Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Sasa vitu vitapanda Bei g Sababu ya Vita ya urusi na Ukraine kwani Vita imeisha?
SI angeacha tu maisha yaendelee na yeye alishakubali kuwa vitu lazma vipande Bei.
Vikao vya Nini?
Tatizo lako niuelewa finyu tu, hakuna zaidi.
 
Nakupa mfano.
Nondo ya mm 12 Tani moja ni 2,000,000
Zinakaa pcs 94 ukigawanya unapata kila nondo 1 ni shilling 21,270.
Lakini Sasa hivi nondo ya 12 mm inauzwa 26,000 mpaka 27,000.
Faida kwa nondo moja ni 5,000+
Lakini kwa kuwa yeye ameshasema vitu vitapanda.
Nani wa kufuatilia hizi Bei za vitu?
Na yeye ameshatoa kauli vitu vipande?
Tatizo lako niuelewa finyu tu, hakuna zaidi.
 
Piga kazi mama tumecheleweshwa mnooo kama taifa
 
Maigizo tu haya. Kwann wasingejadili kabla ya kupandisha?

Au ndo Create a problem, then solve it to be seen as if you are working [emoji847]
Ndo hivyo yaan hatupo proactive tunafanya reaction baada ya madhara kutokea .samia ni sikio la kufa wanafikiri wanawakomoa sukuma gang

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni jambo jema , vilevile watoke na mpango kabambe wa Kutoka kutegemea mafuta na kutegemea gesi yetu ya Mtwara kama nishati mbadala ya magari, pikipiki .
Kukiwa na ushindani sokoni Kati ya mafuta na gesi kwa vyovyote Bei ya mafuta itashuka
 
Kitu kikubwa hivyo kinaweza kupandishwa bila yeye kujua? Pale kawekwa kwa ajili gani, yeye aendelee kuupiga tu mwingi, iko sikuMungu atatutetea tu!
 
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

kikao cha dharula au walienda kula
 
Back
Top Bottom