Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Watanzania tuna shida gani?

Hilo tangazo mmesoma vizuri kabla ya kuanza kubishana kuhusu kima cha chini?

Nanukuu " NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA IKIWEMO KIMA CHA CHINI KWA 23%"

sasa kuna wengine mmeonna KWA KIMA CHA CHINI tu.
 
Wengi huenda bado hamjaelewa
 
Kuongeza mishahara aitatusaidia hali kuna bidhaa ambazo ni muhimu kila kukicha zinapanda bei na sio watanzania wote ni wafanyakazi . Mimi nafikiri jambo la msingi ni kuwapa unafuu wananchi katika bidhaa muhimu wanazotumia kila siku. Wanaokula keki ya taifa ndio wanaozidi kufaidi hali mtu asie na kazi anaumizwa ktk bidhaaa
 
Yule Ibilisi anajisikia vibaya huko kuzimu.
Hivi kwanini hii nchi ina watu wenye roho mbaya na uchawi kama woiso woiso .
Haiwezekani mshahara tuongezewe sisi kuumia wanatumia wao.
Hivi mshahara ungekuwa hauna maana hata Samia na mawaziri wake pamoja na wabunge wangelipwa hata laki mbili au laki moja kisha wangejikita kupunguza bidhaa bei.
 
Wewe ni MPUMBAVU. Tumekaa miaka 6 bila nyongeza ya mishahara hapa.
 

Hii 23.3% kwa kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma? Ina maana gani hasa? Msishangilie kwa hili​

🧐🧐Naam waweza shangilia kumbe hujui hiyo asilimia 23 inamaana gani?
 
Je wewe ni mtumishi wa serikali? Maana kuongeza asilimia za mshahara kwa kima cha chini hakujaanza mwaka huu.
Kumbuka hata kwenye kodi ilipunguzwa kwa wenye kima cha chini ikawa asilimia 8 kwa wenye kima vha chini kama sijakosea wakati ambao hawapo kwenye kima cha chini wanalipa zaidi ya hapo.
Hivyo wanapotumia kima cha chini wana sababu zao za kimahesabu. Hii 23% sio flat rate na utakuja kukiri mwenye hapa.
Kubisha mie siwezi.
 
Mkuu mbona hilo tangazo la ikulu liko wazi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…