Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Watanzania tuna shida gani?

Hilo tangazo mmesoma vizuri kabla ya kuanza kubishana kuhusu kima cha chini?

Nanukuu " NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA IKIWEMO KIMA CHA CHINI KWA 23%"

sasa kuna wengine mmeonna KWA KIMA CHA CHINI tu.
 
Mama ni Mama, yaani hapa ndio utajua, JPM alituua sana watanzania, yaani Mama katika mwaka mmoja kapandisha 23.3% yaani Watumishi wa umma wataandamana kumpongeza Mh. Rais Samia.

Mama Samia, watumishi wa Umma watakuombea kwa Mola na miaka yako iwe utakavyo duniani. Hii ni kazi kubwa sana Mama yetu kaifanya. Hakika Serikali ya CCM chini ya Mama yetu Samia imetenda makubwa hapa. Mungu ambariki Mama Samia sana.
Wengi huenda bado hamjaelewa
 
Kuongeza mishahara aitatusaidia hali kuna bidhaa ambazo ni muhimu kila kukicha zinapanda bei na sio watanzania wote ni wafanyakazi . Mimi nafikiri jambo la msingi ni kuwapa unafuu wananchi katika bidhaa muhimu wanazotumia kila siku. Wanaokula keki ya taifa ndio wanaozidi kufaidi hali mtu asie na kazi anaumizwa ktk bidhaaa
 
Yule Ibilisi anajisikia vibaya huko kuzimu.
Hivi kwanini hii nchi ina watu wenye roho mbaya na uchawi kama woiso woiso .
Haiwezekani mshahara tuongezewe sisi kuumia wanatumia wao.
Hivi mshahara ungekuwa hauna maana hata Samia na mawaziri wake pamoja na wabunge wangelipwa hata laki mbili au laki moja kisha wangejikita kupunguza bidhaa bei.
 
507945227df005eeaa.jpg
 
Kuongeza mishahara aitatusaidia hali kuna bidhaa ambazo ni muhimu kila kukicha zinapanda bei na sio watanzania wote ni wafanyakazi . Mimi nafikiri jambo la msingi ni kuwapa unafuu wananchi katika bidhaa muhimu wanazotumia kila siku. Wanaokula keki ya taifa ndio wanaozidi kufaidi hali mtu asie na kazi anaumizwa ktk bidhaaa
Wewe ni MPUMBAVU. Tumekaa miaka 6 bila nyongeza ya mishahara hapa.
 

Hii 23.3% kwa kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma? Ina maana gani hasa? Msishangilie kwa hili​

🧐🧐Naam waweza shangilia kumbe hujui hiyo asilimia 23 inamaana gani?
 
Naelewa nachosema, nchi zote Duniani hutumia hiyo standard katika kuset mishahara. Unapongeza mshahara huwezi sema kila kada itakuwa hivi na hivi, Unataja kwa ujumla sasa kima cha chini kitapanda kwa % kadhaa, hapo una maanisha wengine wataongezeka kutokana na asilimia hizo hapo.

SERIKALI INAPANDISHWA MISHAHARA KWA WATUMISHI WAKE WOTE KWA UJUMLA NA RATE SAWA. MTATOFAUTINA POSHO KULINGANA NA TAASISI.
Je wewe ni mtumishi wa serikali? Maana kuongeza asilimia za mshahara kwa kima cha chini hakujaanza mwaka huu.
Kumbuka hata kwenye kodi ilipunguzwa kwa wenye kima cha chini ikawa asilimia 8 kwa wenye kima vha chini kama sijakosea wakati ambao hawapo kwenye kima cha chini wanalipa zaidi ya hapo.
Hivyo wanapotumia kima cha chini wana sababu zao za kimahesabu. Hii 23% sio flat rate na utakuja kukiri mwenye hapa.
Kubisha mie siwezi.
 
Afadhali wewe umeliona hilo. Unless otherwise mwandishi naye kiswahili kwake ni taabu, Lakini tafsiri ya aya ya kwanza ni hii.

1. Rais amekubali kuongeza mshahara kwa kiasi ambacho bado hakijawekwa wazi na ameongeza pia kima Cha chini kwa 23.3/%
2. Rasi amekubali kuongeza mshahara kwa 23.3% na kima Cha chini kwa 23.3%.
Mkuu mbona hilo tangazo la ikulu liko wazi kabisa.
 
Back
Top Bottom