Rais Samia atengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt. Raphael Chegeni

Rais Samia atengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt. Raphael Chegeni

Huyu hata hajaimba mkuu, kashika mic tu mama kamwambia nyimbo zako sizitaki.😀😀

Sure man...

Sijui shida i wapi, hii si mara ya kwanza au ya pili n.k kwa mamlaka kupangua gia za teuzi juu kwa juu kabla hata wahusika hawajasema alhamdulilah!
 
Tulikuwa tunashusha mizigo ya chegeni hapa musoma ghafla tunaabiwa turudi nayo tulipotoka
Hahaa, majirani zake aliowaaga kwa mbwembwe kama nawaona wakicheka,

Sijui atawaambia nini mzee wa watu.
Bora asingeteuliwa kabisa, hii ni aibu hadi kwa familia
 
Kwa mujibu wa Taarifa ya Ikulu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassani, amemteua Meja Jenerali Suleimani Mungiya Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na kutengua uteuzi wa Dr. Raphaeli Chegeni.

Kabla ya uteuzi huo, Meja Jenerali Suleimani Mzee alikuwa Kamishina Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini.

#Mwakammojanasamia #kaziiendelee
View attachment 2310209
Hapa aliyedhamiriwa kutenguliwa ni Suleiman Mzee.
 
Yaah CGP kuwa Mkuu wa Mkoa ni demotion tu
Akiwa CGP alikuwa anasimamia magereza na miradi yao nchi nzima, ndo ana manage mafungu yote ya Magereza sasa leo kuwa RC ni kwamba kashuka sana
Unaangalia mafungu kwako ndio kipimo cha demotion,sasahivi huyo anapigiwa saluti na wakuu wote wa majeshi ya ulinzi na usalama,ni raisi katika mkoa wa mara.

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
 
Balaa hili. Huyu kamishina wa magereza kapata demotion ta kufa mtu. Tuliambiwa ni mchapa kazi .Imekuwaje tena ?Chegeni nae nani kamchongea ?Dunia hii ving'ast wamejaa tele. Hapo baba wa watu kishashona suti. ***** [emoji23]
Mmedangwa na nani amekua demoted ,kipesa cjui ila kicheo amepanda ,hapo sasa hivi anapigiwa saluti hadi na CDF .yeye ni sehemu ya rais wa nchi now

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
 
Bora aliyepewa ubalozi hii sasa ni too much[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ubalozi na ukuu wa mkoa,aliyepata shavu ni mkuu wa mkoa ndio representative wa raisi,balozi anaripoti kwa katibu mkuu wizara ya mambo ya nje

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
 
Nadhani hili atalitolea ufafanuzi kesho akiwaapisha.

Watu tupunguze mawazo ya njaa njaa, huyo Chegeni sio kijana useme ndio anatafuta maisha, alishayatafuta kwa kuhudumu serikali zilizopita, sio mgeni kwenye siasa.
Likely anaweza kuwa hata yeye kaomba kusitishwa uteuzi kwa heshima.
 

Teua/Tengua

Cheo Ni Dhamana

Ahadi Ya Mwana TANU
 
Chegeni huyu ninayemjua kaomba mwenyewe kutenguliwa, pesa anazo si za nawazo ..Isamilo Hotel ya jijini Mwanza, Majumba ya kutosha Dar, Dodoma, Mwanza nk...watoto wake wote wapo kwenye Financial institutions kubwa Dubai, Austraria na USA, mke wake.....niishie hapa nisije jichoresha Bure nyuma ya I'd feki! Kifupi jamaa pesa ipo, kwenye siasa Kawa mbuge wa Busega kuanzia kwa Mkapa hadi awamu ya tano alipoondelewa na yule dk wa mifugo....Kisha kuingia tena na baadae Jiwe akamuweka pembeni pamoja na kuongoza kura za maoni!
Kichwani jamaa yupo vizuri, exposure ya nchi za wenzetu pia SI haba...huyu kumpa ukuu wa Mkoa ni sawa na kumuweka kundi la akina Sendeka wachumia tumbo!

Tengua ya Leo ngoja tusubiri ufafanuzi vinginevyo rais wetu kazungukwa na mafisi kundi la watu wa ovyo kuwahi kutokea!
 
Siku chache baada ya Wakuu wa Mikoa wapya 9 kuteuliwa, Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Dkt. Raphael Masunga Chegeni

Amemteua Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, na ataapishwa na Wateule wengine kesho (Agosti 01, 2022)

Kabla ya uteuzi wa Rais, Meja Jenerali Mzee alikuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP)

View attachment 2310242

View attachment 2310215
Kumbe mkeka bado unaendelea
 
Back
Top Bottom