Hatimaye Ole Sabaya ameingia Kingi, hiyo yaweza kuwa headline nzuri kwa magazeti ya kesho.
Nawapongeza sana watu wa mitandao ya jamii kwa kelele na sauti ambazo tulipaza mpaka huyu Dhalimu akapatikana.
Sasa napendekeza tulianzishe kwa Paul Makonda maarufu Kama Daudi Albert Bashite mpaka naye awajibishwe kwa matendo yake maovu. Kimsingi uovu wa Ole Sabaya haufikii hata robo ya uovu wa Makonda. Na kila alilokuwa anafanya Sabaya alikuwa anaiga na ku -consult kutoka kwa Makonda.
Tutumie silaha yetu ya "social media" kama wanavyotuita "key board warriors" mpaka Makonda akapate anachostahili. Tushambulie kila mahali kupitia JF, TWITTER na FB.
Hii kampeni ianze mara moja kutaja madhambi yake. Kama TAKUKURU au Polisi hawatachukua hatua, basi wanahatakati wa haki za binadamu wanaweza wakatushauri mamna ya kumfikisha Mahakamani