Rais Samia aruhusu vyama vya siasa kufanya Mikutano ya hadhara

Tusubirie conclusion. Unaambiwa mikutano ya maridhiano ilikuwa migumu, Sasa sijui asali ililambwaje kwenye mazingira. All in all CHADEMA wamaejitahidi kiasi chao kujishusha ili mambo mengine yaendelee.
Hakika umenena neno la kujenga
 
Samia ana akili sana kwenye eneo hilo la kuwachezea wapinzani
 
Duh! We jamaa umeandika maneno matakatifu, nakuombea Mungu akupe nafasi ya juu kabisa, tusaidiane kuijenga nchi yetu kwa njia ya amani.

Amani ni moja ya tunu tulizoachiwa na wazee wetu! Omukama akubele
 
Hapo Samia kakosea. chadema sio watu wa kuwachekea chekea hata kidogo. Amani ya hii nchi itatoweka hao wehu wakiruhusiwa kukimbizana barabarani.

Amani Tanzania haiwezi kutoweka. Tanzania ni nchi ya amani miak nenda rudi
 
Kuhusu ruhusa ya mikutano ya siasa vile vyama shikizi vitakuwa vimenuna. Vitapata wapi watu wa kuhudhuria? Labda maeneo ya sokoni na stendi tu.
 
Rais wetu Mama Dokta Samia hana nongwa kabisaa ila wanasiasa wa upinzani ndio hawaishi nongwa.

Tunavitaka vyama vya upinzani viuze sera kwetu sio vurugu na chuki.

Nchi hii ni yetu hivyo tubishane kwa nia ya kujenga sio kubomoa.
 
Hiki Cha kupewa kwenye kisahani hakinogi, mtaani hakina mzuka.

Ni kama ulivyo Uhuru wa Tanganyika, taste yake ni tofauti na uoe wa kenya

Ulitaka wapate kwa kumwaga damu?. Kwa Tanzania Hilo haliwezekani. Watanzania ni watu wa amani watamaliza tofauti zao kwa amani, shida ni CCM tu.
 
Ulitaka wapate kwa kumwaga damu?. Kwa Tanzania Hilo haliwezekani. Watanzania ni watu wa amani watamaliza tofauti zao kwa amani, shida ni CCM tu.
Namaanisha CCM ni wataalamu wa ku-manage changes, wanaonekana kuitoa ruhusa kwa ridhaa yao, sio shinikizo la wapinzania, wapinzani wamebweka weeee, hawakufanikiwa
 
Rais wetu Mama Dokta Samia hana nongwa kabisaa ila wanasiasa wa upinzani ndio hawaishi nongwa.

Tunavitaka vyama vya upinzani viuze sera kwetu sio vurugu na chuki.

Nchi hii ni yetu hivyo tubishane kwa nia ya kujenga sio kubomoa.

Acha uongo. Mbaya anajulikana ni CCM . Ndio chanzo Cha yote haya. Wangekubali katiba mpya kipindi kile Leo nchi ingekuwa mbali. Tatizo la hii nchi ni ccm fullstop.
 
Namaanisha CCM ni wataalamu wa ku-manage changes, wanaonekana kuitoa ruhusa kwa ridhaa yao, sio shinikizo la wapinzania, wapinzani wamebweka weeee, hawakufanikiwa

Unajua unachoongea?. Haya ni matunda ya harakati za CHADEMA. Mama alikutana na Lissu pia akakutana na Mbowe unajua waliongea Nini? CHADEMA wapewe heshima yao wamepambana Sana mpka leo tumefikia hapa.

Tuwape CHADEMA heshima yao bwana. Akina Zitto walisema wanataka katiba mpya baada ya 2025 au umesahau?. Ni CHADEMA pekee yao walisimamia ajenda ya katiba mpya.
 
Kwahiyo unakiri mlifanya upumbavu kwenda Dom..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…