Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Alishafeli na zile kauli zake.
Sasa anajirudi.
Kauli zipi? Mimi naona wewe ndiye uliyefeli.

Mama anachapa kazi nyinyi mnapayuka. Unafikiri nchi inalala hata Rais ashindwe kuitisha kikao usiku? Wewe una information alizonazo yeye? Alikuita wewe au kawaita watendaji wake, fikiri kabla hujapayuka hovyo.
 
Yaaani mafuta yapande wiki mbili kabla akawndelwa na ROyo tour !!!!!usikute ndo wanapangankupandiaha bei
 
Baada ya kukamilisha kipaumbele cha kuzindua Royo Tua(Royal Tour) zote nje na ndani ya nchi sasa ndo wanahundua kuwa kuna kupanda bei na kinafanyika kikao cha dharura kabisa
 
Itakuwa ni agiza agiza kila siku, ila hapo kuna viongozi unawaona kabisa hawana uchungu na wananchi kwakuwa vipato walivyonavyo hawaathiriki sana, mf huyo mwigulu hana uchungu kabisa na wananchi linapotokea suala la kuwaumiza wananchi yeye anaangalia serikali itanufaika vipi, suala la kutoa tsh920 kwenye kodi ya mafuta si suala la kusubiri maagizo au mijadala ya usiku, mafuta ndiyo yanayopandisha karibu kila kitu ukiondoa kodi ya mafuta utafanya bidhaa zipungue bei na kuwapa unafuu wananchi, serikali yoyote inayowathamimi wananchi wake haiwezi kuwa na Waziri kama mwigulu, yeye anakuwa upande wa kuwaumiza wananchi
 
Bajeti ya kikao Bilion 2[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yani hiki kikao ilitakiwa kiitishwe ile siku bei zimepandaaa na iwe ni Kunywa majiii Tuu sio wanaongelea matatizo makubwa ya mfumuko wa bei wanakula kama wapo Vacation... Yani kujali mitumboo yao tuu
 
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

View attachment 2217468
Hivi Mama ana dhani Mwigulu ataweza kumsaidia? Wakati Mwigulu ana furahia Mama kulaumiwa ili aonekane hafai kuwa Rais ili na yeye agombee 2025!!!
 
Wonder woman alikuwa busy lokesheni na uzinduzi wa movie, jana usiku ndo kapata taarifa ya kupanda bei vitu ndo ikabidi aitishe kikao cha dharura ila kikao chenyewe inaonekana ni kama anafuturisha
 
Samia anachezewa sana na hajui chochote!

Inakuwaje mafuta yanapanda kwa sh. 300 nzima?

Kama Samia aliweza kukaa USA siku 8 na mafuta yakapanda maradufu, niaminini mimi kwamba hajui chochote
 
Tutarajie kushuka kwa bei ya mafuta.
Kwa wafanyabiashara hata mafuta yakishushwa bado bidhaa zilizopandishwa bei kwa kisingizio cha mafuta hazishuki bei asilani!! Hivyo ndivyo walivyo miaka yote !! TUME YA BEI NI MUHIMU NCHI HII !!!
 
Kwa hiyo Vita imeisha?
Kwa hiyo wewe ulikuwa unangoja vita iishe? Anza kutumia gari za solar za kipanya wewe.

Wewe si poyoyo, utaondolewa kodi "direct" kwenye mafuta utapachikiwa kodi "indirect" kwengine utachekelea mafuta yameshuka.
 
Kutoa 400 bado sio suluhisho. Anatakiwa kutoa buku kabisa. Mbona hizo kodi tunaweza kuzipata kirahisi tu. Bongo tunaifanya ndio supplier wa mafuta nchi zote zinazotegemea bandari yetu. Na tunaweka kakodi kadogo tu kufidia pale tulipotoa.
Kusema ni rahisi Sana,haya unaifanyaje kuwa supplier kwa short term? Acha kuropoka mkuu..

Unajua athari ya buku kwenye bajeti? Afu bidhaa kama mafuta ambayo hata ukitoa ina inelastic demand itakusaidia nini?

Serikali ikijitahidi nasema kama ikijitahidi itatoa chini ya 500 na ceiling itakuwa ni maeneo ya pembesoni bei isizidi 3000/ltr
 
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

View attachment 2217468

kikao cha dharura unaitisha Rais then unawaagiza wakatafute Suluhu sho ?​

Wewe kama Rais unatakiwa ukitisha kikao cha dharura uwe na suluhisho tena la haraka.​

Hali ya mafuta ya kula ni mbaya hata kuliko mafuta ya petrol nchini , lita moja ni Tsh 9,000 wakati petrol ni Tsh 3,341​

Kwa sababu mama ni muislamu kwa hiyo wahujumu uchumi wanamuujumu.
Hilo unalisema wewe. Hamna pakuhujumu zaidi ya maneno ya kijinga tu. Tunawafahamu, mlikuwa hivihivi wakati wa Mwinyi, mkayarudia tena wakati wa Kikwete na mtaendelea nayo kila ataposhika Muislam. Mwiso wa siku tukilinganisha tunaona kuwa hakuna viongozi bora wa nchi hii zaidi ya Waislaam.
 
Back
Top Bottom