Rais Samia ampinga Shaka kuhusu kuzaa zaa
Nakubaliana na Mwenyekiti wangu kwa [emoji817]%,haiwezekani uwepo wa madarasa , huduma za afya na wawekezaji iwe kigezo Cha watu kuzaliana hovyo ,

Kuzaa Kuna maaana pana sana, yaani chakula, mavazi pamoja na malazi, haiwezekani mtu azae harafu watoto wanatembea matako wazi, wanashindia mlo mmoja na mahali wanapolala hata mbwa wa dimond hawezi kupumzika hata kwa dakika moja

Rais asiishie hapo tu, watu waelimishe, ikibidi kuwe na Sera ya taifa watu wazae mwisho watoto watatu tu,

hapa ninapoishi Kuna jirani yangu, kula kwake Hadi aje kunichotea maji ndo apate pesa ya matumizi,chakusikitisha ana watoto wanne,na juzi tu mke kajifungua mtoto wa tano,Sasa unabaki kujiuliza anamzalia Nani,au Kuna mahali mwenzangu nanampango wa kwenda kuuza hao watoto!!? Huwa natamani kumchalaza bakora Ila Basi tu.
 
Raisi wangu mpendwa yuko sahihi kabisa, sisi Wanadamu tunafikiria hii Dunia ni kubwa wakati sio kweli, tukizaliana kama Mchwa tutamaliza Rasilimali za hii sayari matokeo yake tutaangamia kama viumbe vilivivyopita Madinosaurs.

Hebu angalia hii picha iliyopigwa na chombo cha anga za juu cha China kikionyesha Dunia na Mwezi wake.😟

Tupange uzazi wa mpango laa sivyo Cannibalism ndio itakua future yetu.

Tuacheni kuharibu Mazingira tutumie Condom wakati wa kustarehe.

fYBHA8iF5DUmfQveFAtVFH-1280-80.jpg

👆Dunia yetu na Mwezi wake tafakari chukua hatua.

Very fragile.
 
Kuzaa bila mpango kunaongeza ushirikina, mtu anaamua kumchukuwa NDUGU yake msukule ili maisha yaendelee. Hata wazazi wanaweza kubebwa ili tu familia ijitoe katika ufukara.
 
Kituo kimoja tu cha Buseresere watoto alfu kwa mwezi?
Imagine Nchi mzima kwa ujumla
whew.png
 
Hilo limetokea wakati Rais Samia Hassan akizungumza na Wananchi wa Runzewe, leo Oktoba 16, 2022

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka aliwasisitiza Wananchi kuzaa zaidi kwa kuwa madarasa na vituo vya afya vinajengwa na wawekezaji wanaongezeka Nchini

Rais Samia akajibu “Hilo la zaeni tu hapana, jana nimesimama Buseresere naambiwa kituo kimoja kinazalisha watoto 1000 kwa mwezi, sasa hapo baada ya miaka mitatu ni madarasa mangapi? Kama ni vituo vya afya vingapi, tani za chakula ni ngapi? Punguzeni kidogo spidi.”
Shaka mswahili anajua wasukuma washamba flani wa kupenda kuzaa hovyo hawajastaarabika ni dharau halafu wao wanachekelea
 
Shaka mswahili anajua wasukuma washamba flani wa kupenda kuzaa hovyo hawajastaarabika ni dharau halafu wao wanachekelea
Pale Wasukuma ni minority Wasumbwa hawapendi kuzaa kama Wasukuma.
Na sio waharibifu wa mazingira hawakati miti ovyo kwasababu wanategemea Nyuki kwa ajili ya asali.

Ndio maana penye Msumbwa mapori bado yako

Msukuma na Mhutu ndio adui wa Mapori wakiachiwa wanaweza kuyamaliza ndani ya miaka mitano.
 
Yoda na imhotep acheni uoga, hii nchi ni kubwa mno zaeni tu na hamna uwezo wa kuijaza…. mmeoshwa ubongo mkasuuzwa.
 
Shaka mswahili anajua wasukuma washamba flani wa kupenda kuzaa hovyo hawajastaarabika ni dharau halafu wao wanachekelea
Hivi kwa nini huwa mnapenda kutumia lugha ya dharau kwa makabila ya wenzenu? Wewe unawaona wasukuma hawajielewi! Je unawazidi maisha? Ushawahi kuwalisha au kuwasaidia kulea watoto! Wako wengi tu wanamaisha mazuri kukuzidi wewe na ukoo wako! Punguza dhararu man!
 
Pale Wasukuma ni minority Wasumbwa hawapendi kuzaa kama Wasukuma.
Na sio waharibifu wa mazingira hawakati miti ovyo kwasababu wanategemea Nyuki kwa ajili ya asali.

Ndio maana penye Msumbwa mapori bado yako

Msukuma na Mhutu ndio adui wa Mapori wakiachiwa wanaweza kuyamaliza ndani ya miaka mitano.
Runzewe huwezi kusema wasukuma ni manority! Kahama na bukombe yote ni asili ya wasumbwa ila kwa sehemu kubwa shughuli za pale zinatawaliwa na wasukuma wahamiaji! Hata nyakanzi kwa sehemu kubwa bado wasukuma wanaiendesha! Wasumbwa ni kabila dogo sidahini kama wanaweza kuwa na majority runzewe!
 
Ndugu utakuwa Msukuma ondoa kwanza hiyo boriti ya Kikabila ndio tuwe na mjadala mzuri.
 
Ndugu utakuwa Msukuma ondoa kwanza hiyo boriti ya Kikabila ndio tuwe na mjadala mzuri.
Sasa mi kiwa msukuma sio shida! Msukuma na ukabila wapi na wapi? Niko Dar mkuu! Hayo maeneo nayajua sana huwezi kunidanganya hata kidogo kuanzia Tinde-isaka-kahama-runzewe-nyakanazi -rusumo mpaka benako nayajua maeneo hayo vizuri!
 
Back
Top Bottom