Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

Acheni kujifariji na kutafuta faraja kwa watu ambao walishawapuuza nyie wapinzani mliokosa Sera na ajenda na kubakisha ubabaishaji tu na kudandia vimatukio tu vya mpito Kama ukungu wa asubuhi, Nani mwenye Akili Timamu wakuweza kuwafikiria au kuwapigia kura nyie? Nani wakuwaunga mkono nyie upinzani? Kwa Sera na ajenda zipi mlizonazo? Kwa ushawishi gani mlio nao kwa watanzania? Hamuoni kuwa watanzania walishawapuuza na kuwadharau kwa Sasa? Hamuoni kuwa watanzania walishawatupa mkono? Hamuoni kuwa watanzania hawataki kuwasikiliza kwa lolote? Hamuoni hata namna ambavyo hamsikilizwi Wala kutiliwa maanani na watanzania kwa lolote mtakalo ongea na kuzungumza?

Nani awape nchi wasaliti wakubwa Kama nyie? Nani awaamini vigeu geu Kama nyie? Unazani watanzania wamesahau akili zenu za 2015? Nani awaamini watu Kama nyie wa upinzani mliokosa dira na muelekeo? Nani awape Imani watu Kama nyie ambao hamueleweki hata mnachosimamia? Nani awaamini nyie mliokosa mizizi ya kila kitu? Nani awaamini nyie mliokosa hata safu Bora ya uongozi wa kueleweka? Nani awaamini nyie ambao hata kuandaa mtu wa kugombea Urais mnasubili atoke kwetu CCM? Nani awaamini nyie mnaokosa hata uwezo wa kujiongoza na kujisimamia wenyewe?

Kwa Taarifa yako Ni kuwa Rais Samia Ndio chaguo la mamilioni ya watanzania, Ndio Tumaini la watanzania katika kuwaletea maendeleo, Rais Samia Ndio kiongozi aliyebeba Imani ya watanzania, Raisi Samia Ndio kiongozi anayekubalika na kuaminika na watanzania kwa matendo na kauli zake, Hakuna wa kumtikisa Wala kumyumbisha Rais Samia,

Naona mmeanza kupata kiwewe baada ya kuona Kiwango Cha kukubalika kwa Rais Samia kinazidi kuongezeka Zaid, mmepata kiwewe baada ya kugundua kuwa makundi yote yanamkubali na kumuunga mkono Rais Samia, mnataka kujaribu kutuchonganisha CCM ili mpate kupumua, lakini kwa Taarifa yenu Ni kuwa CCM Ni moja, wanaccm ni wamoja, wanachama Ni wamoja na sote tupo pamoja chini ya Mwenyekiti wetu na Rais wetu mh mama Samia suluhu Hassani

Kazi iendeleee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Mwashambwa kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Ccm wamefanya nin Cha maana kwa miaka 60 waruhusu uchaguzi huru na haki kama wanajiamini
 
Tutapata KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA,

Hlyo ndo itazaa Tume huru ya Uchaguzi.
Pia elewa bavicha ni tone tu kati ya mamilioni ya Watanzania wanaodai KATIBA mpya.

So rudia tena kufanya calculation.

Ameeeen.
Wanadai katiba wakiwa chumbani?
 
Njoo mtaani huku uone watu wanavyomuongelea kiufupi hawamuelewi kabisa nenda hata facebook upate maoni ya raia kiukweli watu wamekataa kabisa kumuelewa na yeye anajua hilo pamoja na kwamba kajenga madarasa na blahblah kibao ila watu HAWAMUELEWI
Ni lini watu wa FACEBOOK wamewahi kuwa na akili? Wale watu bado wanafikiri Magufuli atagombea mwaka 2025.

Huko mtaani unaongelea wale wanaoitwa WANYONGE (The Wretched), sasa watu wamekubali kuitwa WANYONGE na aliyewaita amekufa, unadhani watamkubali mtu anayetaka kuwabadili kuwafanya binadamu wa maana?
 
Ndo ushangae waliosema Katiba mpya itaanza 2026, ghafula wakasikiliza sauti ya Walio chumbani!!
Umeshinda mkuu,umejibu kistaarabu mnoo.. tofaut na vijana wengi wa BAVICHA
 
Umeshinda mkuu,umejibu kistaarabu mnoo.. tofaut na vijana wengi wa BAVICHA
Mm Si Bavicha, bt nasimamia HAKI kusimama ktk Nchi.

Bavicha wakitoka Kwa mstari Huwa nashughulika nao Kwa hoja Kwa maslah mapana ya Nchi. Ameeeen.
 
Tangu nianze kufuatilia siass za nchi hii, sijawahi ona kiongozi wa CCM alie madarakani akikataliwa, kupingwa na kuongezewa vivyo sivyo kama Mama yetu wa leo.

Kwanini hali hii?

1. Mama kulinganishwa na Mwendazake

Mama kulinganishwa na Mwendazake na hapa ndipo hata baadhi ya wana-CCM wanapoungana na watanzania wengine kumuhukumu na kumuona hatoshi na wanaona ni bora 2025 watafute mgombea mwingine vinginevyo ni bora wachague mpinzani.

Kwanini Mwendazake anamgharimu?
Wakati wa Mwendazake, kuna kundi kubwa la watanzania waliamini wizi na ufisadi vilikuwa vimekomeshwa/ vimedhibitiwa jambo ambalo halikuwa kweli kwa asilimia 100.

Mwendazake alidhibiti vyombo vya habar, alidhibiti Bunge, mitandao na vyanzo vingine vya kupashana habari matokeo yske tuhuma za wizi na ufisadi Wakati wa Mwendazake havikupata nafasi.

Kingine ni Mwendazake kutumia media kuendesha propaganda za kumsifu na kumtukuza mambo ambayo sasa hayapo kwa kiwango kile na hivyo kuleta tofauti kubwa ya kimtazamo kati ya Mama na Mwendazake.

2. Kundi la Sukuma gang
Hili kundi ni kundi la watu wanaonekana kuwa na chuki dhidi ya huyu Mama na ndio wanachangia sana kuonyesha kuwa Mama hatoshi sababu tu hawampendi. Ni kama hawakuta Mama amrithi Mwendazake na hivyo kutumia madhaifu ya Mama kummaliza kisiasa mbele ya umma.

Na kama Mama angeshindwa kuendeleza miradi iliyoachwa na Mwendazake, basi hili kundi lingepata cha kusema na lingekuwa kinara katika kuwaongoza watu wamkatae Mama hiyo 2025.

Mama akijitahidi kukamilisha Miradi yote iliyoachwa na Mwendazake, basi atafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza nguvu za hili kundi mitandaoni na kwingineko

3. Madai kuwa Mzee wa Msoga ana influence katika uongozi wake
Madai haya ni moja ya mambo ambayo yanamgharimu sana Mama hasa ikizingatiwa Mzee wa Msoga anachukuliwa kama mtu alieacha rushwa na ufisadi vikatamalaki sana katika nchi hii.

Hivyo, madai kuwa Mama anafanya baahi ya mambo kwa influence ya Mzee wa Msoga, madai haya yanamgharimu sana kisiasa na 2025 atakuja kuona matokeo yake.

4. Madhaifu binafsi ya Mama
Madhaifu au mapungu haya ni pamoja na haya na kukithiri kwa tozo katika awamu yake, kauli za kuruhusu watu wale kulingana na urefu wa kamba zao, kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei, kuhamisha wamasai kule Loliondo, safari za mara kwa mara nje ya nchi, kauli zake za majukwaani na mambo mengineyo.

5. Jinsia yake
Ukweli mwingine unatokana na mila na desturi zetu plus mtazamo potofu wa jumla kwa baadhi ya watu kuwa Mwanamke hafai kushika nafasi kama hio hivyo ni bora wakati ukifika, tumuweke mtu mwingine

6. Wanawake kutopendana
Madai kuwa wanawake huwa hawapendani, yanaweza kuchangia anguko la Mama na Wanawake wengi kwa sasa ni miongoni mwa watanzania wanaomuo Mama hatoshi.

Hivyo, kwa ujumla hayo ndio mambo yanayomgharimu Mama kwa sasa na ndio yatamgharimu vibaya sana 2025 na anaweza asipate hata asilimia 30 ya kura zote.

Ukitaka kuamini haya nayosema juu ya kukubalika au kutokubalika kwa Mama, fanya tu kautafiti kasiko rasimi kwa kuhoji tu watu mbalimbali utagundua wengi wanampinga na kutorodhishwa na uongozi wake wakiwemo hata watu wa chama chake.

Hivyo, wapinzani wakijipanga vizuri 2025 na tukawa na Tume Huru, basi uwezekano wa wapinzani kushinda uchaguzi ni mkubwa mno kuanzia kwenye uraisi mpaka ubunge.
 
Attachments

  • IMG_6117.MP4
    600 KB
Badili kichwa cha habari kwanza ili uzi wako uwe na maana kwa msomaji. Mama anatekeleza miradi huko mikoani.

Nasikitika kukwambia kwamba hao wanaopata madarasa mapya hawasomi uzi kama wa kwako. Hawa wanaopata umeme huko vijijini ndani ya muda huu hawana muda wa siasa za maji taka kama hizi.

Kuna watu wanaguswa moja kwa moja maisha yao, hao hawana muda wa kusoma ulichoandika achilia mbali kuwa na muda wa kukitafsiri kwa kina.
Punguza hasira ndo unaweza ukamwelewa jamaa hicho alichokisema jamaa kina ukweli au laa.
 
Tangu nianze kufuatilia siass za nchi hii, sijawahi ona kiongozi wa CCM alie madarakani akikataliwa, kupingwa na kuongezewa vivyo sivyo kama Mama yetu wa leo.

Kwanini hali hii?

1. Mama kulinganishwa na Mwendazake

Mama kulinganishwa na Mwendazake na hapa ndipo hata baadhi ya wana-CCM wanapoungana na watanzania wengine kumuhukumu na kumuona hatoshi na wanaona ni bora 2025 watafute mgombea mwingine vinginevyo ni bora wachague mpinzani.

Kwanini Mwendazake anamgharimu?
Wakati wa Mwendazake, kuna kundi kubwa la watanzania waliamini wizi na ufisadi vilikuwa vimekomeshwa/ vimedhibitiwa jambo ambalo halikuwa kweli kwa asilimia 100.

Mwendazake alidhibiti vyombo vya habar, alidhibiti Bunge, mitandao na vyanzo vingine vya kupashana habari matokeo yske tuhuma za wizi na ufisadi Wakati wa Mwendazake havikupata nafasi.

Kingine ni Mwendazake kutumia media kuendesha propaganda za kumsifu na kumtukuza mambo ambayo sasa hayapo kwa kiwango kile na hivyo kuleta tofauti kubwa ya kimtazamo kati ya Mama na Mwendazake.

2. Kundi la Sukuma gang
Hili kundi ni kundi la watu wanaonekana kuwa na chuki dhidi ya huyu Mama na ndio wanachangia sana kuonyesha kuwa Mama hatoshi sababu tu hawampendi. Ni kama hawakuta Mama amrithi Mwendazake na hivyo kutumia madhaifu ya Mama kummaliza kisiasa mbele ya umma.

Na kama Mama angeshindwa kuendeleza miradi iliyoachwa na Mwendazake, basi hili kundi lingepata cha kusema na lingekuwa kinara katika kuwaongoza watu wamkatae Mama hiyo 2025.

Mama akijitahidi kukamilisha Miradi yote iliyoachwa na Mwendazake, basi atafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza nguvu za hili kundi mitandaoni na kwingineko

3. Madai kuwa Mzee wa Msoga ana influence katika uongozi wake
Madai haya ni moja ya mambo ambayo yanamgharimu sana Mama hasa ikizingatiwa Mzee wa Msoga anachukuliwa kama mtu alieacha rushwa na ufisadi vikatamalaki sana katika nchi hii.

Hivyo, madai kuwa Mama anafanya baahi ya mambo kwa influence ya Mzee wa Msoga, madai haya yanamgharimu sana kisiasa na 2025 atakuja kuona matokeo yake.

4. Madhaifu binafsi ya Mama
Madhaifu au mapungu haya ni pamoja na haya na kukithiri kwa tozo katika awamu yake, kauli za kuruhusu watu wale kulingana na urefu wa kamba zao, kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei, kuhamisha wamasai kule Loliondo, safari za mara kwa mara nje ya nchi, kauli zake za majukwaani na mambo mengineyo.

5. Jinsia yake
Ukweli mwingine unatokana na mila na desturi zetu plus mtazamo potofu wa jumla kwa baadhi ya watu kuwa Mwanamke hafai kushika nafasi kama hio hivyo ni bora wakati ukifika, tumuweke mtu mwingine

6. Wanawake kutopendana
Madai kuwa wanawake huwa hawapendani, yanaweza kuchangia anguko la Mama na Wanawake wengi kwa sasa ni miongoni mwa watanzania wanaomuo Mama hatoshi.

Hivyo, kwa ujumla hayo ndio mambo yanayomgharimu Mama kwa sasa na ndio yatamgharimu vibaya sana 2025 na anaweza asipate hata asilimia 30 ya kura zote.

Ukitaka kuamini haya nayosema juu ya kukubalika au kutokubalika kwa Mama, fanya tu kautafiti kasiko rasimi kwa kuhoji tu watu mbalimbali utagundua wengi wanampinga na kutorodhishwa na uongozi wake wakiwemo hata watu wa chama chake.

Hivyo, wapinzani wakijipanga vizuri 2025 na tukawa na Tume Huru, basi uwezekano wa wapinzani kushinda uchaguzi ni mkubwa mno kuanzia kwenye uraisi mpaka ubunge.
Atashinda kwa kutumia vyombo vya dola lakini ni kweli wengi wamemchoka sana
 
Labda wewe tu, lakini mh Rais Samia anakubalika na mamillion ya watanzania wanaoendelea kuhitaji utumishi wake ulionyeshaa na kuleta matumaini makubwa Sana
Atashinda kwa kutumia vyombo vya dola lakini ni kweli wengi wamemchoka sana
 
Back
Top Bottom