Rais Samia aridhia TAMISEMI kuajiri watumishi 21,200 kada ya Afya na Elimu

Rais Samia aridhia TAMISEMI kuajiri watumishi 21,200 kada ya Afya na Elimu

Naombeni ushauri wenu wadau au kama Kuna member mwenye tatzo kama langu anisaidie mawazo. Mimi nimehitimu Diploma in secondary education mwaka 2015, nilikua nikisoma masomo ya Sanaa yaani Historia Kiswahili na English.

Nimekua nikiomba kazi Kila serikali ilipotoa tangazo la kazi lakin sijawahi kupata, mbaya zaidi kipengele Cha diploma in secondary education hakimo kwenye mfumo wa maombi japo nimekuwa nkijishusha kuomba ngazi ya primary.

Sasa sijui tatizo ni gani wakati Nina ufaulu mzuri wa GPA ya 3.8 na Nina uwezo mkubwa wa kufundisha secondary.

Naomba kama Mh rais alivyosema kuwa anapitia humu ajaribu kutuonea huruma sisi wahitimu wa 2015 tupewe kipaumbele.
 
Kozi za masikini ni
•Afya
•Elimu
•Kilimo
• uvuvi
Hizi utaendeleza umasikini ukooni kwenu

Kozi za wato masikini wenye ndoto za kupata unafuu wa maisha ni
•Mechanical engineering (fani yangu)
•Electrical engineering
•ICT
Kama hao waalimu na madaktari wangekua hawapo usingesoma hiyo mechanical engineering yako

Kuwa na heshima na kada za watu
 
Serikali yatakiwa ijitafakari hili swala la kuajiri watu 21,000 kwa mwaka na wanaohitimu ni zaidi ya 100,000 kwa vyuo vikuu na vya kati, hili swala litaleta shida...
Tanzania imeshakuwa donor country, nahis hilo litawezekana
 
Kuna binti sikumbuki jina lake alipost humu uzi kakata tamaa ana shahada ya madawa sijui kitu gani.

Alienda mpaka kozi akiwa anajua kaishaula, kisha wakapimwa mara ya pili akaambiwa hayupo fiti, biashara zote alikuwa kafunga.

Kama kuna mtu anamkumbuka amtag tafadhali.
 
Et atakufa shoga.ni kwel nakumbuka enzi za JK alikuwa anajiri walimu elf 30.saiv elf 21 walimu na afya..
Msisahau kipindi kile shule za kata ndo zimefunguliwa na zahanati za kata hakukuwepo walimu ko walikua wanaajiriwa wote ila sa hivi haiwezi kua hivyo ,mbona kada nyingine tofauti na ualimu na udaktari hawajawahi ajiri kwa style kama hiyo?

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
TAMISEMI yatangaza ajira 21000 afya na elimu 2023

======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa Kada za Ualimu na Afya...
Nyingine zinakuja.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema katika mwaka 2023 Serikali imepanga kuajiri Wataalamu wa afya 12,000 ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha huduma kwa Wananchi hasa maeneo yenye upungufu wa Watumishi na kupunguza changamoto ya ajira kwa Wataalamu wa afya nchini.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Aprili 12, 2023 Bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu, Minza Simon Mjika katika Mkutano wa 11 kikao cha tano ambapo amesema Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na TAMISEMI kuhakikisha Mwananchi anapata huduma bora, kwa kuhakikisha maeneo yote yenye uhitaji hasa katika visiwa kunakuwa na zahanati katika kila kijiji na Wataalamu wa afya ili kupunguza kufuata huduma za afya kwa umbali mrefu.

Ajira hizi 12,000 zinahusisha Watumishi wa hadi Hospitali za Mikoa, Kanda na Rufaa ambazo zinasimamiwa na Wizara ya Afya na ni tofauti na ajira 21,200 ambazo Rais, Dkt. Samia kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI amezitoa leo katika Kada ya Elimu na Afya ikiwemo Watumishi 13,130 watakaofundisha katika Shule za Msingi na Sekondari na Kada ya Afya ni Watumishi 8070 watakaofanyakazi katika Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati, zinazosimamiwa na TAMISEMI.
 
Kuna binti sikumbuki jina lake alipost humu uzi kakata tamaa ana shahada ya madawa sijui kitu gani.

Alienda mpaka kozi akiwa anajua kaishaula, kisha wakapimwa mara ya pili akaambiwa hayupo fiti, biashara zote alikuwa kafunga.

Kama kuna mtu anamkumbuka amtag tafadhali.
Yeah aisee niliuona ule uzi
Ilikuwa ni Lab nafikiri.
Aidama
 
Ili kukabiliana na tatizo la ajira, serikali yapaswa ajiri angalau watu 50,000 kila mwaka.

Na ibadilishe mfumo wa ajira kutoka kuwa wa kudumu hadi wa mkataba maana kuna watu wanaridhika sana
Tatizo ni sheria za kimataifa mzee sio kwamba serikali inajisikia tuu na mfumo huo ukija kwenye serikali basi iwe na hela kweli kweli maana baada ya kumaliza mkataba unapata kipute chako kama mbunge vile.
 
Kozi za masikini ni
•Afya
•Elimu
•Kilimo
• uvuvi
Hizi utaendeleza umasikini ukooni kwenu

Kozi za wato masikini wenye ndoto za kupata unafuu wa maisha ni
•Mechanical engineering (fani yangu)
•Electrical engineering
•ICT
Natamani kukutukana ila acha nkae kimya😂
 
Hivi wanangu haya maisha na hizi ajira watu watakuja kutoboa kweli au ndo ile kupata basic needs tu maan dah napigaga hesabu naonaga mmmh mbona hatari
 
Back
Top Bottom