Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

Hata ije time kutoka marekani Rais Samia na CCM watatangazwa washindi tu wa uchaguzi kutokana na kuwa na Sera na ajenda zinazokubalika kwa watanzania wengi ukilinganisha na upinzani ambao wenyewe Sera na ajenda zao Ni mgombea husika na hisia zake zinavyomtuma na kumpeleka
Mahera alishampa uhakika wa kushinda
 
Basi mumeo atakuwa PM
 
Ndugu uko nchi hii hii au ndio unatetea ugali wako🤔🤔🤔
Mwanzo waliandika kuelekea 2020 sasa wamebadilisha. Kuamini kuwa JPM ndio kigezo cha urais wa SSH ni kuwa na mawazo yenye kufanana na yale ya mlevi.

Ni viongozi wawili tofauti kabisa, uwezo wao wa kujenga hoja unatofautiana, uwezo wao wa kushawishi kwa kutumia akili za kiuongozi unatofautiana pia.
 
Punguza hasira ndo unaweza ukamwelewa jamaa hicho alichokisema jamaa kina ukweli au laa.
Huyo ni team JPM haihitaji akili za mwanasayansi anayekwenda mwezini na kurudi kuweza kumuelewa.

Amekariri maisha yale yale ya awamu ya tano.
 
Huyo Sekou Toure aliishi miaka ya sitini na sabini, karibu miaka 50 iliyopita. Hiyo busara yake ilikuwa na mashiko miaka hiyo lakini nyakati hizi za utandawazi ni iman tu potofu zilizopitwa na wakati.

Pia ni akili zile zile za uoga wa kujichanganya na dunia inayobadilika kila kukicha, huwezi kumkimbia mgeni kwa kumuita beberu, mwizi au kumtungia jina baya ili unaowaongoza wakuone kiongozi wa maana.
 
Huko huko mtaani ulipo wewe na mimi nipo pia. Mkuu biashara za watu zilizokuwa zimekufa awamu ya tano kwa sasa zinafufuka. Mzunguko wa pesa unaanza upya kabisa. Frems za maduka yale yanayouza bidhaa za utalii kule Masaki zinaanza kufanya biashara. Malori yanayosafirisha bidhaa za transit za kwenda Zambia, Malawi naZimbabwe yanapita kwa wingi huko njiani.

Huwezi kumlinganisha Samia na JPM, ni viongozi wawili tofauti kabisa.
 
Dogo amka kutoka usingizi wa mchana
 
Hizi ni kama ramli, CCM wakati wa uchaguzi huwa ni wengine kabisa, na ni vigumu sana kwa vyama vya upinzani kushika dola, watanzania watafute njia za kuinua maisha yao wenyewe wasitegemee chama chochote kurekebisha hali za wananchi.
 
Ati auto pilot!!!..nchi ikiongozwa kwa auto pilot utajenga lami kuliko awamu tatu zilizopita,utaajiri kiasi kile,utaongez $20b+ kwenye GDP!?...
 
Tunawapa madini wanachimba badala ya kuacha tuje kuyachimba wenyewe hata ikija kuwa Ni baada ya miaka 500.
Tuwatoe wamasai ili kujichanganya na waarabu.
Ni kweli ilikuwa muda huo wa kizamani Ila saivi tuko nyakati za kijanja na za kimaendeleo.


Tuko nyuma vibaya mno kwa nchi za Asia ambazo tulikuwa nazo sawa miaka iyo 50-60s.


Ngoja tujipendekeze kuendana na utandawazi
 
. Madai kuwa Mzee wa Msoga ana influence katika uongozi wake
Kati ya vitu vinavyonitia kichefuchefu kwenye huu utawala wa huyu mama ni hili la kuruhusu wastaafu kuingilia utawala wake.

Ukiona mpaka akina Makamba wanatangaza hadharani kwamba,.. 'kwa utawala wa mama tunalamba asali'..hiyo ni dhahiri kuna mengi ya hovyo nyuma ya pazia yanayofanywa na hao wastaafu akiwemo JK.
 
Upinzani wa nchi hii unaishi kinafhatia sana...Kama fisi wanaosubiri mkono udondoke
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Sidhani kama wastaafu wanashida iwapo wanatoa backstop kwa waliopo front line, tatizo ni zaidi ya wastaafu na hilo no tatizo la watanzania wote, kupenda maisha ya bure pasipo kuyatolea jasho; wenye nafasi wanajitungia sheria za ku access maisha bora kwakuzuia wengine, wasio na nafasi wanapiga vota wenye nafasi, kiufupi taifa zima kuwa morally corrupted...Hakuna tena utu wema kila mtu amegeuka kuwa mzabibu mwitu...
 
Mwamba baada ya kumshinda ya CDM ameham8shia goli huku katika harakati za kujifariji kidogo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…