Rais Samia: BoT wajiandae kuruhusu Crypto-Currency

Rais Samia: BoT wajiandae kuruhusu Crypto-Currency

Rais Samia Suluhu Hassan hataki Sheria za nchi ziwe kikwazo kwa watanzania kutumia Sarafu za Kimtandao. Ameyasema haya leo wakati anazindua jengo la BoT Tawi la Mwanza.

Hivyo ameitaka BoT kuandaa mazingira ya kisheria na taratibu nyingine ya wananchi kutumia Sarafu za Kimtandao:- mfano Crypto-Currency na Bitcoin.
Mama naona anaelea kwenye mstari wa uchumi wakufaidisha watu wengi

Nikipata nafasi ya kukutana yae nitanshauri mambo mengi sana mazuri hasa kwenye upande wa wajasiriamali

Pesa za kigeni tunazikosa Kwasabu ya uzembe wa viongozi wa ccm kutokuwa wabunifu kwa muda mrefu

Kwanfano dunia iko kwenye e-commerce tuna weza uza bidhaa zetu kama mazao Madini na vitu kibao kwanjia ya online kupita EMS Posta nakupata pesa za kigeni lakini kuna vikwazo vya kufa mtu

Bidhaa zandani pia serekali inabidi sera na mipango inayokwenda na wakati watu wanatoka kwenye nfumo wa kuuza bidhaa madukani kuhamia kwenye maduka ya online Dunia iko huko kitambo
 
Crypto currecy ni very volatile wawe makini sio inshu za kukurupukia! Bank zinategemea fees na interest km asset/revenue with crypto currency kama bitcon,litecoin,etherium izo mambo hazipo wajiandae kisaikolojia ila km inchi tunaweza kuencourage matumizi ya blockchain techology coz inapply sehemu nyingi ilanmambo virtual curency yakaja baadae kidogo!
 
China juzi juzi imepiga marufuku Cryptocurrencies kutoka na sababu mbali mbali. Tesla nayo imetengua uhamuzi wake wa awali wa kukubali malipo ya crypto.

Crypto inakubalika nchi kama El Salvador ambayo inanuka rushwa!!

Tuwe waangalifu kuiga mambo ya wenzetu bila kufanya utafiti wa kina!!! Je tunajua sababu zinazowafanya magaidi , majangili na hard criminals wengine kupenda kutumia crypto currencies? What is the secret behind these currencies such that even China has put a stop to their use!
 
Cryptocurrencies imekuwa ina husishwa na,
1)fraud
2) money laundering
3)Bad for environment.
4)….list goes on

Crypto currecy is very secure transactions no fraud ,no intermidiatery km BOT nk,haiwi regulated na central bank coz yenyewe ni mtu kwa mtu transaction. The only problem ipo limit nadhani 21million na pia ni volatile sana - inaeza kupomoka thamani in matter of second au ikapanda haraka sana.Sioni hababu ya TZ kwenda huko kwa sasa
 
Crypto currecy ni very volatile wawe makini sio inshu za kukurupukia! Bank zinategemea fees na interest km asset/revenue with crypto currency kama bitcon,litecoin,etherium izo mambo hazipo wajiandae kisaikolojia ila km inchi tunaweza kuencourage matumizi ya blockchain techology coz inapply sehemu nyingi ilanmambo virtual curency yakaja baadae kidogo!
Ma bank ya Kibongo nayo yako kama ccm mambo yalishabadilika kitambo mtu unalipigia mzigo Dubai au ununugari Japan kwa BTC unatuma milioni 10 kwa fee ya buku ukiwa kitandni umelala

Kidogo kwenye Fiat itasaidia
 
Nimegundua kitu huyu mama ni mwepesi sana kumdanganya, naona kabisa tunapoelekea vitaruhusiwa vitu ambavyo hata shetani mwenyewe anaviogopa

Hakuna mfanyabiashara makini au anayefanya biashara zake kihalali akakubali malipo ya haya mafedha mtandao leo ukiuliza hyo bitcoin mwenyewe au founder ni nani wanasema ni Satoshi Nakamoto yupo wapi hakuna anayejua sasa kama mwanzilishi kajificha hyo ni biashara halali kweli?
 
Tuwe waangalifu kuiga mambo ya wenzetu bila kufanya utafiti wa kina!!! Je tunajua sababu zinazowafanya magaidi , majangili na hard criminals wengine kupenda kutumia crypto currencies? What is the secret behind these currencies such that even China has put a stop to their use!
Crypto ndio njia salama ya smugglers,wauza unga, magaidi, kwa nini? Kwa sababu haipo regulated na mamlaka za serikali.
Marekani pamoja na kwenda mbali kiuchumi na technology hawatathubutu kuruhusu crypto. Hapa mama awe makini
 
Nimegundua kitu huyu mama ni mwepesi sana kumdanganya sana naona kabisa tunapoelekea vitaruhusiwa vitu ambavyo hata shetani mwenyewe anaviogopa
Njoo na hoja ukiingia kichwa kichwa kwenye technology kama mganga wa kienyeji utaumbuka kamna una hoja ilete mezani
 
Mama asikimbilie hayo mambo, bado machanga sana na bado yako volatile sana. Nchi nyingi zilizoendelea bado hazijaruhusu hizo currency so hakuna haja ya kukimbilia.

Bitcoin yule jamaa wa Tesla Elon akiongea vibaya inaporomoka thamani, akiongea vizuri inapanda thamani, sasa currency gani iko weak namna hiyo inategemea kauli za wavuta bangi kama wale😂?
 
Hayo madude unaweza kulala tajiri ukaamka maskini kwa matamshi ya mtu.

Muhimu ni kufanikisha njia za watu ku transfer hela zao kwenye kampuni za kununua na kuuza stocks kama robinhood watu wachukue risk kivyao za kununua bitcoin, dogecoin na zingine.
 
Yaani mnakimbizana na vitu vya hovyo hovyo wakati kuzalisha tu mafuta ya mawese imekuwa ni mtihani hadi nchi inaingia kwenye crisis ya kukosa mafuta ya kupikia!
 
Mimi sijaelewa hivi hii inakuwaje sarafu mtandaoni kuukiza si ujinga
 
Nchi za Magharibi haijapigwa marufuku lakini bado Serikali nyingi ziko kimagutu magutu na hii currency kwanza haiko stable inaweza kupanda sana na kushuka sana pia kwa sasa matapeli wa mitandaoni wanaitumia sana hii pesa wakishafanya utapeli wao. Hii currency bado ina safari ndefu kukubalika hivyo tusikurupuke tukaingia kichwa kichwa bila ya kuwa na ufahamu wa kutosha kwenye hii kitu.
China juzi juzi imepiga marufuku Cryptocurrencies kutoka na sababu mbali mbali. Tesla nayo imetengua uhamuzi wake wa awali wa kukubali malipo ya crypto.

Crypto inakubalika nchi kama El Salvador ambayo inanuka rushwa!!
 
Mama anaendelea vzr. Kazi na iendelee Paypal waiintroduce fasta.
 
Crypto ndio njia salama ya smugglers,wauza unga, magaidi, kwa nini? Kwa sababu haipo regulated na mamlaka za serikali.
Marekani pamoja na kwenda mbali kiuchumi na technology hawatathubutu kuruhusu crypto. Hapa mama awe makini
Sio kweli marekani wana makampumy mengi sana kuliko nchi nyingi yoyote ubishi nitayataja hapa

Marekani Japan na baadhi ya nchi nyingine zizozo za wanyonge makampuny yao yanatoa hadi Card kama za bank wa members wao fanya utafiti usipotoshe watu
 
Njoo na hoja ukiingia kichwa kichwa kwenye technology kama mganga wa kienyeji utaumbuka kamna una hoja ilete mezani
Technology gani hapo unazungumzia ??? Nitajie nchi moja tu ambayo wameikubali hyo Bitcoin kuwa legal tender zaidi ya El Salvador? Kila nchi hawataki hayo mambo ya cypto unadhani ni wajinga mama yenu ndo anakili sana?
 
Back
Top Bottom