Rais Samia aruhusu vyama vya siasa kufanya Mikutano ya hadhara

Rais Samia aruhusu vyama vya siasa kufanya Mikutano ya hadhara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa Nchini, leo Jumanne Januari 3, 2023.

Mazungumzo haya yanafanyika Ikulu, Magogoni - Dar es Salaam.



VIONGOZI WAWASILI
Viongozi mbalimbali wa vyama wameshawasili ukumbini, wakiwemo Freeman Mbowe na John Mnyika (CHADEMA), Zitto Kabwe (ACT Wazalendo), Abdulrahman Kinana na Daniel Chongolo (CCM), Profesa Lipumba (CUF), Hashim Rungwe (CHAUMMA), John Cheyo (UDP), Joseph Selasini (NCCR Mageuzi).

KUMBUKUMBU KIKAO KILICHOPITA
Kumbuka kuwa Rais Samia alishakutana na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa Dodoma, Desemba 2021 katika mkutano wa vyama na wadau wa siasa lakini vyama vya CHADEMA na NCCR-Mageuzi viliususia.

MAZUNGUMZO BAADA YA KUKUTANA NA MBOWE
Mazungumzo haya yanafanyika zikiwa zimepita siku mbili baada ya Rais Samia kuzungumza na Mbowe, mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, ikiwa ni wakati huohuo Rais Samia alipokuwa akipokea taarifa ya maridhiano baina ya CCM na CHADEMA yaliyodumu kwa miezi 8.

MAKAMU WA RAIS, WAZIRI MKUU WAINGIA UKUMBINI
Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wamewasili ukumbini, na sasa anasubiriwa Rais.

RAIS AMEINGIA UKUMBINI
Rais Samia Suluhu Hassan ameingia ukumbini na shughuli imeanza.

Msajili wa Vyama vya Siasa: Jaji Francis S. Mutungi
Nawapongeza viongozi wote wa vyama vya 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu vilivyoitikia wito japo ilikuwa ni ndani ya muda mfupi. Kitendo hiki ni dalili nzuri,

Hili ni jambo zuri, Wananchi wanataka kusikiliza Rais atazungumza na nini na hata mataifa ya nje yanataka kusikiliza atakachozungumza Rais.

RAIS SAMIA ANAZUNGUMZA
Nimeitisha kikao hiki kuna mambo tulizungumza na tumekubaliana, yanahitaji maamuzi

Wakati mnanikabidhi madaraka, busara ilinituma kuwa kuna haja ya kufanya taifa kuwa kitu kimoja, wote tuzungumze lugha moja.

Ili Taifa liwe moja lazima tuwe na maridhiano, vyama vya siasa tunawawakilisha Watanzania, ndio maana nikaamua tuwe na mazungumzo ndani ya vyama. Tukaunda kikosi kazi, vyama vikafanya kazi nzuri, tukaletewa mapendekezo lakini kuna chama kikakataa kushiriki

Baada ya chama kimoja kukataa maridhiano, nikapeta maneno mengi kuwa nisiwasikilize, nikamwambia makamu wangu azungumze nao, wamezungumza mengi, wamefanya mikutano sita au saba, mikutano ya awali ilikuwa ngumu lakini sasa mambo ni mazuri na tunakwenda pamoja.

Leo chadema wapo hapa, ndio faida ya kuzungumza. Watu wazima huko nyuma walisema, kwenye mazungumzo hakukosekani amani. Sasa hiyo ni R ya kwanza ya reconcilliation, mazungumzo bado yanaendelea.

Sasa kwa misingi hii tunayokubaliana tukasema tukae kama Taifa ni R ya pili inafanya kazi. Ni imani yangu vyama vya siasa tutaendelea kukaa.

R ya tatu ni mabadiliko, Reform kwenye nchi yetu, yaonekane mabadiliko kwenye nchi yetu, ambayo tutafanya kwa kuzingatia katiba yetu, sheria zetu, mila na desturi zetu, kwa kuzingatia matamko ya Kimataifa, kwa kuzingatia uwezo wetu kiuchumi.

Na mwisho kabisa tutajenga taifa letu, taifa lisimame, watanzania wenye kuamini nchi yao, wenye kusimama kwa nchi yao popote duniani. Huko ndipo mwenyezi Mungu amenielekeza tuelekee.

Bahati nzuri dhana hii imepata baraka zote za chama changu.

Tuliunda kikosi kazi lakini tulikuwa na mazungumzo na chama kingine pembeni, Serikali inatakiwa kutenda haki kwa watu wote bila kuacha mila na desturi zetu za kitanzania.

Kuna mapendekezo yaliletwa, kubwa kabisa ni mikutano ya hadhara pamoja na mabadiliko ya sheria kadhaa. Mabadiliko ya sheria mbalimbali tunafanyia kazi Serikalini, tunataka kujenga kwa pamoja hivyo tutawaita.

Suala lingine ni marekebisho ya katiba. Haya matatu ndio yamechukua nafasi kubwa. Kikosi kazi kimefanya kazi nchi nzima, lakini tukasema kuna mambo maalumu kwa wenzetu Zanzibar, tuliunda kikosi kazi kidogo kwa ajili ya mambo yao na wamepeleka ripoti kwa Rais.

Mikutano ya Hadhara ni Haki ya Vyama vya Siasa. Nimekuja kutoa ruhusa; nimetengua zuio la Mikutano ya Vyama vya Siasa. Ni haki kwa Vyama vya Siasa kuendesha mikutano yao ya hadhara lakini kuna Wajibu wa kila mmoja na upande wa Serikali ni kulinda mikutano ifanyike kwa usalama.

Ni wajibu wenu kufuata Kanuni na Sheria, fanyeni Siasa za Kistaarabu, Kiungwana na za Kupevuka. Nitakaa na vyombo vyangu vya ulinzi, kazi yetu ni kuwalinda.

Tupo tayari kuukwamua mchakato wa KATIBA, kuna mapendekezo mengi yanatolewa, kuna mambo mengi yamebadilika, kuna haja ya kuendana na hali halisi ya sasa hivi.

Inawezekana michakato yote miwili ya kawatiba ikawa imepitwa na muda lakini tunaweza kuchukua kutoka kwenye zote mbili

Katiba ni ya Watanzania siyo ya vyama vya siasa. Nataka kuwapa faraja kwamba mda si mrefu tutaanza, Katiba hii siyo ya vyama vya siasa, ni ya Watanzania.

Kamati itakayoundwa kwa ajili ya Katiba itaundwa na watu wa aina mbalimbali, itafanya kazi zake kwa maelekezo tutakayowapa, tutawapangia vizuri lakini siyo ile ya vuguvugu.

Mchakato ukiwa unaendelea Nchi iwe imetulia na shughuli nyigine zinaendelea.

Leo hii nimeona tuitane kupeana haya mambo matatu.
HONGERA SANA RAIS SAMIA HAKIKA HOFU YA MUNGU IMEKUTAWALA NA MUNGU AZIDI KUKUBARIKI SANA
 
Kama sio uadui kwanini watu wanapigwa risasi wengine wanatekwa na kupotezwa... fahamu siasa zetu ni vita kwasababu watu hawataki kutoka kwenye mamlaka kwa maslai yao.

Kuna kipindi CHADEMA walipigwa kote kote sio mahakamani, sio bungeni sio serikalini. Na hakuna msaada waliopata, walikuwa Kama yatima. Huku Lissu analimwa Risasi, huku Mbowe anavunjiwa bilcanas, huku akina Halima wanafukuzwa bungeni, huku Saanane anapotezwa. Nani aliwasaidia?.

So CHADEMA wameamua kukaa na maadui zao ili kukomesha hayo yasijirudie Tena, ndio maana wanarekebisha sheria za mikutano ya hadhara ili wapinzani wasiminywe Sana.
 
HUYU MAMA YETU HUYU... YAANI WATU HAWANA HATA HABARI NAE YANI... TANGAZO LINALOMHUSU HATA HALISISIMUI... ZAIDI YA KUZIDI KUTIA HASIRA TU...

KWA SABABU HATA UKISEMA UKAMSIKILIZE ATASEMA NINI... HAKUNA LA MAANA.

Ila Leo kwa Mara ya pili ninamsikiliza baada ya CHADEMA kuhudhuria mkutano wake.
 
Mbowe kwa sasa anaeleweka sana, kaonyesha ukomavu wa kisiasa ila tatizo bado genge lililo mzunguka hawataki kubadilika!!! wanadhani siasa ni uadui!
wanadhani siasa ni ukorofi na kupwayuka!!

Mbowe anao wajibu wa kuwaelimisha walio mzunguka.

wanasiasa hawapaswi kulazimisha mambo wanayo yataka wao bali wanapswa wakubali pia hoja za chama kinacho tawla.
Ndugu yetu mmoja anaitwa MMM anashida twitter Huko kazi yake ni kubisha Tu
 
Hapo Samia kakosea. chadema sio watu wa kuwachekea chekea hata kidogo. Amani ya hii nchi itatoweka hao wehu wakiruhusiwa kukimbizana barabarani.
 
Hamna kitu humo... Washalamba asali hao.

Ulitaka wafanyeje mkuu?. CHADEMA waliitisha UKUTA watu wakawadhiaki, leo mnawaita walamba asali kweli?. Viongozi wao wamepitia mangapi?. Kukaa rumande miezi Saba kwa kosa la Ugaidi kwako ni dogo?. Kupingwa risasi kwako ni kitu kidogo?. Please tuwe realistic kwa CHADEMA
 
Mbowe kwa sasa anaeleweka sana, kaonyesha ukomavu wa kisiasa ila tatizo bado genge lililo mzunguka hawataki kubadilika!!! wanadhani siasa ni uadui!
wanadhani siasa ni ukorofi na kupwayuka!!

Mbowe anao wajibu wa kuwaelimisha walio mzunguka.

wanasiasa hawapaswi kulazimisha mambo wanayo yataka wao bali wanapswa wakubali pia hoja za chama kinacho tawla.
Kumbuka siasa za uadui kuuwana kutekana zimeasisiwa na ccm ya John Joseph Pombe Magufuli anachofanya mama ni kuponya majeraha na kutumia hekima na busara ku suppress vuguvugu la mabadiliko.
 
Upumbavu tu,anaacha kukutana na makundi maalumu katika jamii kama walemavu na wazee..anaenda kukutana na hao mchwa wenzie.

Tuwe watu washukrani hata kwa dogo. Leo kakutana na vyama kesho atakutana na walemavu.
 
Rais Samia katika eneo analofanya vizuri sana sana ni jinsi anavyo handle wanasiasa. Hili ni eneo ambalo JPM lilimshinda, aliamini kwenye matumizi ya nguvu hata maeneo yanayohitaji akili ndogo tu.

Hata jinsi alivyocheza kwenye uchaguzi wa juzi wa CCM amehakikisha kila kundi linajisikia kushinda. Hii initiatives regardless ya uwezekano wa delaying tactics lakini anazicheza kwa akili kubwa sana.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Lkn wewe ni kati ya watu waliokuwa wanasifia kila jambo alilofanya Jiwe
 
Back
Top Bottom