Rais Samia akutana na Baraza la Maaskofu (TEC), Kilaini aelezea Historia yake na utaifishaji wa mashule 1970

Sisi tuliopewa kuzifahamu "siri" za Ufalme wa MUNGU, tunalitizama tu hili "kanisa" la "kinafiki" na kulionea huruma maana tunajua nini utakuwa mwisho wake.
Soma Ufunuo 17:1-2
 
Hizo labda ni ministry ila so called walokole kama TAG/EAGT/FPCT wana mifumo kuanzia jimbo mpaka makao makuu na wana taasisi nyingi chini yao kma vyuo,vituo vya media,shule, hospitali,NGOs n.k so mifumo ipo. More so wanayo CPCT ambayo ni umoja wa makanisa yote ya kipentekoste Tanzania so obviously wana platform.
Hawana mifumo kabisa watu wanatoka Mbezi mwisho kuna kanisa la TAG anaenda kusali Kimara TAG. Mara nyingi makanisa haya wanamfuata mchungaji na si mfumo wa kanisa. Akifa mchungaji wanasambaratika
 
Sasa kama mama ameweza kukutana na waromani bila mtu wa katikati, kwanini wanalazimisha cdm wapeleke hoja zao kwa Shibuda, kabla ya kuzipeleka kwa rais?
Chadema hamna akili, hivyo ni lazima hoja zenu zipitie kwa mwenye akili kwanza kabla ya kumfikia raisi
 
Kwani waliporwa na nani?
Serikali ilitaifisha Ila kuna bàadhi wamesharejeshewa kama Forodhani ambayo Kwa sasa ni St.Joseph IPO Primary na A level. Ziko nyingine pia walirejeshewa.

Kuna kipindi wakati wa kikwete kama sikosei walikuwa na mchakato wa kuomba kurejeshewa nyingine ikiwemo Pugu Secondary, Kikakala, Weruweru, Tabora zote n.k. Kifupi shule nyingi kongwe unazozisikia ni za Kanisa Katoliki na zilikuwa na majina ya Kikatoliki mfano Kikakala iliitwa Marian, Weruweru Assupmpta n.k.
 
Sisi tuliopewa kuzifahamu "siri" za Ufalme wa MUNGU, tunalitizama tu hili "kanisa" la "kinafiki" na kulionea huruma maana tunajua nini utakuwa mwisho wake.
Soma Ufunuo 17:1-2
1 Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
 
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kukutana na Baraza la Maaskofu Katoliki anzania (TEC) leo Juni 25, 2021

Rais atakutana nao katika Makao Makuu ya TEC, Kurasini

==========

5:30 Asubuhi: Rais Samia Suluhu ameshafika na kuimbwa wimbo wa Taifa, kinachoendelea kwa sasa ni utambulisho wa maaskofu

KILAINI AELEZEA HISTORIA YA BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA
5:45 Asubuhi:
Anaeongea kwa sasa ni Askofu Method Kilaini na anaongelea historia ya baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania. Kilaini amesema Baraza la Maaskofu ndio uongozi wa Kanisa Katolika na lilianza na ujio wa Kanisa Katoliki mwaka 1860.

Askofu Kilaini amesema Wamisionari walikuja na mambo matatu muhimu ambayo ni kueneza dini, kutibu wagonjwa na Elimu.

Kilaini amesema waingereza walikuwa wanaitawala Tanganyika kwa udhamini wa Umoja wa Mataifa hivyo hawakutaka kuwekeza. Ndipo Kanisa lilipoamua kujaza Ombwe lililobaki ambapo mwaka 1928 waliwekeana sera kwamba msisitizo uwe Shule. Kilaini anaendelea kwa kusema maaskofu waliwekea sera endapo fedha ni kidogo na inabidi kuchagua kujenga shule au Kanisa, ni bora kuchagua shule na kuacha kanisa na ndio umekuwa msimamo wa kanisa hadi leo.

Kilaini: Mwaka 1956 wakaunda Rasmi umoja wa barza la maaskofu linaloitwa TEC na kati ya waliounda, askofu mwafika alikuwa mmoja, Laurian Rugambwa akiwa askofu wa Rutabwa na polpole waliingia mpaka sasa unaona nyuso za waafrika pekee.

Baraza hili liliendelea na sera hiyohiyo mpaka tulivyofika Uhuru mwaka 1961 na wakaunga mkono juhudi zote alizokuwa anazinya mwalimu Julius Nyerere.

Alivyofika mwaka 1969/70, Nyerere alisema naona mna shule nyingi lakini nataka ziwe za watu wote, akazitaifisha. Mwaka 1970 wakati anataifisha, Baraza la Maaskofu Tanzania lilikuwa na shule za msingi 1,420. Shule za sekondari 44, vyuo vya ualimu nane halafu shule za ufundi ambazo hazikutaifishwa za wavulana 15 na wasichana 48.

Na hizi zilizotaifishwa, mama utakumbana na hii historia katika utawala wako kwasababu mashule mengine yako katikati ya mission, mbele ni kanisa, nyuma ni nyumba ya mapadri na kushoto nyumba ya kanisa, sasa tukotuko lakini tunaenda vizuri, miaka mingi tumekwenda kwenda lakini kila mara inabidi kutia nguvu sana ili kuwaza kukaakaa kwasababu hiki cha katikati hiki ni kiserikali serikali na kilichozunguka ni kimisheni kimesheni, imekuwa ni changamoto kila mara.

Tunakushukuru mama, unapoongea Lugha yako tunaipenda, usione tumevaa mabarakoa wote hapa, maaskofu wanatabasamu sana hapa, ni kwasababu ya matamko yako unayatoa, wote wanafurahi.

Askofu Mkuu(Gervas Nyaisonga)-Rais wa TEC: RISALA YA MAASKOFU

  • Hiki ni chombo cha juu kabisa cha uongozi wa kanisa katoliki Tanzania hivyo ujio wako kwetu na uwepo wako hapa, wewe ni kiongozi mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni heshma kubwa sana kwetu sisi wanabaraza pia ni ishara ya wazi kwamba unathamini baraza hili na mchango wake kwa maendeleo ya watanzania wote.
  • Tunamshukuru Mungu kukubali wewe kuwa kiongozi wa Taifa letu na tunakuombea hekima, afya na mshikamano, Mungu akuwezeshe kutimiza majukumu yako vyema. TECL linakuahidi ushirikiano katika kusimamia ustawi wa watanzania.
  • Tunakuomba uimarishe utawala wa sheria na ujenzi wa Taasisi imara za kidemokrasia ambazo ndio msingi wa utawala bora.
Mheshimiwa Rais tukiwa tunakupongeza na kukushukuru kuwa nasi hapa, hatuna budi tukushirikishe masuala kadhaa kwa ajili ya kutuwezesha sisi kama taasisi inayoshughulika na maendeleo ya kiroho na ustawi wa Watu.
  • Katika utekelezaji wa majukumu yetu, hatuna budi kushukuru ushikiano mzuri uliopo kati ya didi kama taasisi na serikali
  • Mheshimiwa Rais mwaka 2016 sera mbalimbali zilibadilika na kutukwamisha kutoa huduma za kijamii hasa elimu bila kujali uwekezaji mkubwa uliofanywa na kanisa kabla ya hapo hii imesababisha hasara kubwa kifedha na hata rasilimali nyingine pamoja na rasilimali watu
  • Lengo la Shule zetu sio kufanya biashara bali kutoa huduma bila kujali uwezo wa wazazi wanaotaka kueleimisha watoto wao kama ilivyo Sera ya Serikali yako ya Awamu ya Sita

RAIS SAMIA SULUHU
  • Niwashukuru kwa pongezi mlizonipa kwa kushika wadhifa huu mzito na kweli niwaambie ni mzito na mwanzo ni mgumu sana. Lakini mwa ushirikiano na maombi yenu nina imani tutavuka salama,"- Rais Samia Suluhu Hassan
  • Nawashukuru kwa kuwa pamoja na Serikali katika kipindi kizito tulichompoteza kiongozi wetu Hayati John Pombe Magufuli, kwa umoja wetu tuliomba na kushirikiana tukamaliza msiba kwa amani na utulivu na Taifa letu likabaki salama
  • Serikali inawapongeza Kanisa Katoliki kwa mchango wenu kwenye jamii, kwani mmewalea wanadamu kiroho, kiimani, kimaadili, kudumisha amani, kustawisha maisha ya wananchi, kupambana na umaskini, kupunguza tatizo la ajira na kuchochea maendeleo
  • Lengo langu ni kukutana na dhehebu moja moja la dini ili kujua mema na changamoto mlizonazo ili Serikali iweze kujua jinsi ya kuzifanyia kazi

Kichwa cha habari ulichotumia kina ukakasi na nia ovu ambayo sababu yake siioni- UMEHARIBU
 
Kanisa katoliki halijaweza kabisa kutuletea viongozi watenda haki,wenye upendo na kujali maisha na utu wa watu!! Ukiacha hawa wadogo tizama yule wa awamu yakwanza,yatatu na tano!! Watu tumeteseka mmmno na kanisa halikukemea bali kusifu!..
Hilo lilikuwa kanisa langu nikalipotezea. Ina maana kwenye huo mkutano wao wa leo wala hawajagusia kuhusu katiba mpya? Utashangaa mchakato wa katiba mpya ukirejea wakatoa watu wa kwenda kuongelea jambo wasilolipa msukumo.
 
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kukutana na Baraza la Maaskofu Katoliki anzania (TEC) leo Juni 25, 2021

Rais atakutana nao katika Makao Makuu ya TEC, Kurasini

==========

5:30 Asubuhi: Rais Samia Suluhu ameshafika na kuimbwa wimbo wa Taifa, kinachoendelea kwa sasa ni utambulisho wa maaskofu

KILAINI AELEZEA HISTORIA YA BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA
5:45 Asubuhi:
Anaeongea kwa sasa ni Askofu Method Kilaini na anaongelea historia ya baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania. Kilaini amesema Baraza la Maaskofu ndio uongozi wa Kanisa Katolika na lilianza na ujio wa Kanisa Katoliki mwaka 1860.

Askofu Kilaini amesema Wamisionari walikuja na mambo matatu muhimu ambayo ni kueneza dini, kutibu wagonjwa na Elimu.

Kilaini amesema waingereza walikuwa wanaitawala Tanganyika kwa udhamini wa Umoja wa Mataifa hivyo hawakutaka kuwekeza. Ndipo Kanisa lilipoamua kujaza Ombwe lililobaki ambapo mwaka 1928 waliwekeana sera kwamba msisitizo uwe Shule. Kilaini anaendelea kwa kusema maaskofu waliwekea sera endapo fedha ni kidogo na inabidi kuchagua kujenga shule au Kanisa, ni bora kuchagua shule na kuacha kanisa na ndio umekuwa msimamo wa kanisa hadi leo.

Kilaini: Mwaka 1956 wakaunda Rasmi umoja wa barza la maaskofu linaloitwa TEC na kati ya waliounda, askofu mwafika alikuwa mmoja, Laurian Rugambwa akiwa askofu wa Rutabwa na polpole waliingia mpaka sasa unaona nyuso za waafrika pekee.

Baraza hili liliendelea na sera hiyohiyo mpaka tulivyofika Uhuru mwaka 1961 na wakaunga mkono juhudi zote alizokuwa anazinya mwalimu Julius Nyerere.

Alivyofika mwaka 1969/70, Nyerere alisema naona mna shule nyingi lakini nataka ziwe za watu wote, akazitaifisha. Mwaka 1970 wakati anataifisha, Baraza la Maaskofu Tanzania lilikuwa na shule za msingi 1,420. Shule za sekondari 44, vyuo vya ualimu nane halafu shule za ufundi ambazo hazikutaifishwa za wavulana 15 na wasichana 48.

Na hizi zilizotaifishwa, mama utakumbana na hii historia katika utawala wako kwasababu mashule mengine yako katikati ya mission, mbele ni kanisa, nyuma ni nyumba ya mapadri na kushoto nyumba ya kanisa, sasa tukotuko lakini tunaenda vizuri, miaka mingi tumekwenda kwenda lakini kila mara inabidi kutia nguvu sana ili kuwaza kukaakaa kwasababu hiki cha katikati hiki ni kiserikali serikali na kilichozunguka ni kimisheni kimesheni, imekuwa ni changamoto kila mara.

Tunakushukuru mama, unapoongea Lugha yako tunaipenda, usione tumevaa mabarakoa wote hapa, maaskofu wanatabasamu sana hapa, ni kwasababu ya matamko yako unayatoa, wote wanafurahi.

Askofu Mkuu(Gervas Nyaisonga)-Rais wa TEC: RISALA YA MAASKOFU

  • Hiki ni chombo cha juu kabisa cha uongozi wa kanisa katoliki Tanzania hivyo ujio wako kwetu na uwepo wako hapa, wewe ni kiongozi mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni heshma kubwa sana kwetu sisi wanabaraza pia ni ishara ya wazi kwamba unathamini baraza hili na mchango wake kwa maendeleo ya watanzania wote.
  • Tunamshukuru Mungu kukubali wewe kuwa kiongozi wa Taifa letu na tunakuombea hekima, afya na mshikamano, Mungu akuwezeshe kutimiza majukumu yako vyema. TECL linakuahidi ushirikiano katika kusimamia ustawi wa watanzania.
  • Tunakuomba uimarishe utawala wa sheria na ujenzi wa Taasisi imara za kidemokrasia ambazo ndio msingi wa utawala bora.
Mheshimiwa Rais tukiwa tunakupongeza na kukushukuru kuwa nasi hapa, hatuna budi tukushirikishe masuala kadhaa kwa ajili ya kutuwezesha sisi kama taasisi inayoshughulika na maendeleo ya kiroho na ustawi wa Watu.
  • Katika utekelezaji wa majukumu yetu, hatuna budi kushukuru ushikiano mzuri uliopo kati ya didi kama taasisi na serikali
  • Mheshimiwa Rais mwaka 2016 sera mbalimbali zilibadilika na kutukwamisha kutoa huduma za kijamii hasa elimu bila kujali uwekezaji mkubwa uliofanywa na kanisa kabla ya hapo hii imesababisha hasara kubwa kifedha na hata rasilimali nyingine pamoja na rasilimali watu
  • Lengo la Shule zetu sio kufanya biashara bali kutoa huduma bila kujali uwezo wa wazazi wanaotaka kueleimisha watoto wao kama ilivyo Sera ya Serikali yako ya Awamu ya Sita

RAIS SAMIA SULUHU
  • Niwashukuru kwa pongezi mlizonipa kwa kushika wadhifa huu mzito na kweli niwaambie ni mzito na mwanzo ni mgumu sana. Lakini mwa ushirikiano na maombi yenu nina imani tutavuka salama,"- Rais Samia Suluhu Hassan
  • Nawashukuru kwa kuwa pamoja na Serikali katika kipindi kizito tulichompoteza kiongozi wetu Hayati John Pombe Magufuli, kwa umoja wetu tuliomba na kushirikiana tukamaliza msiba kwa amani na utulivu na Taifa letu likabaki salama
  • Serikali inawapongeza Kanisa Katoliki kwa mchango wenu kwenye jamii, kwani mmewalea wanadamu kiroho, kiimani, kimaadili, kudumisha amani, kustawisha maisha ya wananchi, kupambana na umaskini, kupunguza tatizo la ajira na kuchochea maendeleo
  • Lengo langu ni kukutana na dhehebu moja moja la dini ili kujua mema na changamoto mlizonazo ili Serikali iweze kujua jinsi ya kuzifanyia kazi
Kwa maana nyingine LEO shilingi zimekutana.
 
1 Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
Ndugu yangu watu wengi wanaojiita "Wakristo" hawajui kuwa Ufunuo aya ya 17 na 18, anayezungumziwa ni kanisa katoliki. Siri hii nawapa leo, yule KAHABA ni kanisa katoliki na mji ule mkubwa wenye uflame juu ya wafalme wa nchi ni jiji la Roma.

Mwenye masikio na asikie.
 
Back
Top Bottom