Rais Samia haupigi mwingi tena, kuna dalili za kutosha kuwa Uchumi utamuelemea

Athari hasi za kiuchumi za miaka mitano iliyopita zitaendelea kuiandama nchi hii kwa miaka si chini ya 10 ijayo.

Kwa kuanza, serikali ilitakiwa isifanye matumizi yasiyokuwa ya lazima/muhimu/faida. then pesa kidogo tunayodunduliza ingetumika kustimulate uchumi kwa wananchi wa uchumi mdogo na uchumi wa kati.

Badala yake, Rais na watu wake ndio wakwanza kufuja pesa, Majuzi nilikuwa safarini kurudi Dom, njiani tukasimama kupisha msafara wa mama, aisee gari kama 30 hivi na helicopters 2 juu, walikuwa wanaenda Dar, ajabu ni kuwa kesho yake msafara huo huo ukarudi Dodoma. Mama anaogopa nini kukaa sehemu moja? achague sehemu moja akae, Sisi tutamuelewa kuliko hiki anachokifanya sasa.
 
Furaha imerejea mtaani, uwekezaji umeshamiri, Uhuru wa kuongea umerudi...unapigwa mwingi!
Samia it seems anashindwa kucapitalize kwenye mafanikio na confidence aliyoijenga kwa wananchi katika siku zake 100 za kwanza ofisini.
Hizi measures zake za kufanya maisha ya watu kuwa magumu zaidi halafu at the same time anataka kuendelea na mbinu zilezile za kuminya political space kinyume cha katiba haviwezi kumfikisha popote zaidi ya kuchukiwa na wananchi!.
 
Mambo magumu mwanasiasa anatakiwa kuyafanya wakati ana political capital.....

Bado anayo, wacha aitumie.
 
Siyo Samia tu mwenye kupenda kuzunguuka zunguuka nchini na kushinda angani. Kuna misafara ya mawziri, maktibu wakuu, watumishi wengine kutwa kucha wako barabarani Dar-Dodoma, Dodoma-Dar. Yaani imekuwa serikali ya kusafirisafiri tu, Hawatulizani sehemu moja
Tatizo siyo safari yao, tatizo ni kuwa hizi safari ni gharama kwa mlipa kodi!
 
Sahihi kabisa ndugu!
 
Tulieni...uchumi ujengwe
 
W
Anajua kuwa wakijenga sanamu basi tutajua kuwa wapo pamoja na marehemu na huku Alibana Sana hela zetu
 
Ni vizuri tukatangaziwa makusanyo ya kodi kwa kila mwezi!! Tunapochangia kwa kutoa kodi, ni halali tukaambiwa zimekusanywa sh ngapi kwa kila mwezi ili tujue mwelekeo waserikali katika kutimiza majukumu yake. Kodi siyo siri.
 
Zipo kila dalili kuwa hali ya uchumi kwenye utawala huu wa Rais Samia unaenda kuwa fyongo! Hali hii itaenda kuyafanya maisha ya wananchi kuwa magumu sana.....
Consequences: Inflation juu, riba ya mikopo juu, FDI flows hasi, exports hasi, imports juu, household consumption "marginal" na miayo kwa wingi, utulivu kisiasa hakuna ukiambatana na matumizi makubwa ya nguvu za dola, uasi na magereza kufulika, na hatimaye anguko la chama tawala na serikali yake.
 
Nadhani Siyo uchumi utamwelemea,ulishaanza kumwelemea tayari! Unafikiri Deni la Taifa alilokuta la t.71/- linalipwaje? Bado kukamilisha miradi iliyoendeshwa kwa kukwapua fedha za wafanyabiashara (fedha zetu za ndani)!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…