PostGE2025 Rais Samia: Hakuna dini ya ku-override serikali, toka niingie madarakani TEC wametoa nyaraka 8

PostGE2025 Rais Samia: Hakuna dini ya ku-override serikali, toka niingie madarakani TEC wametoa nyaraka 8

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
umeongea points zenye akili nakukubalia asilimia 100 sema kwa mfano kuhusu upinzani kuna sehemu walizingua wenyewe, kuanza kugoma na kutoa maneno makali sana wakati yeye aliwalegezzea ki ukweli inaudhi,

Pili kweli kabisa ana makosa kafanya kwenye kuwapoteza vijana wakosoagi lile bonge ya kosa sasa sijui washauri wake akina nani ? ila hawa wanaharakati kutoka nje na mikwara ya mabunge ya ulaya utaona kabisa wanatufanya sisi watoto wadogo wanastahili kukemewa japo bado sisi wachanga
Ukiwa mwanasiasa lazima uwe na wanasema " thick skin"
Colin Powell alikataa kugombea urais US licha ya kuwa na sifa zote na kupendwa na vyama vyote lakini alihisi hatoweza kuvumilia "intense scrutiny"
Sio kila kitu ujibu, Mkapa alisema huwezi kuzuia masikio kusikia lakini unaweza kuzuia mdomo kusema
Wapinzani ni sehemu ya maisha ya kisiasa, Watu wanamkosoa Mungu wanalalamika mara jua kali, baridi imezidi etc sembuse binadamu anayekwenda nya!
Wahisani wana nguvu zao, hata hayo mazao au bidhaa na rasilimali tulizo nazo wao ndio wanapanga bei huko masoko ya dunia
Nyerere aliyaona hayo ndiyo maana alikubali kuachia ngazi ili aje mtu atakayekubali masharti yao
Leo unaona US anavyotetemeshana na wababe wenzie China, EU, RUssia kwenye tariffs na hawa kina South Afrika na Venezuela sembuse sie huku wakiamua inatumwa chpa tu wanamyakua Rais kama yule wa Honduras au Panama
 
Mwislamu mwenzangu na Mama yangu katika Imani wanakudanganya kwamba hao TEC sijui ni Wakristo wanaleta udini hakuna udini naomba ukiweza kaa nao hao uongee nao tena wale wanaokupa maneno mabaya kuhusu udini wasiwepo kwenye kikao chenu Tanzania watu wameoana kila sehemu hizo mambo hazipo kaa chini ukague vizuri utakuja kusema..
 
Nashukuru kuona kuna wakatoliki wenzangu hili linawakwaza... Wachunga kondoo wamegeuka wana siasa.. niko Bikira Maria Mpalizwa ila kwa haya yanayojiri kiukweli hata Hija ya bagamoyo tarehe 6 siendi na imekosa mvuto mana kama alivyosema Madam presida kanisa limepata mkanganyiko hatuongei tena lugha moja Sifa kuu ya wakatoliki ni watu watulivu hatupendi heka heka ila TEC wametuletea heka heka ambazo hazina ulazima wowote! Imekua kama kikundi cha Siasa ...
Amani iwe kwenu sasa iko wapi? Amani yangu nawaachia Amani yangu nawapa iko wapi? Kiukweli hata tuhuma tulizopewa Rwanda nimeanza kuziona zinakuja hapa
Mkuu niko pamoja na wewe. Mimi niko Parokia ya Bikira Maria wa huruma, Mbezi Tangi Bovu. Natoa zaka na kuchangia jenga jimbo wakati wa Xmas na Pasaka. Lakini sikubaliani na namna Fr Kitima anavyofanya kazi ya TEC. It seems yeye ana nguvu kuliko Rais wa TEC Bishop Pisa
 
si mlikuwa mnamponda Magufuli kwa kauli hiziii kauli hizii
Kwa Jina la mwenyenzi mungu aliye hai muumba wa mbingu na nchi Magufuli yupo na malaika wanaimba pamoja
 
Huyu bata maji anajaribu kuleta narrative ya udini ili ajinasue but hawezi fanikiwa, uovu wake upo hadharani
 
na ndipo tunapoelekea, waliofika huko walianza hivi hivi
hata humu mijadala ya kidini unaona ilivyo na chuki za wazi
Kiongozi anapaswa kuonesha leadership na siyo kuwa sentimental kwa vitu sensitive hasa vya dini kabila etc
Hasira zake kwa haya mambo azifanye chini kwa chini kama alivyokuwa JK, anawapokea anasikiliza halafu anapotezea au kufanyia kazi kivyake kimya kimya
Nyerere alipiga vita haya mambo, tena hadharani, hata kama alitenda tofauti chinichini
Huyu anakosea sana!
Mkuu mbona amesema dini zote
Tec wametolewa tu mfano ila wameambiwa dini zote hakuna ilio juu ya sheria...nk
Au mm ndo sijasikia
 
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN :VIONGOZI WA DINI MSIJEPE VYEO VYA KUONGOZA NCHI.HATA KAMA HAMUMPENDI RAIS MAMA SAMIA KWA DINI YAKE AU KWA JINSIA YAKE.MNGOJEENI AMALIZE MUDA WAKE WA UONGOZI MUMCHAGUE KIONGOZI MUNAYEMPENDA.


View: https://www.youtube.com/watch?v=nIAs66cv2Vw

Baba Wa Taifa Mwalim Julius Nyerere azungumzia Ukabila na Udini​

 
Anaojaribu kuchezea sharubu wamemzingira mpaka uvunguni mwa anakolala watakapomchoka na dharau zake hatopona!
 
Back
Top Bottom