Rais Samia aruhusu vyama vya siasa kufanya Mikutano ya hadhara

Rais Samia aruhusu vyama vya siasa kufanya Mikutano ya hadhara

No i don't think so, ni kwa vile kiongozi alie madarakani ni mwenye mtazamo tofauti na alietangulia.

Swala la kuanza kufanya mikutano na maandamano mbali mbali halikuanza kupangwa leo. Wengi walijaribu lkn walizuiwa kufanya hiyo mikutano hata ile ya ndani, na wengine walifunguliwa kesi za kufanya mikutano bila kibali bila wapinzani wenzao waliopo nje kufanya chochote.

So kwa sasa ni kushukuru tu kutokana na aina ya kiongozi tulie nae, bila maamuzi yake hakuna ambae angefanya mkutano hata wewe mwenyewe rohoni unalijua hilo mkuu.
Mkuu sipingi mawazo ila nakwambia ilikua swala la mda tu, hivi mfano chadema ingeamua KILA Kijiji au mtaa tz nzima FANYA mikutano ya adhala KWa siku MOJA ,nini kingezuia, ?

By the way Kiongozi tulienaye sio kwamba ni mzuri kuliko wengine ,bali yapo mazingira yanakulazimu FANYA Jambo hata kama hulipendi
 
Acha uongo wako hapa wewe,Chama gani Cha kujitambua hicho? Chama gani kingeweka mguu wake jukwaani pasipo ruhusa ya mh Rais wetu mpendwa?
Huu mwaka tu 2026, chahwa wote wa ccm hawana nafasi ya kubishana na mpakwa mafuta wa Bwana , KAZI imeishaisha kilichobaki ni mda tu, mtaanza ishi KWa aibu sana
 
Na Samia Suluhu Hassan

Wakati naanza uongozi wa nchi yetu, busara zilinituma kwamba jinsi nilivyolipokea taifa hili kuna haja ya kufanya liwe kitu kimoja. Nikasema lazima tuwe na maridhiano. Kwenye maridhiano, jukwaa kubwa ni vyama vya siasa. Nikasema kwanza tuwe na mazungumzo ndani ya vyama.

Desemba 2021 niliunda Kikosi kazi cha Kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa ambacho kilifanya kazi kwa weledi kwa miezi 10 na kuleta mapendekezo. Moja ya jambo lililozungumzwa sana ni zuio la mikutano ya hadhara. Leo nimeruhusu kuondolewa kwa zuio hilo.

Mbali na zuio la mikutano ya hadhara, yapo mapendekezo ya marekebisho ya sheria mbalimbali. Sheria kadhaa ziko njiani kurekebishwa ikiwemo ya Tume ya Uchaguzi. Wakati sheria hizi zinafanyiwa kazi lazima kuwa na ushiriki mpana wa vyama vya kisiasa na vya kijamii.

CCM tunaamini kukosolewa na kukosoa. Kazi ya serikali itakuwa ni kutekeleza. Ndio maana mimi siwaiti vyama vya upinzani bali vyama vinavyotuonyesha kasoro.

Tukaendeshe siasa za kistaarabu, zenye kuheshimu sheria, mila na desturi. Vyombo vya ulinzi na usalama vitawalinda.

Chanzo: @Instagram?/samia_suluhu_hassan
 
Hii Ndio Tanzania ninayoijua Mimi!

Umoja na mshikamano ndio ngao yetu!!

Hebu twende Sasa!!
Mkuu ' Mwl Athumani Ramadhani' ninakuaminia sana katika hili la "Umoja na Mshikamano", nami niko bega kwa bega nawe juu ya hili.
Lakini hivi ni kweli tunaizungumzia Tanzania, wakati kuna watu kati yetu wana "mambo yao", yanayowatenganisha na waTanzania wengine?

Hivi kwa nini isitoshe tu kuwa sote ni waTanzania, mwanzo na mwisho!
 
Kila hatua ni fursa kwa watu wenye kujielewa.
Hii hapa itakuwa ni fursa inayoweza kubadili mwelekeo wa nchi endapo watu watakuwa tayari kuitumia. Kama kuna ujanjaujanja unaofanywa, watu watauona na kuusema wazi kuwa ni ulaghai.

Pa kuanzia kukaza nati ni hapo kwenye hiyo Kamati inayotarajiwa kuundwa (sijui inaundwa na nani); na ni nani anaipa "maelekezo."?
 
Mkuu sipingi mawazo ila nakwambia ilikua swala la mda tu, hivi mfano chadema ingeamua KILA Kijiji au mtaa tz nzima FANYA mikutano ya adhala KWa siku MOJA ,nini kingezuia, ?

By the way Kiongozi tulienaye sio kwamba ni mzuri kuliko wengine ,bali yapo mazingira yanakulazimu FANYA Jambo hata kama hulipendi
Mkuu kwa vijana wa miaka hii amini kwamba hakuna ambae angekuwa tayari kuweka maisha yake hatarini dhidi ya serikali.
Usirubuniwe na maandalizi ya mitandaoni ambayo mwisho wa siku wale wanaohimiza wenzao mitandaoni huwa hawatokei mkutanoni kwa kuogopa kibano cha polisi.
Mifano ni mingi nafikiri hata wewe unajua. Labda upinzani wa miaka ile ya 2012, 2013 hadi 2015. Ila kwa sasa hakuna ambae angeona gari la polisi nje au barabarani afu aende mkutanoni, nakuapia mkuu hakuna, huo ndio ukweli.

Tushukuru raisi kaamua kutumia busara zake, vinginevyo hakuna ambae angefanya chochote kama ilivyokuwa wakati ule wa kesi ya Mbowe, Ukuta nk.
 
Mkuu binafsi siwezi kurubuniwa na mtu au kundi flani, but nitafanya kitu kile nimeamua nikiwa na akili timam ,

Ukifa KWa mateso ila KWa haki ni neema Sana, na ndo unakua mpango wako wa kifo tangu TOKA tumboni mwa mama mzazi wako, mengine hua ni mapambio kwamba amekufa kisa flani,

Nasema tena ilikua swala la mda tu , naongea hivi WENDA ukachukulia simple ila yapo mengi ndani ya faragha yangu na Mungu wangu,
 
Moyo wa mtu msitu mkuu, sina uhakika kama haya unayoyasema ni ya kweli au la. Ila sasa je ungepambana peke yako. Maana kama nilivyokwambia kuna watu ni mahodari wa kuchagiza jambo ila unapofika muda wa vitendo mtu anaingia mitini na kukuacha peke yako.
Narudia tena pengine wewe ungeweza lkn vijana wenzako wa mitandaoni wasingeweza. Believe me mkuu.
 
Mkuu , serikali yangu ya kiroho ni kubwa kuliko serikali zote za kidunia , naishia apa,
 
Binafsi naona mama ameruhusu mikutano ili apate cha kuwaambia mabalozi wa mataifa makubwa wakati atakapokutana nao kwenye hafla ya mwaka mpya kama ilivyo desturi.

Mama hatamani kabisa kitu kinaitwa mikutano ya hadhara ila mkopeshaji hilo ni sharti lake kuu.

Ndio maana unamuona anatamani kuwaambia wapinzani kasemeni hivi na vile ili iwe rahisi kwake kujibu.

Mikutano hii ni kama amejipalia makaa kichwani ngoja tuone
 
HUYU MAMA YETU HUYU... YAANI WATU HAWANA HATA HABARI NAE YANI... TANGAZO LINALOMHUSU HATA HALISISIMUI... ZAIDI YA KUZIDI KUTIA HASIRA TU...

KWA SABABU HATA UKISEMA UKAMSIKILIZE ATASEMA NINI... HAKUNA LA MAANA.
[emoji2957][emoji2957] SASA MATANGAZO YA KUNYA AKILI NA KUBAKISHA [emoji117][emoji90][emoji90][emoji90] NA LEGACY YAKE YA KUNYA AKILI.......NANI ANAVITAKA LABDA MZAZUZU TU
 
Back
Top Bottom