Rais Samia aruhusu vyama vya siasa kufanya Mikutano ya hadhara

Rais Samia aruhusu vyama vya siasa kufanya Mikutano ya hadhara

Mbowe kwa sasa anaeleweka sana, kaonyesha ukomavu wa kisiasa ila tatizo bado genge lililo mzunguka hawataki kubadilika!!! wanadhani siasa ni uadui!
wanadhani siasa ni ukorofi na kupwayuka!!

Mbowe anao wajibu wa kuwaelimisha walio mzunguka.

wanasiasa hawapaswi kulazimisha mambo wanayo yataka wao bali wanapswa wakubali pia hoja za chama kinacho tawla.
Mbowe ni mwema sana kuliko magufuri.........
 
Ummemsikia Samiah akisema kuwa majadialianao yalikuwa magumu?. Mara sita wamekaa, na kina Wana CCM walikuwa hawataki mikutano iruhusiwe.

Nikuulize aliyeufyata ni Nani? Aliyezuia kufanya mikutano au aliyeruhusiwa kufanya mikutano
Kama CCM, tutaendelea kuwapa series za filamu mpaka mchoke, tumemaliza hiyo, inayofuata pia mtachukua mwaka na nusu mpaka 2024 August
 
Kuna kipindi CHADEMA walipigwa kote kote sio mahakamani, sio bungeni sio serikalini. Na hakuna msaada waliopata, walikuwa Kama yatima. Huku Lissu analimwa Risasi, huku Mbowe anavunjiwa bilcanas, huku akina Halima wanafukuzwa bungeni, huku Saanane anapotezwa. Nani aliwasaidia?.

So CHADEMA wameamua kukaa na maadui zao ili kukomesha hayo yasijirudie Tena, ndio maana wanarekebisha sheria za mikutano ya hadhara ili wapinzani wasiminywe Sana.
Wanapoozwa tu kiaina ila mbinyo bado upo pale pale.

Allen Kilewella JokaKuu
 
Kwa nini shujaa wako alizuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa?!
 
Sheria Inaruhusu Shughuli Za Vyama Vya Siasa Kwa Mujibu Wa Katiba

Aliyezuia Alitumia Sheria Ipi?Alitengua Iliyokuwepo


JE Viongozi Wanaapa Kulinda Katiba Na Kuitetea
Wakati Mfano Inavunjwa Mbona Anayevunja Haambiwi Mfano Na CDF,IGP
 
Yaani hawa wapinzani wa Tz sio Kama wataacha Legacy yoyote .

CCM chama kimejaa watu waliokosa utu na Huruma na zero brain...
Kumbuka hata TANU ilibidi wakae Meza moja na Wakoloni, ANC ilibidi wakae Meza moja na Makaburu... Wakoloni Weusi kukubali kukaa Meza moja na Wapinzani ni mwanzo mzuri.
 
249137BB-84B4-4A96-947B-6505F894E1E4.jpeg

#LIVE: Rais Samia na viongozi wa kisiasa

Leo Jumanne, Januari 3, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia amesema; "uwepo wangu leo hapa mahali nimekuja kufanya ruhusa ya mikutano hii, nimekuja kutangaza kuondoa zuio la kuzuia mikutano ya hadhara na ninasema kwamba, sasa linaondoka."

Ili kuendelea na mikutano hiyo, Rais Samia amesema jukumu sasa linabaki kwa vyama vya siasa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola kama sheria na kanuni zinavyoelekeza ili vipatiwe ulinzi.
Rais amesema hatua waliyoifikia katika mazungumzo baina ya vyama hivyo na Serikali kwa sasa, mikutano hiyo haitazuiliwa tena.

"Ruhusa ya mikutano ya kisiasa itatolewa, wajibu wetu sisi Serikali ni kuwalinda mfanye mikutano yenu salama mmalize vizuri, kufuata kanuni ndio wajibu wenu vyama vya siasa," amesema.

Ikumbukwe kuwa hatua hiyo ya Rais Samia inakuja ikiwa ni takribani mwezi mmoja umepita tangu akabidhiwa ripoti ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi, ambapo katika ripoti hiyo, viongozi wa vyama vya siasa waliweka bayana hitaji namba moja kuwa ni mikutano ya hadhara ambayo ilizuiliwa.

Akiwasilisha mapendekezo ya kikosi kazi mwezi uliopita kwa Rais Samia, Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho, Profesa Rwekaza Mukandala alisema kuwa kilipendekeza mikutano ya hadhara iruhusiwe kufanyika kwa mujibu wa katiba na sheria.

“Yafanyike marekebisho ya sheria ili kuhakikisha mikutano ya hadhara inafanyika kwa ufanisi, sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258, Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi Sura 322, Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa za mwaka 2019,” alisema Profesa Mukandala.

Leo akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa, Rais Samia amesema atazungumza na vyombo vya dola ili kuhakikisha suala hilo linatekelezwa kwa ufanisi.

“Ni haki kwa vyama vya siasa kuendesha mikutano ya hadhara lakini ndugu zangu tuna wajibu. *Kwa upande wa serikali tumeshajipa wajibu wetu kuwa ni kulinda mikutano ya vyama vya siasa, wajibu wenu vyama vya siasa ni kutupa taarifa kama sheria na kanuni zinavyosema kisha vyombo vinatoa ruhusa,” amesema
“Wakiona kuna hatari hawatoi ruhusa kwa hatua tuliyofika ruhusa za kufanya mikutano zitatolewa kwa sababu wajibu wetu ni kuwalinda mfanye mikutano kwa usalama, mmalize vizuri muondoke vizuri.”*

Pia, amesema, “mimi siwaiti nyie vyama vya upinzani, vyama vya kuwaonyesha changamoto zilipo, mnapinga nini, mnampinga nani, ndani ya Tanzania tunapingana kwei, tunaonyeshana changamoto ziko wapi, kasoro ziko wapi na mkinionyesha nikiwa msikivu nikazitekeleza nitaongeza imani kwa wananchi.”

Rais Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM amesema; “mazungumzo baina ya Serikali na vyama vya siasa bado yanaendelea, kuna mambo mengi ambayo itabidi tuitane, tuzungumze, tushauriwe, tukubali, tukatae kwa hoja lakini hivyo mazungumzo na maridhiano bado yanaendelea.”

“Mimi imani yangu, vyama vya siasa tutaendelea kukaa tuzungumze mambo yanayohisu nchi yetu,” amesema
 
Back
Top Bottom