Rais Samia: Haiwezekani jeshi lifanye mauaji na lijichunguze lenyewe

Rais Samia: Haiwezekani jeshi lifanye mauaji na lijichunguze lenyewe

FB_IMG_1643977097439.jpg
 
Kesi ya nyani....

Hongera sana Mama kwa hilo yaani hawa Polisi huwa wanabebana sana
 
Polisi walishatoa tamko rasmi kwa umma kupitia msemaji wao Masime.

Sasa ikibainika haikuwa sahihi sijui watajisafishaje hawa maafande.

Inanipa mashaka hii ripoti kuwa tofauti na ile ya polisi wenyewe.
 
Unapounda timu kwenda kufanya kazi na ukategemea tume ifanye kazi nakuleta taarifa kamilifu unataka kuwaweka NJE ya ofisi inayochunguzwa watu wote wanaotuhumiwa. Jana IGP alifanya mabadiliko ya RPCs Lakini Mtwara aliachwa.

Kwa kauli ya Mhe. RAIS Nadhani RPC Mtwara pamoja na ukweli Kwamba yeye ahusiki na kile kilichotokea anapaswa kuhamishwa kituo Cha kazi kabla tume haijafika. Kumwamisha inasaidia kumlinda yeye asionekane amekwamisha kazi Lakini pia inatoa Uhuru wa tume kufanya kazi yake.

Akiendelea kuwepo Mtwara kwa muundo wa tume zetu anaweza kutakia kuisadia tume baadhi ya mambo na ikitokea bahati mbaya akwama tu kutoa ushirikiano ataonekana amekwamisha kazi.

Naamini kwa wataalamu wa utawala wataelewa namaanisha nn?
 
Ndio maana tunahitaji kutia moto msukumo wa kupata KATIBA mpya,hii issue sio ya kuundiwa tume maana huu ni ubadhilifu wa fedha za umma,katiba mpya ingetupa kitu kinachoitwa IPID hawa ni police within police ambao wajibu wao ni kupeleleza kesi zote ambazo police ni suspects,hawa wana uwezo wa to ARREST na kumfikisha mahakamani suspect(s)baada ya kushauriana na DPP,hawa IPID ni kama MPs wa jeshi ,ila wao wanauwezo zaidi wa kisheria.
 
KAMATI KAMATI KAMATI KAMATI KAMATI,
Matokeo ya kamati = Zero
Tupo wepesi kusahau.
Kamati ya Jaji yule aliyechunguza kuuwawa wale wachimba madini wa Morogoro, ili pendekeza kuwa polisi wahusika wapelekwe mahakamani.
Hapo ndipo ukweli ukaanza kujulikana wazi kuwa waliuwawa ili waporwe fedha zao.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Suluhisho ni Katiba Mpya.

Huyu Sirro alifaa awe pembeni siku nyingi sana.
 
However, huhitaji katiba mpya kuwa na chombo huru cha kusimamia taasisi ya jeshi la polisi.
Huwezi kuwa na katiba ambayo ni exhaustive namna hiyo. Kwamba kila kitu kiwe constitutionally covered. Mambo mengine yanahitaji kutungiwa tu sheria basi
An Act of Parliament vile. Ni sawa.
 
In the same token basi hata hiyo katiba mpya haitaleta muujiza wowote maana watu ni wale wale with the same mindset
Siyo kweli kwa kuwa uki- overhaul katiba utendaji wa watendaji utabadilika na baadhi ya watendaji wataondoka katika nafasi zao!
 
toka umemua Rais leo ndio umeongea kitu cha msingi kabisa .

Polisi ndio wahalifu namba 1 Tanzania halafu eti hao hao wanapambana na uhalifu !

si ujinga huu wa kiwango cha rami kabisa ?
 

Rais Samia Suluhu Hassan amezungumzia mauaji yaliyotokea Mtwara ambapo maafisa wa Jeshi la Polisi wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara Mussa Hamisi ambapo Jeshi limeunda kamati kuchunguza tukio hilo.

Rais amesema haiwezekani Jeshi kutuhumiwa kisha liunde kamati ya kujichunguza lenyewe, hivyo amesema amemuagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aunde kamati nyingine kuchunguza tukio hilo.

Amesema taarifa ya kamati ya polisi inayochunguza tukio hilo, italinganisha na taarifa ya kamati huru itakayoundwa na Waziri Mkuu.

Ameyasema hayo akiwa njiani akielekea Mwanza.

=======

Pia soma:
Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7 (25/01/2022)

Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022 (26/01/2022)


Kiundwe chombo huru cha kusimamia Jeshi la Polisi (25/01/2022)

Kwenye kamati itakayoundwa miongini mwa wanakamati wawemo na watetez wa haki za binadamu
 
Sidhani kama Kuna mtu anaweza kupinga hatua hii aliyochukua. lakini hiyo haifanyi watu wasipingine mengine ambayo wanaona hayapo sawa.
Hakuna kitu hapo. Serikali ndio mwajiri wa polisi, tume yake haiwezi kuiumbua idara yake. Hata polisi alie nyongwa mahabusi daktari(idara ya serikali) aliamuriwa kuandika hati ya kifo.
 
Watanzania ni wapumbavu sana. Juzi hapa mlikuwa mnalalamika kuwa haiwezekani JESHI LIJICHUNGUZE LENYEWE, leo Rais kaamua kuwe na tume huru ya kufanya uchunguzi huo bado mnalalamika. WAPUMBAVU
Huo si upumbavu, bali kulalamikia utawala mbovu. Miaka yote serikali inalifanya hilo, hakuna sheria au kanuni za kuunda tume.
 
Wengi wanafikiri kwamba Katiba mpya ni magic bullet ya kumaliza kila tatizo. Hakuna katiba itayokuwa ina cover kila kitu.
Pia katiba mpya inatakiwa iwe practised sio maneno matupu.
Katiba Mpya Kenya haijamaliza kila tatizo na bado wana matatizo ya Rais na makamu wake kupingana waziwazi.
 
Polisi ni waonevu sana. Nahisi wanayopewa mafunzo yanawaharibu akili.
 
" Haiwezekani jeshi lifanye mauaji na lijichunguze lenyewe" hii kauli imebeba ujumbe mzito sana, sijui Sirro bado anafanya nini ofisini mpaka leo.

Hapo nampongeza Rais, ni sahihi jeshi haliwezi kujichunguza, ila muhimu na hiyo kamati huru iliyoundwa na serikali iwe huru kweli wanasiasa wasiachwe wakaingilia maamuzi yake.

Nasema hivyo nikitambua mahusiano yaliyoko kati ya jeshi la polisi na wanasiasa wa CCM, inawezekana uhusiano wao hauishii kulindana kwenye chaguzi pekee unakwenda mbali zaidi, hawa wasije kuingilia kazi ya kamati iliyoundwa.

Napendekeza hiyo kamati iundwe na kuongozwa na watu huru wasio na mahusiano na siasa au wanasiasa, sio Waziri Mkuu.
Kuna mtu anaandaliwa KUFUNGASHA VIRAGO....
 
Back
Top Bottom