Rais Samia haupigi mwingi tena, kuna dalili za kutosha kuwa Uchumi utamuelemea

Rais Samia haupigi mwingi tena, kuna dalili za kutosha kuwa Uchumi utamuelemea

Nadhani Siyo uchumi utamwelemea,ulishaanza kumwelemea tayari! Unafikiri Deni la Taifa alilokuta la t.71/- linalipwaje? Bado kukamilisha miradi iliyoendeshwa kwa kukwapua fedha za wafanyabiashara (fedha zetu za ndani)!
Deni la taifa trillion 71? Sio kweli ni trillion 47
 
Katikati ya Covid-19 nchi za watu wenye kupanga mambo zinatoa hela kusaidia raia wake wasitetereke kiuchumi.

Sisi huko ndiyo kwanza tunawanyuka wananchi kwa kodi na tozo.

Serikali imejikita kwenye miradi mingi ya kijinga, kama daraja jipya la Selander, ambalo limejengwa kama mapambo ya kupendezesha jiji zaidi ya kusolve traffic flow, na sasa inahitaji hela kulipia madeni makubwa haya.
 
Siyo Samia tu mwenye kupenda kuzunguuka zunguuka nchini na kushinda angani. Kuna misafara ya mawziri, maktibu wakuu, watumishi wengine kutwa kucha wako barabarani Dar-Dodoma, Dodoma-Dar. Yaani imekuwa serikali ya kusafirisafiri tu, Hawatulizani sehemu moja
Tatizo siyo safari yao, tatizo ni kuwa hizi safari ni gharama kwa mlipa kodi!
Tulia mkuu!

Sasa hivi mnapumua! Mna uhuru mliokuwa mnautaka!
 
Nilikuwa namsapoti kufikia juzi tu ila leo ukiniuliza kama bado nna matumaini nae nakuambia hapana.
Kwa namna anavyorukia mambo sensitive ya kiuchumi yanayokwenda kuumiza watu wa chini ni wazi huu ni utekelezaji wa sera za mashirika ya kimataifa ambazo hazijawahi kumuacha salama kiongozi yoyote wa Africa.
Nimekata tamaa nae.
 
Zipo kila dalili kuwa hali ya uchumi kwenye utawala huu wa Rais Samia unaenda kuwa fyongo! Hali hii itaenda kuyafanya maisha ya wananchi kuwa magumu sana...
Kuna watu mnapendwa sana kufurahishwa. Mama samia anafanya kazi nzuri kuliko marais wote waliopita
 
Mama Samia atuonee huruma kwa kweli, mara nyingi kila kitu kinachigusa waliowengi kinawekewa vikwazo au ndio tunatakiwa tubaki wanyonge milele.
 
Mod naomba msibadilishe heading imekaa vizuri tuu!

HAYA NDO MAKATO MAPYA KWA MATUMIZI YA SIMU, KUTOA NA KUWEKA PESA.

MMEONA MAKATO MAPYA YA MIAMALA KUTOA KWA WAKALA????

Kutoa 100,000 ilikua 3600 sasa hivi 6,100
Kutoa 200,000 ilikua 5300 sasa hivi 8,240
Kutoa 300,000 ilikua 6500 sasa hivi 10,000
Kutoa 400000 ilikua 7000 sasa hivi 11,100
Kutoa 500,000 ilikua 7500 sasa hivi 12,700
Kutoa 600,000 ilikua 8000 sasa hivi 13,900
Kutoa 700,000 ilikua 8000 sasa hivi 15,100
Kutoa 800,000 ilikua 8000 sasa hivi 15,520
Kutoa 900,000 ilikua 8000 sasa hivi 16,900
Kutoa 1,000,000 ilikua 8000 sasa hivi 17,400
Kutoa 3,000,000 ilikua 10000 sasa hivi 20,000

Hiyo list ni ya MAKATO YA ZAMANI NA YA SASA NA HAPO NI KUTOA KWA WAKALA.
 
Maneno huwa ni roho kamili inayoishi,yule alitusomesha namba huyu keshalewa madaraka nae katuzika kabisa.
Hela zenyewe zinaenda kuliwa utasikia mkurugenzi kapiga 400 mara wizara fulani 800
 
Mod naomba msibadilishe heading imekaa vizuri tuu!

HAYA NDO MAKATO MAPYA KWA MATUMIZI YA SIMU, KUTOA NA KUWEKA PESA.

MMEONA MAKATO MAPYA YA MIAMALA KUTOA KWA WAKALA????

Kutoa 100,000 ilikua 3600 sasa hivi 6,100
Kutoa 200,000 ilikua 5300 sasa hivi 8,240
Kutoa 300,000 ilikua 6500 sasa hivi 10,000
Kutoa 400000 ilikua 7000 sasa hivi 11,100
Kutoa 500,000 ilikua 7500 sasa hivi 12,700
Kutoa 600,000 ilikua 8000 sasa hivi 13,900
Kutoa 700,000 ilikua 8000 sasa hivi 15,100
Kutoa 800,000 ilikua 8000 sasa hivi 15,520
Kutoa 900,000 ilikua 8000 sasa hivi 16,900
Kutoa 1,000,000 ilikua 8000 sasa hivi 17,400
Kutoa 3,000,000 ilikua 10000 sasa hivi 20,000

Hiyo list ni ya MAKATO YA ZAMANI NA YA SASA NA HAPO NI KUTOA KWA WAKALA.
Na yote hayo mwananchi ndo ubebeshwa hapo bado mafuta petrol vijijini 2500 kwa lita,
 
Back
Top Bottom