa irejeshwe (Hizo statements zilionesha she aint in a position to change nothing)...

Sasa nini kimebadilika sasa? Wakati moja ya effects za vita hiyo ilishakuwa wazi kwamba mafuta yataenda juu, hivyo viongozi wa nchi nyingine walipaswa wawe na different strategies za namna ya kupambana na tatizo hilo...

Sasa hawa wa kwetu ndio wanakuja kushtuka leo, sijui hata walikuwa wanasikilizia nini? kwamba Russia ataondoka Ukraine ndani ya muda mfupi na kila kitu kitarudi sawa!!!
 
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

View attachment 2217468
Hapo sana sana watatoa ile tozo ya sh.100 na kuruhusu waagizaji binafsi . USELESS!
 
Kama tangu mwanzo walijua kuwa bei ya mafuta itapanda na hawakuchukua hatua yoyote zaidi ya kututangazia kuwa bei ya kila kitu kitapanda bei sasa hiki wanachotaka kukifanya ni kuwafanya wafanyabiashara wapige super profit maana mafuta yatashuka ila bei ya vitu haitashuka.
Walishindwaje kuchukua hatua kabla ya kupandisha bei ya mafuta??
 
Huwa inashangaza sana , kipindi cha jiwe walikuwa wanapenda kula sambusa kwenye matukio.
Waafrika tunapenda sana kula imagine kikao serious kama hicho kimejaa machupa na majuisi sijui makorosho kwani wangekula baada ya kumaliza ingekuwaje? Hatuko serious kabisa kila sehemu tunawaza kula kula hovyo tu.
 
Sasa kila siku wanaitana na wanaagizana harafu hawaji na majibu..

Yaani kila mtu anaogopa lawama..

Mimi nawapa ufumbuzi,punguza Kodi na tozo kwa sh 400 harafu gap la kufidia mapato,TRA iendeshwe oparesheni ya kuhakikisha kila muuzaji anatoa risiti na kila mnunuzi anachukua risiti..

Wasiofanya hivyo ni faini na kupiga mnada bidhaa zao, mapato yako mengi Sana kwenye Bar,Migahawa,Guest House,madukani nk..mfano kuna mauziano ya mali yanafanyika daily ila hakuna anaelipa Kodi .

Kuendelea kuchekea watu wasiowajibika ila waanadai haki itawatokea puani.
Kutoa 400 bado sio suluhisho. Anatakiwa kutoa buku kabisa. Mbona hizo kodi tunaweza kuzipata kirahisi tu. Bongo tunaifanya ndio supplier wa mafuta nchi zote zinazotegemea bandari yetu. Na tunaweka kakodi kadogo tu kufidia pale tulipotoa.
 
Yeye ndiye alipaswa kuja na masuluhisho kadhaa kisha wamshauri yapi ni mazuri zaidi au waongeze mengine.
 
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

View attachment 2217468
Mezani kumenona, wangetoka na suluhisho humohumo sio kwenda kutafuta suluhisho wakati muda unayoyoma
 
Wafanyabiashara wa Mafuta wanamhujumu Mama, Mbona nchi ya Malawi imethibiti awamu hii mafuta kutokupanda bei, source MERA maintains fuel prices. Wasaidizi wa Mama wafanye kazi yao pia. Siyo wanapandishe bei, ili wapate Faida kubwa. Pia wananchi wapewe taarifa. Jamani eeeh mzigo umepanda bei, mafuta yatakayoingia baada ya week mbili bei itaongezeka.
 
Back
Top Bottom