Rais Samia atoe amri Paul Makonda naye akamatwe kwa Tuhuma zake zinazoendana na za Ole Sabaya

Rais Samia atoe amri Paul Makonda naye akamatwe kwa Tuhuma zake zinazoendana na za Ole Sabaya

Nasisitiza Rais Samia Suluhu Hassan aamuru upesi sana aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Christian Makonda ( Daud Albert Bashite ) nae akamatwe na achunguzwe kwa Tuhuma zake ambazo ni zaidi ya alizonazo DC Ole Sabaya. Acha Unafiki Hopeless mkubwa Wewe sawa?
Si uende wewe mwenyewe ukafanye hayo unayo muagiza kama unaona amekuchelewesha?

Kwa nini uje kulialia humu JF. Sisi hatuwezi kukusaidia na ukichaa wako huo.

Naona kama wewe na Sabaya hamtofautiani kitabia.

Lakini ngoja nikuache na wazo la maana sana kama unaweza kulifanyia kazi na kukuletea manufaa kuliko hili unalolilia hapa.

Wakati huu ni wakati mzuri wa kukusanya taarifa za huyo Bashite bila ya kusumbuliwa na yeyote.

Ukipata taarifa muhimu zinazomhusu yeye, andika bonge la kitabu.

Ninaahidi kukupa msaada wa kukibadili kitabu chako iwe 'movie' itakayokuingizia pato zuri sana katika maisha yako; licha ya kujijengea umaarufu Tanzania nzima na nje ya Tanzania.
 
Makonda hayuko Serikalini sasa ila je, huko nyuma hakuwa Serikalini huko?

Kwahiyo Tuhuma za Mtumishi wa Serikalini huwa zinayeyuka pale akitoka Serikalini?

Kuna Waziri nchini Uingereza amestaafu miaka 17 iliyopita ila alikamatwa kujibu Tuhuma zake.

Nionyeshe ni wapi katika Katiba ya Tanzania inazuia Mtumishi aliyetoka Serikalini asihojiwe.

Kuna Watu mna Akili za hovyo hovyo tu.
Usiwe na haraka atashughulikiwa. Tulia
 
Makonda hayuko Serikalini sasa ila je, huko nyuma hakuwa Serikalini huko?

Kwahiyo Tuhuma za Mtumishi wa Serikalini huwa zinayeyuka pale akitoka Serikalini?

Kuna Waziri nchini Uingereza amestaafu miaka 17 iliyopita ila alikamatwa kujibu Tuhuma zake.

Nionyeshe ni wapi katika Katiba ya Tanzania inazuia Mtumishi aliyetoka Serikalini asihojiwe.

Kuna Watu mna Akili za hovyo hovyo tu.
Jambo la muhimu ni kwa wewe unayefahamu hayo makosa ukashtaki na uyatolee ushahidi mahakamani
 
Huu Uzi nusu umechangiwa na mwanzilishi. Anatumia nguvu kulazimisha hoja zake zikubaliwe.
 
Kwa katiba wanaweza kutafanya tuishi kama tumbili tena muda wowote.
Kubwa la maadui "Hon Paul Makonda" tumbo la kuharisha limemshika huko alipo.

Eid hii kuna watu watailia Mzena Hospital na drip za glucose mikononi ku stabilize BP.

Hawa viongozi waliopewa nyadhifa kutuongoza walitufanya tuishi kama tumbili ndani ya nchi yetu, unaamka asubuhi unasali kwa dini zote ili usiingie kwenye mikono yao ukapotezwa, sasa muda wao kuishi kama ngedele mamaqxe.
 
Kwa katiba yetu Tanzania Rais anaweza kufanya chochote.Anaweza kumfuatilia hata mtu aliyestafu mwaka 1970.
Hoja hapa ilikuwa Rais awachukulie hatua wengine kama alivyomchukulia Sabaya ya kuwasimamisha kazi wote kwa pamoja na ndipo likatajwa jina la Makonda!! Hapo ndipo tukabainisha kuwa Makonda hayupo tena serikalini hivyo sio rahisi kumchukulia hatua ya kumsimamisha!!

Suala la kuhojiwa kwa matendo yake alipokuwa RC na kama alivunja sheria hilo liko chini ya taasisi husika na sioa kazi ya rais kuwaambia nini cha kufanya kwani sheria ndio inayochukua mkondo wake!
 
Huko mnakotaka kuelekea siyo kwenyewe na taifa hili litabomoka. Mama aangalie sana.

Ili kutibu majeraha yote mama afuate ushauri wa Lissu. Aunde tume ya maridhiano, watu waombane misamaha, wasameheane, wenye kulipwa fidia walipwe halafu tusonge mbele. Haya mambo ya visasi hayataliacha salama taifa hili.
Yaani Intarahamwe kama Paul Makonda aombe Radhi kwa aliyoyafanya hadi hata Kumuudhi na Kumshangaza Shetani Mkuu Lucifer halafu Watanzania wamsamehe?
 
Nimejikuta nacheka tu, mshusha thread mwandiko wako, jazba na kurudia rudia kutaja jina lako vinashabihia na IDs nyingine mbili tatu hivi.

Umechangamsha genge somehow, hayo ya Bashite tuwe na subra muda utatupa majibu kwani yanayoendelea behind the curtain kwa tulio nje ya system hatuyafahamu.
Nadhani SASHA anakwenda sawia, one step at time huku akizingatia taratibu za kisheria si kama phase ya mwendazake ya kidnappings, detentions na eliminations.
SHASHA it is then!!!👍
 
Sijui unazungumzia sheria za wapi, huwezi kuchunguzwa under house arrest not in our jurisdiction kwa sheria za Tz haipo hiyo, uchunguzi waweza fanyika under police custody....
Sewahaji na Kibasila zote ni Muhimbili.
 
Si uende wewe mwenyewe ukafanye hayo unayo muagiza kama unaona amekuchelewesha?

Kwa nini uje kulialia humu JF. Sisi hatuwezi kukusaidia na ukichaa wako huo.

Naona kama wewe na Sabaya hamtofautiani kitabia.

Lakini ngoja nikuache na wazo la maana sana kama unaweza kulifanyia kazi na kukuletea manufaa kuliko hili unalolilia hapa.

Wakati huu ni wakati mzuri wa kukusanya taarifa za huyo Bashite bila ya kusumbuliwa na yeyote.

Ukipata taarifa muhimu zinazomhusu yeye, andika bonge la kitabu.

Ninaahidi kukupa msaada wa kukibadili kitabu chako iwe 'movie' itakayokuingizia pato zuri sana katika maisha yako; licha ya kujijengea umaarufu Tanzania nzima na nje ya Tanzania.
Kichaa zaidi yangu ni Yule aliyekuzaa tu.
 
Kwangu Mimi kutokana na Tuhuma zao ( hasa walipokuwa katika Nyadhifa zao ) namfananisha Ole Sabaya na Papa na Paul Makonda ni Nyangumi.

Utoaje AMRI ya Kuchunguzwa kwa Papa Ole Sabaya na ukamuogopa au ukamuacha Nyangumi Paul Makonda? Hapa Rais Samia Mimi Krav Maga sijakuelewa.

Rais Samia tafadhali hakikisha na hiki ulichokifanya kwa Ole Sabaya pia ukifanye kwa Paul Makonda kwani ana Madhambi yaliyomshangaza hata Shetani.
Kwa hiyo kila mtu akiamka anamuelekeza mama kitu cha kufanya!!???
 
Back
Top Bottom