Rais Samia atoe amri Paul Makonda naye akamatwe kwa Tuhuma zake zinazoendana na za Ole Sabaya

Kuwa serikalini au kutokuwa serikalini hakufuti jinai ama matumizi mabaya ya ofisi pindi wakitumika... rejea kesi ya kina Yona na mwenzake...
 
Huyu bwana, Ambaye alijitanabaisha mwenyewe kwamba anakula bata kuliko mtu yeyote nchi hii katika awamu ya mwendazake. Na ni kweli alikuwa hagusiki.

Kwa namna huyu jamaa alivyokuwa anayaishi maisha ya uongozi, kama asingegombea ubunge akabaki na ukuu wa mkoa mpaka leo. Kwa huu uongozi wa mama yawezekana angekuwa Lupango. Huyu jamaa kwa madhambi nadhani kamzidi Sabaya.

Kama ikitokea akafanyiwa uchunguzi huyu haponi wala hasafishiki na tuhuma zake ziko wazi kabisa.

Vijana mnapopewa madaraka, Ongezeni kwa haki, weledi na ubunifu kumbukeni kuna kesho.
 
watampa ukuu wa wilaya huko mbelembele hakuna namna amepauka sana analialia tu kwenye makanisa kila siku
 
Hamna walichofanya hao ni kawaida yao kulindana tu, wanakutumbua wanakuondoa kwenye nafasi yako then wanakuacha, huyu Sabaya sidhani kama watampeleka mahakamani.
 
Hamna walichofanya hao ni kawaida yao kulindana tu, wanakutumbua wanakuondoa kwenye nafasi yako then wanakuacha, huyu Sabaya sidhani kama watampeleka mahakamani.
Kwa kosa gani alilofanya kwanza
 
Kuna uwezekano mkubwa Paul Makonda akaunganishwa kwenye tuhuma za uhujumu uchumi zinazomkabili Ole Sabaya ambaye Rais Samia Suluhu ameamuru achunguzwe. Sababu zinazopelekea kuunganishwa huku ni kwa sababu ya staili ya uporaji fedha kutoka kwa wafanyabiashara inayotumiwa na Sabaya kufananishwa na staili ya Makonda (Makonda style). Ukimsikiliza vizuri mfanyabiashara huyu hapa chini aliyeibua sakata la uporaji wa Sabaya utagundua kwamba Makonda na Sabaya huenda wapo kwenye kikosi kimoja na aina yao ya uhujumu uchumi inafanana pia:

Mfanyabiashara huyu ametamka kinagaubaga kwamba Sabaya alipokuwa akimtisha ampe fedha alisema anatumia ‘Makonda style’. Kwa maana hiyo, Sabaya anafahamu staili ya uporaji wa Makonda na kwa kuwa mwizi hushikwa na mwizi mwenzie, kuna uwezekano mkubwa wawili hawa walikuwa akishiriki uhujumu uchumi kwa namna moja.

Kuna ufanano mkubwa wa Makonda na Sabaya katika mambo mengi tu. Mosi, wote ni ‘watoto’ wa mwendazake kwa kuwa hata wafanye madudu kiasi gani mwendazake alikuwa hawezi kuwachukulia hatua zozote. Ishu ya Sabaya kupora fedha za wafanyabiashara kwa vitisho ilishawafikia mwendazake na Waziri Mkuu lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Jeuri hii iliwapelekea kufanya chochote watakacho bila hofu yoyote.

Pili, Makonda alishuhudiwa akiwadhalilisha wanaume wa Dar kupitia programu bubu ya kuwasaka wanaume waliowatelekeza wanawake zao na hali hii ilikwakera watu wengi lakini hakufanywa chochote na aliyemteua. Aidha, Sabaya amefanya madudu mengi sana wilayani Hai lakini mwendazake alikaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea.

Tatu, Sabaya amekuwa akitembea na kikundi cha Mungiki (mabaunsa) ambao huwatumia kutimiza azma yake ya kuhujumu uchumi. Hali kadhalika, Makonda alikuwa anamiliki kikundi kama hicho (makirikiri) ambao walikuwa wakimsaidia kutimiza uhujumu wake. Mfano mzuri ni pale alipovamia studio za clouds TV akiwa na kikosikazi chake hicho na kufanya vurugu kubwa akitaka kipindi chake kirushwe hewani (utadhani yeye ndiye Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media):

Ukilinganisha mfanano wa wawili hawa kisha ukaunganisha nukta, utatengeneza mstari unaowaunganisha wote pamoja. Kuna ishu ya Sabaya kukutwa na kitambulisho kinachoonyesha kuwa yeye ni mtu anayefanya kazi kikosi maalumu (wengi mmekiona mitandanoni). Huenda Makonda na Sabaya wote wamo kwenye kikosi hiki kwa kuwa pia staili zao za uhujumu zinafanana.

Kwanini sasa DPP asimuunganishe Makonda kwenye ishu ya Sabaya ili suala hili lishughulikiwe kwa pamoja badala ya kusubiri kumkamata peke yake? Wakiunganishwa wote wawili hata gharama za kuwashughulikia zitakuwa ndogo kuliko kudeal na mmoja mmoja kwa nyakati tofauti.

Mimi namshauri DPP amuunganishe Makonda kwenye skendo hii ya Sabaya kwa kuwa tayari ametajwa na Sabaya kuwa wanatumia staili moja ya uhujumu (kupitia kwa mfanyabiashara huyo anayelalamika hapo juu).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…