Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Hilo limetokea wakati Rais Samia Hassan akizungumza na Wananchi wa Runzewe, leo Oktoba 16, 2022

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka aliwasisitiza Wananchi kuzaa zaidi kwa kuwa madarasa na vituo vya afya vinajengwa na wawekezaji wanaongezeka Nchini

Rais Samia akajibu “Hilo la zaeni tu hapana, jana nimesimama Buseresere naambiwa kituo kimoja kinazalisha watoto 1000 kwa mwezi, sasa hapo baada ya miaka mitatu ni madarasa mangapi? Kama ni vituo vya afya vingapi, tani za chakula ni ngapi? Punguzeni kidogo spidi.”
 
Kuzaaa zaa hovyo ni sera ya jiwe, huyu mwenezi wa CCM naye hana akili kama anaamini kwenye watu kuzaa hovyo kisa miradi, huku Tanzania na Dunia ikikabiliwa na ukame na njaa.

Ukosefu wa ajira, uvamizi wa vyanzo vya maji, uvamizi wa misitu, machinga kujaa mitaani na kuziba barabara halafu unawaambia watu wazae watoto 9?
 
Ahsante sana Mhe.Rais na mwenyekiti wangu hakika leo umeweza kunifurahisha sana haiwezekani kijana aongee bila kufikiri.

Kuzaa na kuongezeka ni mpango wa Mungu lakini hiyo haina maana mtu azae bila mpangilio. Tangu mwanzo nilisema Shaka sio mbadala wa Polepole naona yanatimia.
 
Kuzaa hovyo ndiko mpaka leo kumetufikisha hapa kwenye maisha magumu,ukuaji wa miji haueleweki Wala mpangilio,sisi wenyewe kwetu tumezaliwa 13 maisha tight kinyama.Siungi mkono Sera hiyo hata kidogo
 
Kwenye nchi ambayo watu wanaozalisha (producers) ni wachache na Watumiaji (consumers) ni wengi unawezaji kusema watu wazaliane hovyo?

Ongezeko la watoto wasio na baba ni kubwa na hao ndo wanazalisha vibaka, wezi, mashoga, malaya n.k sababu wanakosa malezi from the ground

Pia familia nyingi zina watoto wengi hawawezi kuwapatia huduma na humuachia Mungu awalelee

Hii haikubariki BIG UP samia kwa hili.
 
Yeye kuzaa hataki ameleft kwenye group akajiunga na upunde wa mvua afu anataka watu wazae zae TU hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…