Rais Samia atoe amri Paul Makonda naye akamatwe kwa Tuhuma zake zinazoendana na za Ole Sabaya

Rais Samia atoe amri Paul Makonda naye akamatwe kwa Tuhuma zake zinazoendana na za Ole Sabaya

Umesahau Pompeo ashamwambia marufuku kusafiri, nchi gani itafanya kinyume na US ilichotamka!
Mwisho wao umefika walidhan jiwe atatawala milele, wakae mkao wa kula na ikiwezkana passport yake izuiwe kwanza..
 
Tungesamehana tu tukatafuta katiba mpya na tume huru ili kutengeneza mfumo bora ( justice)

Tunasahau mifumo yetu ya utawala ndio inafanya watu wajisahau na kutena uovu kama huu.

Visasi havijawai kuleta amani na umoja.

Nelson Mandela angefanya visasi sijui kama angekuwa anakumbukwa kwa mazuri leo.
Ungekuwa mhanga ungeyasema hayo? Huyu anetuhumiwa na Marekani kwa kunyima haki ya kuishi.

Vyombo viachwe vifanye Kazi yake.Binafsi hata ungekuwa wewe umenitendea ubaya siwezi kukusamehe
 
Members, Kwa mujibu wa Gazeti la mwananchi Kamanda wa Takukuru Hamduni anasema watakapomuhitaji Paul Makonda watasema.

Hivi kwa mtu smart Unawezaje kuendelea kuwepo Nchini kwa matukio kama ya Makonda.

Maisha ya kuishi bila dhamana yatakuharibia familia na wewe mwenyewe, Una muda wa kujipanga na kukimbia, Sasa Unajadiliwa wewe kila kona ya nchi.

Mfalme hayupo tena, Nasema ondoka, Ondoka unasagiwa kunguni.

Tuhuma nyingi nzito hata kabla ya Ole Sabaya zilielekezwa kwa Paul Makonda na Kikosi kazi chake, Tena huyu alitembea na watu wenye sare kabisa bora ya Ole Sabaya,Makonda alipovamia Clouds media ili awashughulikie Shilawadu ilikuwa ni kama movie ya kivita.

Mali alizojipatia Bwana Makonda toka kwa matajiri kwa dhuluma zinajulikana, Ni Kheri akakimbia na kuanza upya maisha, Akikamatwa Mali hatazitumia tena.

Mtu smart angeanza kuuza Mali zake za dhuluma taratibu kabla ya kukamatwa.

Nina hakika hata akiendelea kubaki tayari amejawa hofu ambayo itamfanya aishi kama digidigi, Huyu alisema hakuna mtu anakula raha Tanzania kama yeye.
Hawezi kukimbia tena kwakuwa wako nyuma yake 24/7 ... Na mawasiliano yake yote yako mikononi mwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Chadema ilishindwa kwa sababu waliweka wagombea dhaifu
Ni dhaifu kuliko lile bunge ka ndugai pale dodoma?
Au unamaanisha dhaifu kiafya kuliko marehemu meko aliyekuwa na upungufu wa kinga mwilini covid ikamuondoa?
Unamaanisha udhaifu upi we mataga?
 
Atakimbilia nchi gani ili akawachafue watao mpokea wakati Marekani wamekwisha mtanganza ni muhaini wa kudhurumu uhai wa watu ? Hana pa kukimbilia, agangamane humu humu Tanzania... kama ni debe litamfaa tu, hakuna namna... Mwendazake kaondoka , kunguru wanarukaruka nani wa kuwakubali na mauchafu yao yote...mzoga wa kunguru hauliwi hata na wadudu...!
 
Kama serikali haitamchukulia hatua na kumchunguza huyu mtu,wananchi watakuwa na jambo lao
 
Members, Kwa mujibu wa Gazeti la mwananchi Kamanda wa Takukuru Hamduni anasema watakapomuhitaji Paul Makonda watasema.

Hivi kwa mtu smart Unawezaje kuendelea kuwepo Nchini kwa matukio kama ya Makonda...
Sasa akimbie aende wapi? Hapo koromije si watamkamata kama kuku wa mdondo tu!
 
Leo nimemuona Makonda akiwa Chato kutembelea Kaburi la Magufuli.

Katika ziara hiyo, Makonda eti alisimamishwa na wananchi wa Chato na kuzungumza nao. Na katika maigizo hayo,Makonda amelia sana...
Picha ipo wapi? Au unatuimbia mapambio tu!
 
Kwangu mimi kutokana na Tuhuma zao (hasa walipokuwa katika Nyadhifa zao) namfananisha Ole Sabaya ni Papa na Paul Makonda ni Nyangumi...
Una ushahidi ukisemacho? Mwache Raisi afanye kazi, ikigundulika makonda anahusika sheria itamshughulikia ipasavyo, mama hataki zulma. Hata JOKATE anahusishwa pia, nae yuko njiani.


Mama hataki ujinga, na atawanyoosha tu. Mitano tenaa, 10 tenaa
 
Leo nimemuona Makonda akiwa Chato kutembelea Kaburi la Magufuli.

Katika ziara hiyo, Makonda eti alisimamishwa na wananchi wa Chato na kuzungumza nao. Na katika maigizo hayo,Makonda amelia sana...
atuonyeshe pia lilipo kaburi la saa 8.
 
Katika ziara hiyo, Makonda eti alisimamishwa na wananchi wa Chato na kuzungumza nao. Na katika maigizo hayo,Makonda amelia sana.

Juzi niliona gazeti moja limeandika kuwa jalada la uchunguzi wa utekwaji wa mfanyabiashara maarufu Mo limepelekwa kwa DPP.
Huyu makonda ni mnafiki na mhuni mkubwa, 'amedhulumu' maisha ya watu, ametesa sana watu, amepora watu fedha zao na kila aina ya uhuni ameufanya huyu mtu. Sheria ichukue mkondo wake na asiachwe hata kdg.
 
Makonda alimpigia debe Mama ili awe makamu wa rais ndani ya bunge maalum la katiba. Sidhani kama ni rahisi kwa Rais kwa sasa kuweza kumfanya lolote Makonda.

Labda JK ambaye anao ushawishi awamu hii awe hajamsamehe Makonda kwa suala lile la mtoto wake kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya. Hivyo bado ipo sababu ya kumshughulikia ingawa namuona Rais akiwa na uhusiano mzuri na Makonda.

Alitumwa tu
 
Kuweka rekodi sawa, Makonda kama ilivyo kwa Sabaya, hana kitu chochote kile cha kujibu kwa yoyote yule hapa Tanzania na duniani.
Swali: Kama ni kweli kwanini basi Ole Sabaya anashikiliwa na polisi?...
Sasa mbona mayowe mengi,tulieni majambazi yashughulikiwe. Kama nauona ule msambwanda siku akibong'oa kukaribishwa gerezani Ukonga.
 
Tukianzia tukio la kuivamia clouds na mabunduki!
 
Kwangu mimi kutokana na Tuhuma zao (hasa walipokuwa katika Nyadhifa zao) namfananisha Ole Sabaya ni Papa na Paul Makonda ni Nyangumi...
Yaani huyo jamaa amejua life span yake imefika yaani Malaika wa zamu wameshaanza kimpigia simu tujiandaeni taratibu tu tutaimba zile nyimbo za taraatibu ndio maana anasema 2023 huko mbali hafiki
 
Back
Top Bottom