Rais Samia akikupa mualiko Ikulu wa dakika 5 utamshauri nini kama kijana wa kitanzania?

Bora ule mbuno mkuu, wao wanakula pesa zetu, sie tufurahie mbuno tu🀣🀣🀣
 
Cha kwanza kabisa ni hawa wanaofisadi hela zetu harafu kabla ya kufukuzwa KAZI wanahamishwa vituo vya kazi kama Tz haina wasomi.Yaan aanze kupitia majina yote ya viongozi wenye kashfa ya wizi tu wapigwe chini na kufilisi mali zao .Najua huko atakusanya pesa nyingi kuliko mapato ya mIezi miwili ya TRA
 
Nitamshauri aniteue ukurugenzi wa jiji la Dar es salaam
 
Nitamshauri Mh Rais afanye Kila linalowezekana Aweke Mitaji Mikubwa kwenye Mabank ya Serikali ili yaweze kuchangia kwenye Uchumi wa Nchi hasa kwenye UANZISHAJI WA VIWANDA KWA WAZAWA.

Kenya inakusanya Kodi kubwa kwa Sababu ya VIWANDA.

Mikopo ya VIWANDA hapa kwetu ina Commercial rate na hakuna Grazing period!
Matokeo yake kila mtu anakuwa tu machinga wa kuagiza bidhaa nje!

Hili Eneo ni Muhimu sana!

Mikopo Maalum kwa ajili ya VIWANDA,KILIMO/MIFUGO na UJENZI.

TIB-Ni bank Nzuri sana lakini haina Mtaji

TADB
AZANIA
TCB.

Mama aweke pesa HUMU-TRILLIONS halafu ILE Wizara ya Mipango itoe Economic Growth Master plan kwa kufungua Madirisha Maalum kwa ajili ya kutekeleza Mipango hiyo kupitia hizo Bank!

Miaka kumi tu ndani ya program hiyo NCHI YETU ITAZIDI NCHI ZOTE ZA EA.

Pesa zitatoka wapi?

Ongezeko la Makusanyo ya Kodi ya Bandari kutokana na Transformation ya DP World.

Jambo la Pili:
Apambane na RUSHWA!

Kuna RUSHWA ZA KIJINGA SANA SERIKALINI!

Hakuna maendeleo yoyote ikiwa RUSHWA itakuwa sehemu ya utendaji Serikalini!

Otherwise SSH is my Best President so far!
 
ujumbe wako umepokelewa chief , pia jali afya kwenye hizo mbuno .
 
hata mimi nimepata somo chief, ujumbe utamfikia alikiri yeye ni mdau wa jf
 
Bora ule mbuno mkuu, wao wanakula pesa zetu, sie tufurahie mbuno tu🀣🀣🀣
Na starehe kuu ya masikini ndio hiyo. πŸ˜‚πŸ€£
Nauli ya kwenda ibiza au copa cabana naipatia wapi?
 
Lakini pia zipo changamoto kadha wa kadha ambazo watanzania wanatamani wamfikishie Rais wao, nao wajione ni sehemu ya watanzania wanaofaidi matunda ya nchi hii!
Siyo changamoto ni woga na kuwalinda maswahiba, namshauri
  1. Awachukulie hatua waliotajwa kwenye report ya CAG ikibidi afumue namkusuka upya baraza la mawaziri
  2. Aboreshe maslahi na mafao ya watumishi wa umma ili kuboresha utendaji kazini
  3. Aachane na timu ya wale jamaa wa Chalinze
  4. Tupate katiba mpya ili kuondokana na hii adha ya kuchezewa na wajanja wachache
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…