Rais Samia aridhia TAMISEMI kuajiri watumishi 21,200 kada ya Afya na Elimu

Rais Samia aridhia TAMISEMI kuajiri watumishi 21,200 kada ya Afya na Elimu

TAMISEMI yatangaza ajira 21000 afya na elimu 2023

======


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa Kada za Ualimu na Afya.

Idadi ya Watumishi watakaoajiriwa katika Kada za Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha katika shule za Msingi na Sekondari.

Aidha idadi ya watumishi watakaoajiriwa katika kada za Afya ni 8,070 ambao watafanya kazi katika Hospitali za Halmashauro, Vituo vya Afya na Zahanati.
Mungu tenda kitu mwaka huu nipate. Aise kitaa hakiko poa
 
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. @SuluhuSamia ameridhia kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa Kada za Ualimu na Afya.

“Idadi ya Watumishi watakaoajiriwa ktk Kada za Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha ktk shule za Msingi na Sekondari. Aidha idadi ya watumishi watakaoajiriwa kada za Afya ni 8,070 ambao watafanya kazi katika Hospitali za Halmashauro, Vituo vya Afya na Zahanati”

Angela Kairuki
TAMISEMI
 
Serikali yatakiwa ijitafakari hili swala la kuajiri watu 21,000 kwa mwaka na wanaohitimu ni zaidi ya 100,000 kwa vyuo vikuu na vya kati, hili swala litaleta shida

Serikali itafute vyanzo vya mapato vipya ili waajiri Walimu, Afya, Kodi

Mf kwa Mwaka huu Darasa la Kwanza ni zaidi ya 1.2mil ila walimu ni wale wale
Fani zote ni laki moja sawa ila hii ni afya na ualimu tu
 
Hapa ndio utaamini uchawi upoo, kuanzia leoo utaona

Access denied...
404 forbidden...
No network.....
Please wait....
Network error....

Mara cheti ukikitafta kwenye documents hukioni nakati kila siku ulikua unapitana nacho...
Simu kuisha charge haraka, umeme kukata...
 
Back
Top Bottom