Rais Samia aruhusu vyama vya siasa kufanya Mikutano ya hadhara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa Nchini, leo Jumanne Januari 3, 2023.

Mazungumzo haya yanafanyika Ikulu, Magogoni - Dar es Salaam.

VIONGOZI WAWASILI
Viongozi mbalimbali wa vyama wameshawasili ukumbini, wakiwemo Freeman Mbowe na John Mnyika (CHADEMA), Zitto Kabwe (ACT Wazalendo), Abdulrahman Kinana na Daniel Chongolo (CCM), Profesa Lipumba (CUF), Hashim Rungwe (CHAUMMA), John Cheyo (UDP), Joseph Selasini (NCCR Mageuzi).

KUMBUKUMBU KIKAO KILICHOPITA
Kumbuka kuwa Rais Samia alishakutana na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa Dodoma, Desemba 2021 katika mkutano wa vyama na wadau wa siasa lakini vyama vya CHADEMA na NCCR-Mageuzi viliususia.

MAZUNGUMZO BAADA YA KUKUTANA NA MBOWE
Mazungumzo haya yanafanyika zikiwa zimepita siku mbili baada ya Rais Samia kuzungumza na Mbowe, mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, ikiwa ni wakati huohuo Rais Samia alipokuwa akipokea taarifa ya maridhiano baina ya CCM na CHADEMA yaliyodumu kwa miezi 8.

MAKAMU WA RAIS, WAZIRI MKUU WAINGIA UKUMBINI
Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wamewasili ukumbini, na sasa anasubiriwa Rais.

RAIS AMEINGIA UKUMBINI
Rais Samia Suluhu Hassan ameingia ukumbini na shughuli imeanza.

Msajili wa Vyama vya Siasa: Jaji Francis S. Mutungi
Nawapongeza viongozi wote wa vyama vya 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu vilivyoitikia wito japo ilikuwa ni ndani ya muda mfupi. Kitendo hiki ni dalili nzuri,

Hili ni jambo zuri, Wananchi wanataka kusikiliza Rais atazungumza na nini na hata mataifa ya nje yanataka kusikiliza atakachozungumza Rais.

RAIS SAMIA ANAZUNGUMZA
Nimeitisha kikao hiki kuna mambo tulizungumza na tumekubaliana, yanahitaji maamuzi

Wakati mnanikabidhi madaraka, busara ilinituma kuwa kuna haja ya kufanya taifa kuwa kitu kimoja, wote tuzungumze lugha moja.

Ili Taifa liwe moja lazima tuwe na maridhiano, vyama vya siasa tunawawakilisha Watanzania, ndio maana nikaamua tuwe na mazungumzo ndani ya vyama. Tukaunda kikosi kazi, vyama vikafanya kazi nzuri, tukaletewa mapendekezo lakini kuna chama kikakataa kushiriki

Baada ya chama kimoja kukataa maridhiano, nikapeta maneno mengi kuwa nisiwasikilize, nikamwambia makamu wangu azungumze nao, wamezungumza mengi, wamefanya mikutano sita au saba, mikutano ya awali ilikuwa ngumu lakini sasa mambo ni mazuri na tunakwenda pamoja.

Leo chadema wapo hapa, ndio faida ya kuzungumza. Watu wazima huko nyuma walisema, kwenye mazungumzo hakukosekani amani. Sasa hiyo ni R ya kwanza ya reconcilliation, mazungumzo bado yanaendelea.

Sasa kwa misingi hii tunayokubaliana tukasema tukae kama Taifa ni R ya pili inafanya kazi. Ni imani yangu vyama vya siasa tutaendelea kukaa.

R ya tatu ni mabadiliko, Reform kwenye nchi yetu, yaonekane mabadiliko kwenye nchi yetu, ambayo tutafanya kwa kuzingatia katiba yetu, sheria zetu, mila na desturi zetu, kwa kuzingatia matamko ya Kimataifa, kwa kuzingatia uwezo wetu kiuchumi.

Na mwisho kabisa tutajenga taifa letu, taifa lisimame, watanzania wenye kuamini nchi yao, wenye kusimama kwa nchi yao popote duniani. Huko ndipo mwenyezi Mungu amenielekeza tuelekee.

Bahati nzuri dhana hii imepata baraka zote za chama changu.

Tuliunda kikosi kazi lakini tulikuwa na mazungumzo na chama kingine pembeni, Serikali inatakiwa kutenda haki kwa watu wote bila kuacha mila na desturi zetu za kitanzania.

Kuna mapendekezo yaliletwa, kubwa kabisa ni mikutano ya hadhara pamoja na mabadiliko ya sheria kadhaa. Mabadiliko ya sheria mbalimbali tunafanyia kazi Serikalini, tunataka kujenga kwa pamoja hivyo tutawaita.

Suala lingine ni marekebisho ya katiba. Haya matatu ndio yamechukua nafasi kubwa. Kikosi kazi kimefanya kazi nchi nzima, lakini tukasema kuna mambo maalumu kwa wenzetu Zanzibar, tuliunda kikosi kazi kidogo kwa ajili ya mambo yao na wamepeleka ripoti kwa Rais.

Mikutano ya Hadhara ni Haki ya Vyama vya Siasa. Nimekuja kutoa ruhusa; nimetengua zuio la Mikutano ya Vyama vya Siasa. Ni haki kwa Vyama vya Siasa kuendesha mikutano yao ya hadhara lakini kuna Wajibu wa kila mmoja na upande wa Serikali ni kulinda mikutano ifanyike kwa usalama.

Ni wajibu wenu kufuata Kanuni na Sheria, fanyeni Siasa za Kistaarabu, Kiungwana na za Kupevuka. Nitakaa na vyombo vyangu vya ulinzi, kazi yetu ni kuwalinda.

Tupo tayari kuukwamua mchakato wa KATIBA, kuna mapendekezo mengi yanatolewa, kuna mambo mengi yamebadilika, kuna haja ya kuendana na hali halisi ya sasa hivi.

Inawezekana michakato yote miwili ya kawatiba ikawa imepitwa na muda lakini tunaweza kuchukua kutoka kwenye zote mbili

Katiba ni ya Watanzania siyo ya vyama vya siasa. Nataka kuwapa faraja kwamba mda si mrefu tutaanza, Katiba hii siyo ya vyama vya siasa, ni ya Watanzania.

Kamati itakayoundwa kwa ajili ya Katiba itaundwa na watu wa aina mbalimbali, itafanya kazi zake kwa maelekezo tutakayowapa, tutawapangia vizuri lakini siyo ile ya vuguvugu.

Mchakato ukiwa unaendelea Nchi iwe imetulia na shughuli nyigine zinaendelea.

Leo hii nimeona tuitane kupeana haya mambo matatu.

Mh rais samia utakubwa daima na utaacha alama muhimu ktk taifa letu kama utatupatia katiba mpya ya jaji Warioba
 
"Rasimu ya warioba irudi mezani SASA ijadiliwe iwe Katiba Mpya"

Marekebisho ya katiba Bado nakiona ni kichaka cha kujifichia na kuogopa kuwajibika KWA wananchi!!!

Mungu amsaidie mh.Rais akubaliane na ukweli kuwa katiba mpya ndicho kinacho hitajika sio marekebisho ya hii iliyopo!

Mkiipaka Rangi hii iliyopo akija Mwingine asiye na kifua ataitumia tena kuwaumiza wananchi KWASABABU ya uhuru wao wa kutoa maoni!

MWANACCM Huru nimeandika Ili ajaye asiharibu utaifa wetu tulioujenga KWA Miaka mingi!

Mungu ibariki Tanzania nchi yetu niipendayo Sana!
 
Matawi ya vyama vya upinzani yalikufa, ni wakati wa kuyafufua sasa. Ni wakati sasa wa vyama vya upinzani kuja na hoja maridhawa ya kuwaambia watanzania wakiwapa ridhaa ya kuongoza dola watafanya nini kipya kwa maendeleo ya taifa
 
Unatoaje ruhusa kwenye kitu ambacho ni haki ya kikatiba?

Yani raisi aje akwambie "nakupa ruhusa ya kuishi". Yeye kapata wapi haki ya kutoa ruhusa hiyo?

Hiyo nguvu ya kuruhusu anaipata wapi? Au ndiyo ubabe tu?
 
TRA aliambiwa hivyo hivyo acha kama ilivyokuta, akaja na akili zake; sasa hivi u-turn.

Huku nako ni swala la muda tu ataelewa kwanini mikutano ya hadhara ilizuiawa, ila U-turn itakuwa ngumu sana.

Huko kwenye katiba kila tukio CDM wanakwambia tutarekebisha na katiba mpya. Tukio la mwisho la Diamond, solution yao katiba mpya. Sasa TRA na katiba mpya wapi wapi wakati aina ya kodi wanazotoza chanzo ni budget, namna watakavyofanya kazi na kwenyewe parliament act.

Asubiri hayo maoni ya kipuuzi ambayo either hayatekelezi au demands za changes to administration workings ambazo ni impractical ndio ataelewa kwanini katiba mpya ilifeli kama akuelewa alipokuwa naibu speaker wa bunge la katiba, ataelewa sasa.

Mikutano ya hadhara salalee hayo mambo yalikuwa ignored for reasons na watangulizi wake uongo kila kukicha ambao unachanganya raia, badala ya kuendesha nchi unajikuta una kazi ya kujibu upotoshaji.

Ngoja ajionee na yeye ataelewa soon kwanini watu walichukua hayo maamuzi.

Si anataka cheap politics ngoja aone kinachofuata, na U-turn sio rahisi maana atapewa kila jina la kishetani akithibutu.

Mbona marekani siasa kila siku Tena wenyewe wa uchaguzi Mara mbili ndani ya awamu moja, na wanamaendeleo?. Kwa hivyo tubaki na CCM pekee yake?

Mnazuia watu kufanya mikutano ikifika uchaguzi mnaiba kura. Si bora mfute hiyo mfumo wa siasa wa vyama vingi?.
 
Hawastahili heshima yoyote, CCM ndio imeamua, mlishaufyata nyie

Ummemsikia Samiah akisema kuwa majadialianao yalikuwa magumu?. Mara sita wamekaa, na kina Wana CCM walikuwa hawataki mikutano iruhusiwe.

Nikuulize aliyeufyata ni Nani? Aliyezuia kufanya mikutano au aliyeruhusiwa kufanya mikutano
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa Nchini, leo Jumanne Januari 3, 2023.

Mazungumzo haya yanafanyika Ikulu, Magogoni - Dar es Salaam.

VIONGOZI WAWASILI
Viongozi mbalimbali wa vyama wameshawasili ukumbini, wakiwemo Freeman Mbowe na John Mnyika (CHADEMA), Zitto Kabwe (ACT Wazalendo), Abdulrahman Kinana na Daniel Chongolo (CCM), Profesa Lipumba (CUF), Hashim Rungwe (CHAUMMA), John Cheyo (UDP), Joseph Selasini (NCCR Mageuzi).

KUMBUKUMBU KIKAO KILICHOPITA
Kumbuka kuwa Rais Samia alishakutana na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa Dodoma, Desemba 2021 katika mkutano wa vyama na wadau wa siasa lakini vyama vya CHADEMA na NCCR-Mageuzi viliususia.

MAZUNGUMZO BAADA YA KUKUTANA NA MBOWE
Mazungumzo haya yanafanyika zikiwa zimepita siku mbili baada ya Rais Samia kuzungumza na Mbowe, mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, ikiwa ni wakati huohuo Rais Samia alipokuwa akipokea taarifa ya maridhiano baina ya CCM na CHADEMA yaliyodumu kwa miezi 8.

MAKAMU WA RAIS, WAZIRI MKUU WAINGIA UKUMBINI
Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wamewasili ukumbini, na sasa anasubiriwa Rais.

RAIS AMEINGIA UKUMBINI
Rais Samia Suluhu Hassan ameingia ukumbini na shughuli imeanza.

Msajili wa Vyama vya Siasa: Jaji Francis S. Mutungi
Nawapongeza viongozi wote wa vyama vya 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu vilivyoitikia wito japo ilikuwa ni ndani ya muda mfupi. Kitendo hiki ni dalili nzuri,

Hili ni jambo zuri, Wananchi wanataka kusikiliza Rais atazungumza na nini na hata mataifa ya nje yanataka kusikiliza atakachozungumza Rais.

RAIS SAMIA ANAZUNGUMZA
Nimeitisha kikao hiki kuna mambo tulizungumza na tumekubaliana, yanahitaji maamuzi

Wakati mnanikabidhi madaraka, busara ilinituma kuwa kuna haja ya kufanya taifa kuwa kitu kimoja, wote tuzungumze lugha moja.

Ili Taifa liwe moja lazima tuwe na maridhiano, vyama vya siasa tunawawakilisha Watanzania, ndio maana nikaamua tuwe na mazungumzo ndani ya vyama. Tukaunda kikosi kazi, vyama vikafanya kazi nzuri, tukaletewa mapendekezo lakini kuna chama kikakataa kushiriki

Baada ya chama kimoja kukataa maridhiano, nikapeta maneno mengi kuwa nisiwasikilize, nikamwambia makamu wangu azungumze nao, wamezungumza mengi, wamefanya mikutano sita au saba, mikutano ya awali ilikuwa ngumu lakini sasa mambo ni mazuri na tunakwenda pamoja.

Leo chadema wapo hapa, ndio faida ya kuzungumza. Watu wazima huko nyuma walisema, kwenye mazungumzo hakukosekani amani. Sasa hiyo ni R ya kwanza ya reconcilliation, mazungumzo bado yanaendelea.

Sasa kwa misingi hii tunayokubaliana tukasema tukae kama Taifa ni R ya pili inafanya kazi. Ni imani yangu vyama vya siasa tutaendelea kukaa.

R ya tatu ni mabadiliko, Reform kwenye nchi yetu, yaonekane mabadiliko kwenye nchi yetu, ambayo tutafanya kwa kuzingatia katiba yetu, sheria zetu, mila na desturi zetu, kwa kuzingatia matamko ya Kimataifa, kwa kuzingatia uwezo wetu kiuchumi.

Na mwisho kabisa tutajenga taifa letu, taifa lisimame, watanzania wenye kuamini nchi yao, wenye kusimama kwa nchi yao popote duniani. Huko ndipo mwenyezi Mungu amenielekeza tuelekee.

Bahati nzuri dhana hii imepata baraka zote za chama changu.

Tuliunda kikosi kazi lakini tulikuwa na mazungumzo na chama kingine pembeni, Serikali inatakiwa kutenda haki kwa watu wote bila kuacha mila na desturi zetu za kitanzania.

Kuna mapendekezo yaliletwa, kubwa kabisa ni mikutano ya hadhara pamoja na mabadiliko ya sheria kadhaa. Mabadiliko ya sheria mbalimbali tunafanyia kazi Serikalini, tunataka kujenga kwa pamoja hivyo tutawaita.

Suala lingine ni marekebisho ya katiba. Haya matatu ndio yamechukua nafasi kubwa. Kikosi kazi kimefanya kazi nchi nzima, lakini tukasema kuna mambo maalumu kwa wenzetu Zanzibar, tuliunda kikosi kazi kidogo kwa ajili ya mambo yao na wamepeleka ripoti kwa Rais.

Mikutano ya Hadhara ni Haki ya Vyama vya Siasa. Nimekuja kutoa ruhusa; nimetengua zuio la Mikutano ya Vyama vya Siasa. Ni haki kwa Vyama vya Siasa kuendesha mikutano yao ya hadhara lakini kuna Wajibu wa kila mmoja na upande wa Serikali ni kulinda mikutano ifanyike kwa usalama.

Ni wajibu wenu kufuata Kanuni na Sheria, fanyeni Siasa za Kistaarabu, Kiungwana na za Kupevuka. Nitakaa na vyombo vyangu vya ulinzi, kazi yetu ni kuwalinda.

Tupo tayari kuukwamua mchakato wa KATIBA, kuna mapendekezo mengi yanatolewa, kuna mambo mengi yamebadilika, kuna haja ya kuendana na hali halisi ya sasa hivi.

Inawezekana michakato yote miwili ya kawatiba ikawa imepitwa na muda lakini tunaweza kuchukua kutoka kwenye zote mbili

Katiba ni ya Watanzania siyo ya vyama vya siasa. Nataka kuwapa faraja kwamba mda si mrefu tutaanza, Katiba hii siyo ya vyama vya siasa, ni ya Watanzania.

Kamati itakayoundwa kwa ajili ya Katiba itaundwa na watu wa aina mbalimbali, itafanya kazi zake kwa maelekezo tutakayowapa, tutawapangia vizuri lakini siyo ile ya vuguvugu.

Mchakato ukiwa unaendelea Nchi iwe imetulia na shughuli nyigine zinaendelea.

Leo hii nimeona tuitane kupeana haya mambo matatu.

Long live my President.
Hakika una_restore hope mioyoni mwetu.

Hakika MUNGU alikuwa na kusudi lake Ile tarehe 17 March 2021.
 
Back
Top Bottom