Rais Samia ampinga Shaka kuhusu kuzaa zaa
Wewe mwenye watoto wawili una maisha gani mazuri ?
Pamoja na kuwa na kipato cha kawaida ninawasomesha shule nzuri yenye elimu bora, wanakula, kulala na kuvaa vizuri sana. Wanapata malezi bora ya Mama yao na Baba yao kwa ukaribu sana. Na mwisho nimeweza kujenga nyumba mbili nzuri na za kisasa kabisa
 
Hilo limetokea wakati Rais Samia Hassan akizungumza na Wananchi wa Runzewe, leo Oktoba 16, 2022

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka aliwasisitiza Wananchi kuzaa zaidi kwa kuwa madarasa na vituo vya afya vinajengwa na wawekezaji wanaongezeka Nchini

Rais Samia akajibu “Hilo la zaeni tu hapana, jana nimesimama Buseresere naambiwa kituo kimoja kinazalisha watoto 1000 kwa mwezi, sasa hapo baada ya miaka mitatu ni madarasa mangapi? Kama ni vituo vya afya vingapi, tani za chakula ni ngapi? Punguzeni kidogo spidi.”
Pole sana,
Rais kwenye shule na Zahanati alienda mbali.

Nenda Tanzania National Beural of Statistics usome:

1: Maternal mortality rate/idadi ya wamama wanaokufa wakati wa uzazi.

2: Neonatal mortality rate/vifo kwa watoto chini ya umri mwezi mmoja.

3: Under 1 year mortality rate/vifo chini ya umri wa mwaka mmoja.

4: Under five mortality rate/vifo chini ya miaka mitano.

5: Anaemia in under five/ watoto wenye ukosefu wa damu chini ya miaka mitano.

6: Malnutrition in under five/ lishe duni chini ya miaka mitano.

7: Fertility rate in urban vs rural.

8: Income per capital in urban vs rural.

NB: Jitahidi kusoma sababu ya matatizo tajwa hapo juu. Mwisho sema unataka kujenga taifa la namna gani.
 
Nchi kama India na China uchumi wake unakuwa kila siku na hii ni kwa sababu wanategemea soko la ndani kuliko hata la nje.

Unapokuwa na idadi kubwa ya watu maana yake ni kuwa una uwezo wa kuwa na nguvu kazi ya kutosha na pia soko la ndani la bidhaa utazozalisha.

Nashangaa kusikia mkuu wa nchi kutoa tamko watu wapunguze kuzaliana kisa tu ana hofu ya kujenga madarasa na Zahanati.

Zahanati na madarasa ni ngumu Kujenga?

View attachment 2389621
Hakuna nchi yenye sera kali ya uzazi wa mpango kama China elewa hilo. Pamoja na uchumi mkubwa no more than one child per couple. Una maoni gani kulinganisha na sisi makapuku tunaomba hadiisaada ya matundu ya vyoo?
 
Hilo ni jambo ovu sana
Kweli Kabisa hasa Kanisa la KKKT Moshi wanawadanganya waumini wao wazae watoto wengi ili hali hawawatembelei wala hawajui wanakula nini........
 
Hakuna msomi aliyemjia juu Samia kwa kusema mpunguze speed ya kuzaana.
Hizo ni porojo zako tu mataga kujifanyisha nyutro kinafiki.
JPM alisema tuzaane tu 'wasomi ' wakamjia juu na umuhinu wa kizazi wa Mpango

Samia kasema tupunguze speed 'wasomi wetu' wamemjia juu na takwimu za umuhimu wa kuwa na watu wengi

Pohamba nikiwa Rais ntasema tuzaane sana japo tupunguze speed
 
Uko sahihi mkuu kwa 100%
Raisi wangu mpendwa yuko sahihi kabisa, sisi Wanadamu tunafikiria hii Dunia ni kubwa wakati sio kweli, tukizaliana kama Mchwa tutamaliza Rasilimali za hii sayari matokeo yake tutaangamia kama viumbe vilivivyopita Madinosaurs.

Hebu angalia hii picha iliyopigwa na chombo cha anga za juu cha China kikionyesha Dunia na Mwezi wake.[emoji45]

Tupange uzazi wa mpango laa sivyo Caniballism ndio itakua future.

Tuacheni kuharibu Mazingira tutumie Condom wakati wa kustarehe.

View attachment 2389316

[emoji115]Dunia yetu na Mwezi wake tafakari chukua hatua.

Very fragile.
 
Pamoja na kuwa na kipato cha kawaida ninawasomesha shule nzuri yenye elimu bora, wanakula, kulala na kuvaa vizuri sana. Wanapata malezi bora ya Mama yao na Baba yao kwa ukaribu sana. Na mwisho nimeweza kujenga nyumba mbili nzuri na za kisasa kabisa
Huna hata viatu , acha kudanganya mkuu.
 
Hii nchi haipaswi kujazwa yote na Homo Sapiens tu, yanapaswa kubaki maeneo ya kutosha kwa ajili ya Simba, vifaru, Tembo, Twiga na wanyamapori wengine.

Yanapaswa kubaki maeneo ya kutosha kulima, open space, misitu n.k

Halafu kuijaza tu nchi huku mkiwatishwa gharama wengine ni ujinga na ujuha. Madawati ya watoto wenu, barabara mnazopita, hospital mnazotibiwa wengi mnaozaana sana hata hamjazilipia kodi ya maana, huo mzigo wa kodi wanabebeshwa wafanyabiashara na wafanyakazi wachache kuwahudumia wafyatuaji na wajazaji nchi hoehae.
Yoda na imhotep acheni uoga, hii nchi ni kubwa mno zaeni tu na hamna uwezo wa kuijaza…. mmeoshwa ubongo mkasuuzwa.
 
Hii ndio sababu inayokufanya utake kuwa na rundo la watoto kama timu ya mpira??
Ukitaka kujua umuhimu wa watu wengi waulizeni Ukrain, wakati wao wanamibilise watu 15000 Mrusi yeye anamobilise watu 300,000 alafu unaenda pambana naye
 
Kuzaaa zaa hovyo ni sera ya jiwe, huyu mwenezi wa CCM naye hana akili kama anaamini kwenye watu kuzaa hovyo kisa miradi, huku Tanzania na Dunia ikikabiliwa na ukame na njaa.

Ukosefu wa ajira, uvamizi wa vyanzo vya maji, uvamizi wa misitu, machinga kujaa mitaani na kuziba barabara halafu unawaambia watu wazae watoto 9?
Sio kuzaa ovyo.Inatakiwa kuzaa zaidi kupitia ndoa.Hapo Shaka yuko sahihi. Ulaya majumba yanaongezeka yasiyo na watu na majeshi yanakosa makruta.Sera zao ni hizo za kupunguza kuzaa.
 
Ulaya yenyewe unaisikia tu kwenye bomba halafu unakuja kuandika utumbo hapa.
Sio kuzaa ovyo.Inatakiwa kuzaa zaidi kupitia ndoa.Hapo Shaka yuko sahihi. Ulaya majumba yanaongezeka yasiyo na watu na majeshi yanakosa makruta.Sera zao ni hizo za kupunguza kuzaa.
 
Watu kama wewe wazazi wenu wangetumia condom msitokee ingekuwa faida kubwa kwa taifa hili kwa sababu mmegeuka mizigo tu kwa ujinga wenu.
Mama yako na baba yako wasingezaa ovyo inawezekana wewe usingezaliwa
 
Watu kama wewe wazazi wenu wangetumia condom msitokee ingekuwa faida kubwa kwa taifa hili kwa sababu mmegeuka mizigo tu kwa ujinga wenu.
Sasa kwanini usingeshauri wazazi wako na wao wakatumia kondom ili wewe usuzaliwe wafanye uzazi wa mpango?yaani baada ya wewe kuzaliwa ndo unadai uzazi wa mpango?ungekuwa bado upo viunoni mwa baba yako ungedai kweli uzazi wa mpango?basi ngoja nikwambie kitu HAKUNA MTOTO ANAYEZALIWA KWA BAHATI MBAYA.wote wanazaliwa kutoka na mipango ya Mungu kwa viumbe vyake.
 
fYBHA8iF5DUmfQveFAtVFH-1280-80.jpg


Nilikuwa naiangalia hii Picha hadi machozi yakanibubujika.

Mimi shughuli zangu huwa zinanifanya nzunguke karibia Nchi nzima ninaona madhara ya utitiri wa watu kwenye mazingira

Ni miaka ya 80 tu Nji hii ilikuwa na misitu iliyoshiba,sasa hivi hata ukiangalia kwenye Google Earth utajionea mwenyewe
 
Back
Top Bottom