Rais Samia ampinga Shaka kuhusu kuzaa zaa
Namuunga mkono Samia kwa hili kwa 100%.
Haiwezekani watu wazae tu, watu wanapaswa kuzaa kwa uzazi wa mpango.
 
Mwisho wa kuzaa sana kwa wasukuma ni Silaha ya kupata Kura nyingi Za kuiondoa ccm madarakani
Hawana akili hizo, wengi wao masuala ya siasa yamewapita kushoto wapo porini na ng'ombe zao
Jiwe aliwaamsha kidogo ila bado sana
 
Wanasiasa wasiotanguliza maslahi ya nchi badala yake wanaweka kwanza mbele ya chama ni janga kubwa kwa nchi yetu.
Shaka alitaka kuwafurahisha Wasukuma,sababu wao upends kuzaa watoto wengi na kuwa na familia kubwa. Viongozi hawana budi kulisemea ili .Ongezeko la watu lisiloendana na rasilimali ni janga kubwa litakalonyemelea Taifa na watu wake. Kwa hili tuache unafiki wa kisiasa.
 
Nafasi ya ukatibu mwenezi kwa wengine maana yake ni kusema tu kila unapopewa nafasi, tena ikibidi hata usijipe muda wa kutafakari kile unachotaka kusema.
Shaka anaweza kuwa mwenezi wa Chama tawala Tanzania pekee. Hata Sheli Sheli haiwezekani.
 
Nchi kama India na China uchumi wake unakuwa kila siku na hii ni kwa sababu wanategemea soko la ndani kuliko hata la nje.

Unapokuwa na idadi kubwa ya watu maana yake ni kuwa una uwezo wa kuwa na nguvu kazi ya kutosha na pia soko la ndani la bidhaa utazozalisha.

Nashangaa kusikia mkuu wa nchi kutoa tamko watu wapunguze kuzaliana kisa tu ana hofu ya kujenga madarasa na Zahanati.

Zahanati na madarasa ni ngumu Kujenga?

5BBDFB61-E62F-49E0-89D0-526F87C30DA4.jpeg
 
Mbona mwendazake alitwambia TUFTATUE TU. Nini kimebadilika nchi hii?
 
Zaeni ili sisi Walimu Tuendelee kulamba Asali

Hizi fani
Kilimo
Ualimu
Udaktari

Tutalamba Asali Hadi mwisho wa nchi
 
Dunia yote inasisitiza na kuweka mkazo katika kutoa Elimu juu ya uzazi wa mpango, huwezi ukawa na watoto wengi wakati hata kuwalea huwezi, kazi siyo kuzaa tu Bali lazima ufahamu kuwa mtoto akizaliwa anahitaji Mahitaji mengi Sana ambapo tunaona wengi wakishidwa na kuishia kutelekeza watoto au kuwaachia wazazi wao wakihangaiika na malezi ya wajukuu zao,

Tunataka kila mtu awe na watoto anao weza kuwahudumia na kuwalea vizuri, kwani Kuna faida gani mtu akiwa na watoto wengi asioweza hata kuwagharamia madaftari na sare za shule? Watakuwa na mchango gani katika soko na uchumi wa nchi wakati wamekulia na kuishi katika umaskini mkubwa kutokana na wazazi kuelemewa na malezi yao? Watakuwa na mchango gani kwa uchumi Kama watoto Hawa wataishia kuwa watoto wa mitaani? Huoni itakuwa Ni mzigo kwa serikali? Huoni hata Hawa watoto watakuwa hawajatendewa haki kwa wazazi wao kushindwa kuwapa Mahitaji ya msingi? Huoni watakosa msingi mzuri wa kiuchumi ulioandaliwa na wazazi wao?

Shida yako wewe ni kuwa unachuki kubwa Sana na Rais wetu mpendwa, kwako Hakuna jema alilolifanya na analoweza akalifanya ukapongeza,Hata hivyo Ni demokrasia na upo huru kufanya hivyo maana Ni mtizamo wako ulivyo, lakini nasi pia tunaompenda Rais wetu hasa kutokana na uchapa kazi wake tutaendelea kumtetea na kumsemea kwa kadri ya uwezo wetu, maana kila mtu anaziona juhudi za mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani katika kuijenga nchi hii na kuona kila mtanzania anainuka kiuchumi,

Mimi binafsi Nitaendelea kumsemea Rais wangu mama Samia kwa yote mazuri afanyayo ,labda nikose hela ya kununua vocha siku hiyo, lazima Tumpe Faraja na nguvu ya kusonga mbele zidi ya wachache mliojaa chuki katika mioyo yenu hasa baada ya kuona akichanja mbuga kuwatumikia watanzania wanyonge wanaoendelea kumuunga mkono mh Rais wetu
 
Hajampinga kachagiza ni kama kachomekea tuh, upinzani wacheni kutafuta kosa moja kwanye mazuri elfu moja
 
Hilo limetokea wakati Rais Samia Hassan akizungumza na Wananchi wa Runzewe, leo Oktoba 16, 2022

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka aliwasisitiza Wananchi kuzaa zaidi kwa kuwa madarasa na vituo vya afya vinajengwa na wawekezaji wanaongezeka Nchini

Rais Samia akajibu “Hilo la zaeni tu hapana, jana nimesimama Buseresere naambiwa kituo kimoja kinazalisha watoto 1000 kwa mwezi, sasa hapo baada ya miaka mitatu ni madarasa mangapi? Kama ni vituo vya afya vingapi, tani za chakula ni ngapi? Punguzeni kidogo spidi.”
Kweli Kabisa hasa Kanisa la KKKT Moshi wanawadanganya waumini wao wazae watoto wengi ili hali hawawatembelei wala hawajui wanakula nini........
 
Mkuu nadharia yako sio sahihi kabisa. Idadi kubwa ,ya watu sio indicator ya ukubwa wa soko la ndani. Kipzto cha raia ndo determinant kubwa ya soko la ndani; Denmark ni nchi ndogo na ina watu kama milioni tano hivi lakini ni soko kubwa kuliko afrika,mashariki nzima yenye watu milioni 200 . Marekani inq watu milioni mia tatu na ushee lakini ni soko kubwa kuliko india au china zenye wati bilioni moja na nusu kila moja. Mtawalia

Soko la China hivi karibuni limekuwa kubwa kwa kasi kutokana na kipato chq,mtu mmoja mmoja kuongezeka.

Watu wasio na kipato ni disaster katika nchi na kichocheo kikubwa cha uhalifu.

Wawekezaji wanaotarget soko la ndani huangalia per capita income kama kigezo kimojawapo wanapotaka kuwekeza katika nchi.
 
Back
Top Bottom