Rais Samia haupigi mwingi tena, kuna dalili za kutosha kuwa Uchumi utamuelemea

Rais Samia haupigi mwingi tena, kuna dalili za kutosha kuwa Uchumi utamuelemea

Athari hasi za kiuchumi za miaka mitano iliyopita zitaendelea kuiandama nchi hii kwa miaka si chini ya 10 ijayo.

Kwa kuanza, serikali ilitakiwa isifanye matumizi yasiyokuwa ya lazima/muhimu/faida. then pesa kidogo tunayodunduliza ingetumika kustimulate uchumi kwa wananchi wa uchumi mdogo na uchumi wa kati.

Badala yake, Rais na watu wake ndio wakwanza kufuja pesa, Majuzi nilikuwa safarini kurudi Dom, njiani tukasimama kupisha msafara wa mama, aisee gari kama 30 hivi na helicopters 2 juu, walikuwa wanaenda Dar, ajabu ni kuwa kesho yake msafara huo huo ukarudi Dodoma. Mama anaogopa nini kukaa sehemu moja? achague sehemu moja akae, Sisi tutamuelewa kuliko hiki anachokifanya sasa.
 
Furaha imerejea mtaani, uwekezaji umeshamiri, Uhuru wa kuongea umerudi...unapigwa mwingi!
Samia it seems anashindwa kucapitalize kwenye mafanikio na confidence aliyoijenga kwa wananchi katika siku zake 100 za kwanza ofisini.
Hizi measures zake za kufanya maisha ya watu kuwa magumu zaidi halafu at the same time anataka kuendelea na mbinu zilezile za kuminya political space kinyume cha katiba haviwezi kumfikisha popote zaidi ya kuchukiwa na wananchi!.
 
Mambo magumu mwanasiasa anatakiwa kuyafanya wakati ana political capital.....

Bado anayo, wacha aitumie.
 
Athari hasi za kiuchumi za miaka mitano iliyopita zitaendelea kuiandama nchi hii kwa miaka si chini ya 10 ijayo.

Kwa kuanza, serikali ilitakiwa isifanye matumizi yasiyokuwa ya lazima/muhimu/faida. then pesa kidogo tunayodunduliza ingetumika kustimulate uchumi kwa wananchi wa uchumi mdogo na uchumi wa kati.

Badala yake, Rais na watu wake ndio wakwanza kufuja pesa, Majuzi nilikuwa safarini kurudi Dom, njiani tukasimama kupisha msafara wa mama, aisee gari kama 30 hivi na helicopters 2 juu, walikuwa wanaenda Dar, ajabu ni kuwa kesho yake msafara huo huo ukarudi Dodoma. Mama anaogopa nini kukaa sehemu moja? achague sehemu moja akae, Sisi tutamuelewa kuliko hiki anachokifanya sasa.
Siyo Samia tu mwenye kupenda kuzunguuka zunguuka nchini na kushinda angani. Kuna misafara ya mawziri, maktibu wakuu, watumishi wengine kutwa kucha wako barabarani Dar-Dodoma, Dodoma-Dar. Yaani imekuwa serikali ya kusafirisafiri tu, Hawatulizani sehemu moja
Tatizo siyo safari yao, tatizo ni kuwa hizi safari ni gharama kwa mlipa kodi!
 
Sahihi kabisa ndugu!
 
Samia it seems anashindwa kucapitalize kwenye mafanikio na confidence aliyoijenga kwa wananchi katika siku zake 100 za kwanza ofisini.
Hizi measures zake za kufanya maisha ya watu kuwa magumu zaidi halafu at the same time anataka kuendelea na mbinu zilezile za kuminya political space kinyume cha katiba haviwezi kumfikisha popote zaidi ya kuchukiwa na wananchi!.
Tulieni...uchumi ujengwe
 
W
Zipo kila dalili kuwa hali ya uchumi kwenye utawala huu wa Rais Samia unaenda kuwa fyongo! Hali hii itaenda kuyafanya maisha ya wananchi kuwa magumu sana

Nimeangalia kwa mfano viwango vipya vya tozo za miamala ya kutuma fedha na kutoa fedha kupitia mitandao ya simu, Gharama zake zimeongezeka sana wakati mwingine kuwa hata mara mbili ya ilivyokuwa hapo awali.

Athari ya hii kitu, ni kuua microeconomy ambayo ilikuwa imejiintegrate na huu mfumo mitandao ya Mpesa, TiGo oesa na mingineyo, kuua mafanikio ambayo kama Taifa tulishayafikia, maana hii mitandao ilikuwa kama "Miundo mbinu" ya kurahisha biashara kuliko kuwa chanzo kikuu cha mapato ya serikali(Japo hili liligeuka kila kukicha baada ya kuona mafanikio yake).

Sasa hivi wananchi watakuwa wazito kutuma pesa, watakuwa wanatuma tu kama hawana jinsi, lakini wengi watakuwa wanajifikiria mara mbilimbili, kwa hiyo hii itaathiri biashara zilizokuwa zinategemea hii mitandao!. Maana tulishafikia hatua, unanua kitu let say ktk duka fulani liko mbali na wewe kwa kulipia kupitia Mpesa, Tigo pesa halafu unaletewa na mzigo na bodaboda wa kampuni. Sasa hivi ule urahisi na wepesi wa kufanya hivyo hautakuwepo kwa hiyo Mteja hatosumbuka kuagiza mzigo wa mbali na kulipa kupitia hiyo mitandao maana ni ghali sana.

Pia kutuma pesa kusaidia ndugu na jamaa naamini volume ya kutuma itapungua. Maana kila ukituma pesa fulani unajikuta makato ni mengi, kwa hiyo hata ule ubinaadamu wa kusaidia ndugu huko vijijini nao utapungua kidogo. Mtu utakuwa unatuma pale inapobidi sana lakini si kwa frequency kubwa.

Wakati tunaongea hayo, kuna ongezeko la kodi katika mafuta, hii imeanza kuathiri bei za vitu. Tumeona kwa mfano Mamlaka za Usafiri nchini LATRA imetoa bei mpya ua nauli za mabasi mikoani. Gharama nazo zimeongezeka, hii maana yake wafanyabiashara wanaosafiri kufuata mzigo itabidi waongeze gharama za usafiri kwenye bei ya bidhaa watakazouza, matokeo yake bei za vitu zitakuwa juu sana na maisha yatakuwa magumu zaidi.

Wakati huo Samia anaonekana anaenjoy kuendelea kukopa mihela kedekede kutoka nje, Mwezi uliopita au miwili iliyopita alipata mkopo wa Matrilion ya fedha kutoka taasisi za nje, Na sasa hivi anataka mkopo kwa ajili ya masuala ya Korona. Sasa hakuna free lunch duniani, hii mikopo ndiyo inakwenda kutunyonga sisi wananchi, maana ili ilipwe lazima afikirie kutukamua kodi.

Mishahara hujaongeza, gharama za maisha zinazidi kupanda halafu bado unafikiri kutuongezea kodi, hizo pesa tuzipate wapi sisi ewe Samia rais wetu?

Kibaya zaidi, hakuna political reform yoyote inayoendana na uelekeo huu wa maisha magumu ya wananchi. Hii itapelekea Nchi kuvimba, na Samia asipohakikisha anatoa oppoetunity ya nchi kupumua kiuchumi na kisiasa, atajiluta katika wakati mgumu sana kutawala nchi hii! Nimpongeze alishtukia mtego wa kuwafukuza wamachinga akaukataa, ule ungemsumbua sana, maana mwenye njaa hana cha kupoteza!

Huu ni muda muafaka Samia atafute wachumi waliobobea wamshauri namna ya kuendesha huu uchumi. Lazima awe mbunifu wa vyanzo vipya vya mapato.

Hii nchi ina ardhi kubwa, ina bahari, ina mito, ina maziwa, ina kila kitu, huo ubunifu wa kupata hela nyingi kupitia vyanzo hivyo uko wapi?. Mnawaza kuwapiga kodi wananchi doubledouble, yaani nitume pesa nitozwe kodi, nitoe pesa nitozwe kodi tena, yaani kipesa hichohicho mnanyakuanyakua mara mbilimbili cone on!

Wakati hayo yanafanyika kuna watu nchi hii mishahara yao haikatwi kodi, Rais hakatwi kodi, Wabunge hawakatwi kodi, Majaji wa mahakama zetu mishahara yao haikatwi kodi. Hii inakuwaje?, Huu ni unyonyaji!., Tunataka hawa nao waanze kukatwa kodi kwenye mishahara yao kama watu wengine.

Lakini ukiacha hilo, Juzi Jaji warioba alizungumza kuhusu serikali. kubana matumizi.

Sasa sisi tunaona rais Samia muda mwingi yuko kwenye ndege anaenda Dodoma, anaridi Dar, anaenda Dodoma anarudi Dar. Hizo gharama za kupeleka hilo li airbus anazibeba nani?

Hao wakuu wanaompokea Dar airport akija, na hao wanaomsindikiza na kumpokea tena na kumsindikiza tena watafanya kazi zao ofisini saa ngapi, ina maana watafanya kazi ya kumsindikiza na kumpokea Samia tu?

Lakini wakati hayo yakifanyika eti wanawaza kumjengea Magufuli sanamu. Mambo ya ajabu kweli yanafanyika katika nchi hii. Hizo milioni 420 wanazotaka kutumia kujenga sanamu zingetolewa kama mikopo ya ujasirimali. kwa vijana zingesaidia vijana wangapi kutoka katika limbwi la umasikini?

Hapana aisee, Samia angalia Washauri wako wa uchumi na siasa, something is wrong!
Anajua kuwa wakijenga sanamu basi tutajua kuwa wapo pamoja na marehemu na huku Alibana Sana hela zetu
 
Ni vizuri tukatangaziwa makusanyo ya kodi kwa kila mwezi!! Tunapochangia kwa kutoa kodi, ni halali tukaambiwa zimekusanywa sh ngapi kwa kila mwezi ili tujue mwelekeo waserikali katika kutimiza majukumu yake. Kodi siyo siri.
 
Zipo kila dalili kuwa hali ya uchumi kwenye utawala huu wa Rais Samia unaenda kuwa fyongo! Hali hii itaenda kuyafanya maisha ya wananchi kuwa magumu sana.....
Consequences: Inflation juu, riba ya mikopo juu, FDI flows hasi, exports hasi, imports juu, household consumption "marginal" na miayo kwa wingi, utulivu kisiasa hakuna ukiambatana na matumizi makubwa ya nguvu za dola, uasi na magereza kufulika, na hatimaye anguko la chama tawala na serikali yake.
 
Nadhani Siyo uchumi utamwelemea,ulishaanza kumwelemea tayari! Unafikiri Deni la Taifa alilokuta la t.71/- linalipwaje? Bado kukamilisha miradi iliyoendeshwa kwa kukwapua fedha za wafanyabiashara (fedha zetu za ndani)!
 
Back
Top Bottom