Rais Samia atembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko Katesh, Wilaya ya Hanang, Manyara na Kuzungumza na Wananchi, leo Disemba 7, 2023
Wataalamu waelezea udongo kunyonya maji mengi katika mlima Hanang

14 October 2022​

KIFAHAMU CHANZO CHA MAJI CHENYE MITO NANE NDANI YA MLIMA HANANG NA MSAADA WAKE KWA WANANCHI

Mhifadhi wa hifadhi ya Mlima Hanang yenye utajiri wa maji ya kutosha kwa matumizi ya nyumbani na katika mashamba makubwa ya ngano.

View: https://m.youtube.com/watch?v=kXIktyk8JUU
Maji yanayopenya ktk miamba (Underground water system) na kutiririsha maji mengi kupitia chemchemi za maji kujitokeza ktk miamba na kufanya mito ya maji kadhaa kutiririka kutoka hifadhi ya msitu wa mlima Hanang nchini Tanzania.

Mlima Hanang uhifadhi maji kwa misimu mingi hata mvua zisiponyesha kwa miaka kadhaa anabainisha mhifadhi wa msitu wa mlima Hanang.

Hivyo mlima Hanang ni kama dodoki yaani sponji 🧽 kukusanya maji mengi hivyo miamba na ardhi ya mlima kuwa na unyevunyevu petevu kwa kuelemewa na maji, ndiyo maana kuna chemuchemi nyingi kutoka miambani na pia katika miteremko ya mlima huo wa nne kwa urefu nchini Tanzania ....


Dr. Magoma atoa somo kuhusu mafuriko yaliyotokea Hanang
Dr. Derrick Magoma Ph.D afafanua janga lilivyojijenga na kutokea, mbele ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh. Freeman Mbowe na ujumbe alioongozana nao walipofika Hanang' kutoa pole


View: https://m.youtube.com/watch?v=hkLCiGOj3_c
Source : chadema kaskazini

More info :
Washington State

Wataalamu wa Geomorphology wanaelezea utafiti wao kuhusu majanga maporomoko ya ardhi, matope na milima kama ya mlima Hanang yanavyoweza kutokea


View: https://m.youtube.com/watch?v=jDqXgopte-0
Maporomoko ya ardhi hutokea wakati vitu-asili kama vile vifusi vya magogo na majani yaliyooza(mboji), miamba, tope zito na udongo kungoka kutoka uso wa mlima na kuteremka kuelekea chini bondeni kwa kasi inayoweza kukaribia maili 100 kwa saa. David Montgomery msomi kutoka Chuo Kikuu cha Washington aliyejikita kusoma maporomoko ya ardhi yaliyopita na ya sasa ili kujaribu kuelewa ni nini husababisha maporomoko ya ardhi . Kilipu hii ya video "Asili Inapofanya Yake / When Nature Strikes" imetolewa na kituo cha televisheni cha NBC News Learn kwa ushirikiano na mfuko wa Wakfu wa Kitaifa wa Sayansi.


Landslides occur when material like debris, rock, and soil become dislodged from the earth and slide downward at speeds that can approach 100 miles per hour. David Montgomery at the University of Washington studies past and present landslides to try to understand what causes them. "When Nature Strikes" is produced by NBC News Learn in partnership with the National Science Foundation.
 
Hili ndio jambo la Aibu la kufungia Mwaka 2023 , lakini cha kushangaza ni kwamba Wananchi wa Hanang ni kama wamepuuza ujio huo huku wakionekana wazi kujitenga...

Ndugu Freeman Aikael Mbowe ni Mwenyekiti wa Chama kikubwa cha siasa nchini anapokwenda katika shughuli yenye itifaki ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT SAMIA SULUHU HASSAN taarifa zinapaswa kupatikana mapema Je uwepo wa Mbowe Hanang, CHADEMA kilitoa taarifa na Je walikuwa sehemu ya Itifaki?majibu ya Sauti ya matukio ni wazi kutokuwepo taarifa za ujio uwepo wake,

Mbowe amekuwa sehemu ya wananchi wa kawaida kuzuiwa kutokana na taratibu za Itifaki ambapo maeneo aliyokuwa alikusudia kutembelea yalikuwa sehemu ya itifaki ya Mfariji Mkuu wa Taifa ndio maana kwa hekima kubwa kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara amekutana nae na baada ya kujua amefika Mkoani Manyara kuungana na Rais Samia kutoa pole na ratiba ya kutembelea wahanga,itifaki yake ikaandaliwa na kuruhusiwa kuungana na Dkt Samia katika shughuli ya Hanang, lakini yeye na timu yake wakaamua kuishia Babati bila kufika katika eneo la maafa.
 
MAMBO YALIYOFANYWA NA SERIKALI YA RAIS SAMIA, KATIKA KUKABILIANA NA MAAFA YA HANANG

● Serikali Imewaokoa Watanzania 117 na waliopewa huduma bure za matibabu kupitia gharama iliyobebwa na Rais Samia.

● Serikali imegharamia mazishi ya Watanzania 79 waliofariki kwenye maafa ya Hanang.

● Serikali inaendelea na zoezi la kutafuta miili ya watanzania wengine walioathirika na maafa hayo.

● Serikali imeanzisha makazi ya muda kwa wakazi 440 ambao walipoteza makazi yao ya kudumu.

● Serikali inatoa huduma za Malazi, Afya, Chakula, usafi pamoja na huduma za kisaikolojia.

● Serikali imeendelea kugawa misaada mbalimbali kutoka kwa Sekta mbalimbali.

● Serikali inaendelea kusikiliza na kutatua changamoto za mtu mmoja mmoja walioathirika na maafa.

● Serikali imetoa Askari 1200 wanaohusika kwenye zoezi la uokoaji wa maafa.

● Setikali imeandaa chakula kinachotosha kwa siku 30 kwa ajili ya wananchi.

● Serikali inapambana kurejesha miundombinu inayotakiwa kwenye mitaa na vijiji na huduma za biashara zimeanza kurejea.

● Serikali imerejesha tena huduma za umeme Hanang Transfoma 79 zimerejeshwa na Nguzo 600 zimesimamishwa tena.

● Serikali imeanza kuchimba visima 10 vya maji, pia imeleta matanki ya maji yenye lita za maji 5000.

● Serikali imetoa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi Milioni 300.
 
c8b37547-bcd1-4b06-a9cf-6b7a7d8a0e48.jpeg4629cdef-0266-4ce4-81b7-1b422f95fae2.jpeg
 
Yaani Jennister Mhagama kaongea vizuri, kwa Kujiamini utadhani Yeye ndiyo Mtu ila Mtu Mwenyewe kwa dakika zote nilizomsikia sikumwelewa sana sana nilichokuwa nakisikia hasa ni Kikohozi na Kukohoa Kwake Kwingi tu.
You are wasting your time, hivi tangu lini watawala wa Afrika wamekuwa serious na kuongea hoja sensitive kwenye masuala kama haya ya majanga kwa raia wao???

"Katika nchi za Afrika hakuna Serikali, bali kuna Magenge ya watu walioshika silaha na kupora rasilimali za nchi ili kujinufaisha wao wenyewe pamoja na vibaraka wao."
Jonas Savimbi, aliyekuwa Mwanasiasa na Mwanamapinduzi wa Angola.
 
Yaani Jennister Mhagama kaongea vizuri, kwa Kujiamini utadhani Yeye ndiyo Mtu ila Mtu Mwenyewe kwa dakika zote nilizomsikia sikumwelewa sana sana nilichokuwa nakisikia hasa ni Kikohozi na Kukohoa Kwake Kwingi tu.
aisee popoma umesema Kweli hajaongea ishu ya maaan kbsaa hata dkk tano Ni nyingi hotuba gani hi jmn
 
You are wasting your time, hivi tangu lini watawala wa Afrika wamekuwa serious na kuongea hoja sensitive kwenye masuala kama haya ya majanga kwa raia wao???

"Katika nchi za Afrika hakuna Serikali, bali kuna Magenge ya watu walioshika silaha na kupora rasilimali za nchi ili kujinufaisha wao wenyewe pamoja na vibaraka wao."
Jonas Savimbi, aliyekuwa Mwanasiasa na Mwanamapinduzi wa Angola.
Huu ndio usemi wa Savimbi?
 
Yaani Jennister Mhagama kaongea vizuri, kwa Kujiamini utadhani Yeye ndiyo Mtu ila Mtu Mwenyewe kwa dakika zote nilizomsikia sikumwelewa sana sana nilichokuwa nakisikia hasa ni Kikohozi na Kukohoa Kwake Kwingi tu.
Chedema team nayo ilikuwa kule Katesh.
 
Back
Top Bottom