Rais Samia huna nia njema na Wizara ya Nishati, haifiki kokote kwa teuzi za urafiki

Umeandika sawa, ila wanaosema Rais ndo tatizo kwa kumlinganisha na JPM ndo hawapo sawa.
JPM alimchagua Samia kuwa mgombea mweza mara 2. Alifanya hivi akijua Makamu wa Rais ni mtu mwenye sifa zote za urais.
Angeweza kumpeleka Zanzibar akawe Rais kama alivofanya kikwete kwa shein 2010, lakini alimuacha akijua anayaweza majukumu aliyonayo.
Magufuli pia alimteua Makonda kuwa mkuu wa mkoa, Kitwanga kuwa waziri, Muhongo kuwa waziri na Ninja kuwa waziri wa mambo ya ndani.
 
Ushahidi wa akili kubwa ya JPM ukipunguza bei utawezesha watu wengi kupata huduma ambayo kimsingi ni fursa ya wao kujitegemea kwa kuanzisha shughuri mbalimbali zinazotegemea umeme na kujenga uwezo wa kulipia matumizi yao ya umeme,hivyo kuongeza wateja na mwisho wa siku tanesco kupata Pato kubwa,kuongoza kunahitaji maono,mtaishia kujaa madeni Kama hamna timamu.
Kama unazungumzia kupunguza bei ya kuunganisha umeme ... alipunguza hadi kufikia Sh. ngapi na lini?!
 
Mwanamaji ongeza kanyana kidogo.
Mkuu, hili suala mimi naliona katika sura mbili (nina hisia mchanganyiko).

1. Mambo yalivyopaswa kuwa (as it should be).
Kwakuwa umeme na miundombinu yake ni mali ya TANESCO, umeme ulipaswa kuunganishwa kwa mteja bure kabisa. Au pengine kulipaswa kuwa na "bonus" kwa mteja kuunganishiwa umeme.
Mfano, Unganisha umeme ujishindie smartphone, au Unganisha umeme ujishindie unit 100 za bure.

2. Mambo yalivyo (as it is).
Huu sasa ndio UHALISIA wa mambo.
Uwezo wa TANESCO kwa sasa kuunganishia watu umeme bure, au kwa 27,000 ni mdogo mno au haupo kabisa.
Tukiwalazimisha kuunganishia watu umeme kwa hiyo 27,000 au bure, watakua wanachukua buku 27 zetu then wanaanza kutupiga chenga kuunganishia umeme. NJOO KESHO zitakua nyingi.

Msingi mkubwa wa hizi gharama ni "tusaidiane ili mambo yaende" yaani cost sharing.
Hivyo mabishano yote haya msingi wake ni nani achange nini.

Mimi binafsi nawaelewa TANESCO katika hili, elfu 27 kimsingi sio jukumu la mteja, ila kiuhalisia italitia hasara shirika tajwa.
 
Mama amejikuta paap ni rais hivyo hata yeye hajui imekuwaje ni rais, acha tupate tabu
Mama hajui sasa afanyaje ,ila ni msikivu sana tumieni proper channel ,anajitahidi sana kapambana ,mungu amsaidie ila amepunguza wanafiki ,sema kwenye vya technical hakujua angesikiliza tulio maeneo technical ,ila nawaapia tunaenda poa bSSa
 
Mkuu, hili suala mimi naliona katika sura mbili (nina hisia mchanganyiko).

1. Mambo yalivyopaswa kuwa (as it should be).
Kwakuwa umeme na miundombinu yake ni mali ya TANESCO, umeme ulipaswa kuunganishwa kwa mteja bure kabisa. Au pengine kulipaswa kuwa na "bonus" kwa mteja kuunganishiwa umeme.
Mfano, Unganisha umeme ujishindie smartphone, au Unganisha umeme ujishindie unit 100 za bure.

2. Mambo yalivyo (as it is).
Huu sasa ndio UHALISIA wa mambo.
Uwezo wa TANESCO kwa sasa kuunganishia watu umeme bure, au kwa 27,000 ni mdogo mno au haupo kabisa.
Tukiwalazimisha kuunganishia watu umeme kwa hiyo 27,000 au bure, watakua wanachukua buku 27 zetu then wanaanza kutupiga chenga kuunganishia umeme. NJOO KESHO zitakua nyingi.

Msingi mkubwa wa hizi gharama ni "tusaidiane ili mambo yaende" yaani cost sharing.
Hivyo mabishano yote haya msingi wake ni nani achange nini.

Mimi binafsi nawaelewa TANESCO katika hili, elfu 27 kimsingi sio jukumu la mteja, ila kiuhalisia italitia hasara shirika tajwa.
Uzi ufungwe....Kama kuna asiyeelewa hapa ataelewa mbinguni
 
Kuna watu pale wanataka TANESCO izalishe faida kwenye kila stage.

Watambue tu kwamba faida itakuja pale huduma itakuwa bora.

Sasa hivi wamejazana business men na waoiga dili.
 
JNHHP inaendelea kujengwa kama kawaida mkuu. Hakuna wa kuzuiaJNHPP isikamilike. Serikali inatoa hela zote kwa wakati.

LNG plant haiwezi kuua JNHPP. Hakuna mwenye akili mbovu kama hizo. Hilo liko wazi.
Shida ni negativity. Tayari akili zimeshajengwa kwamba bila ya fulani basi mradi hautafanikiwa.

Ndiyo maana kila wakiamka wao kazi yao ni kupiga vita tu.
 
Kama kuna Taasisi au Shirika lililo na changamoto za kiuongozi ni linalohusika na shughuli za uzalishaji kama vile viwanda. TANESCO kwa upande mmoja inazalisha umeme, hivyo basi, inahitaji uongozi wenye sifa na ujuzi wa kuzalisha.

Kwa uteuzi wa "mangwini" (waliopata elimu kwa kutumia vitabu vya "penguin") watapata shida sana kuliendesha kwa kuwa wafanyakazi wazalishaji watakuwa wanawalisha taarifa potofu inapotokea tatizo la kifundi (rejea kauli ya Waziri Makamba ati "umeme unakatikakatika kwa sababu ya waya uchi kugusana"!!!!)

Kama Rais SSH anawaona hao aliowateua wanafaa sana aigawanye TANESCO ya kuzalisha na kusambaza, na ya kutoa huduma (kuuza umeme). Wateule wake waendesha TANESCO huduma.
Kalemani ni mwanasheria

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Tukubali kwamba hii ni Wizara ambayo waliowekwa ni watu misheni town tu.

Nimesikiliza hata huyo anayeitwa Maharage Chande ni aibu tu. Yaani anahangaika na gharama za kuunganisha umeme! Hizo gharama zinaleta faida ktk shirika?

Yeye anatakiwa azalishe na kuuza umeme kwa faida badala ya kuhangaika na kuunganisha kwa gharama kubwa. Hawa ni watu wasiojitambua. Nadhani kosa limeanzia kwenye uteuzi. Huwezi kuteua watu 'ngwini' kwenye wizara ambayo mambo yote ni sayansi.

Waziri 'ngwini'. Mkurugenzi Tanesco 'ngwini' Bodi ya watu 8 ina wahandisi wawili ambao walishasahaulika kwenye bodi ya mainjinia, wengine pia ni Ngwini.

Biashara ya umeme inahitaji uzalishaji wa kisayansi na kuuza umeme kisayansi. Ni tofauti na kutafuta wateja wa Multichoice au kuuza ticketi za TFF.
Vyeo vya shukrani
 
Kama kuna Taasisi au Shirika lililo na changamoto za kiuongozi ni linalohusika na shughuli za uzalishaji kama vile viwanda. TANESCO kwa upande mmoja inazalisha umeme, hivyo basi, inahitaji uongozi wenye sifa na ujuzi wa kuzalisha.

Kwa uteuzi wa "mangwini" (waliopata elimu kwa kutumia vitabu vya "penguin") watapata shida sana kuliendesha kwa kuwa wafanyakazi wazalishaji watakuwa wanawalisha taarifa potofu inapotokea tatizo la kifundi (rejea kauli ya Waziri Makamba ati "umeme unakatikakatika kwa sababu ya waya uchi kugusana"!!!!)

Kama Rais SSH anawaona hao aliowateua wanafaa sana aigawanye TANESCO ya kuzalisha na kusambaza, na ya kutoa huduma (kuuza umeme). Wateule wake waendesha TANESCO huduma.
Teuzi za udini
 
Tukubali kwamba hii ni Wizara ambayo waliowekwa ni watu misheni town tu.

Nimesikiliza hata huyo anayeitwa Maharage Chande ni aibu tu. Yaani anahangaika na gharama za kuunganisha umeme! Hizo gharama zinaleta faida ktk shirika?

Yeye anatakiwa azalishe na kuuza umeme kwa faida badala ya kuhangaika na kuunganisha kwa gharama kubwa. Hawa ni watu wasiojitambua. Nadhani kosa limeanzia kwenye uteuzi. Huwezi kuteua watu 'ngwini' kwenye wizara ambayo mambo yote ni sayansi.

Waziri 'ngwini'. Mkurugenzi Tanesco 'ngwini' Bodi ya watu 8 ina wahandisi wawili ambao walishasahaulika kwenye bodi ya mainjinia, wengine pia ni Ngwini.

Biashara ya umeme inahitaji uzalishaji wa kisayansi na kuuza umeme kisayansi. Ni tofauti na kutafuta wateja wa Multichoice au kuuza ticketi za TFF.
Hao akina Maharage Chande walishajichokea, wameona 27,000/= ndo issue ya kuongelea kwamba shirika linapata hasara lakini wizi mkubwa wa umeme unaofanyika hawajui namna gani watadhibiti. TANESCO inapoteza mabilioni ya pesa kila mwezi kwa wezi wa umeme wakishirikiana na watumishi wasio waaminifu wa shirika inawezekana huo mgao wa pesa unamfikia pia huyo Maharage. Tulikwishawaambia baadhi ya maeneo tunayoyajua yenye wizi mkubwa wa umeme kama Igogo na Sahara Jijini Mwanza, huko kuna watu wana TANESCO yao wameunganishiwa umeme bila mita na wao wanausambaza majumbani kwa malipo yaliyo sawa kwa kila nyumba, uamue kupikia jiko la umeme sawa tu, uambue kutumia mashine ya kuchomelea ni wewe tu lakini malipo ya mwezi ni shilingi 10,000/=
 
Hapo kwenye kuwaunganishia wateja wapya umeme "kisayansi", ndio bei yake inatakiwa kuwa 27,000 nchi nzima mkuu?
Ungeniuliza mimi ningesema 27,000 siyo hata issue ya Mkurugenzi kujadili. Hiyo ni sawa na machinga anavyonunua betri na kuweka kwenye kipaza sauti kuita wateja. Wateja hawahitaji kufidia ghrama za nyaya na nguzo na vikombe na mita. Hizo ni assets za shirika na ni wao wanaojua specification zake.
 
huyo jamaa sio ngwini mkuu, ila labda useme experience tu kwenye hiyo sector

View attachment 2128953
Kwa tafsiri ya neno 'Ngwini' Pale UD, huyu ni 'NGWINI'.
Ungeweza kumtetea sana kwa vigezo vya uzoefu hata hivyo inaonekana uzoefu wa bwana Maharage ni uharibifu. Kama ni kweli alikuwa kwenye ile President's Delivery Bureau, Basi huyu ni mwizi mzoefu. Hiyo Bureau iliundwa ili kuiba pesa za miradi ya serikali. Yawezekana aliiba vizuri sasa wanamkumbuka kwa njia hii. He is a non-starter!
 
Hao akina Maharage Chande walishajichokea, wameona 27,000/= ndo issue ya kuongelea kwamba shirika linapata hasara lakini wizi mkubwa wa umeme unaofanyika hawajui namna gani watadhibiti. TANESCO inapoteza mabilioni ya pesa kila mwezi kwa wezi wa umeme wakishirikiana na watumishi wasio waaminifu wa shirika inawezekana huo mgao wa pesa unamfikia pia huyo Maharage. Tulikwishawaambia baadhi ya maeneo tunayoyajua yenye wizi mkubwa wa umeme kama Igogo na Sahara Jijini Mwanza, huko kuna watu wana TANESCO yao wameunganishiwa umeme bila mita na wao wanausambaza majumbani kwa malipo yaliyo sawa kwa kila nyumba, uamue kupikia jiko la umeme sawa tu, uambue kutumia mashine ya kuchomelea ni wewe tu lakini malipo ya mwezi ni shilingi 10,000/=
Nilipomuona Waziri Januari amevaa suti na miwani, akizungumza kama philosopher ingawa maneno hayakuwa na philosophy, nikajua TANESCO kwa heri. Tanesco haihitaji ujidai unajua, inahitaji mtu anayejitambua hajui ili watu wamweleze asiyoyajua. Sasa kama aliingia kwa ujuaji, ameanza kuonesha u-mbumbumbu wake.

Pale Dar kuna viwanda vinayeyusha vyuma chakavu usiku kwa kutumia umeme bila mita. Mchana ukienda wanatumia mita. Vijana wa TANESCO wanajua na wanakula bili kila mwezi! Haya ni mengi muno na 'mameneja' wa kanda na mikoa na makao makuu wanafahamu. Sasa huyo Maharage Chande na ujanja wa misheni misheni atafika wapi na wa-TZ?
 
Mkuu, ni kiwanda au viwanda gani hivyo.
Nadhani ukifichua wizi utakua umesaidia shirika na umesaidia nchi yetu.
TUPAZE SAUTI
 
Alipunguza kutoka bei iliyokuwapo Hadi 27000 nchi nzima ili watanzania wapate fursa ya kutumia umeme.
Bei ya 27,000 ipo tangu 2014!

Sasa kama JPM alikuwa Rais 2014 au hata waziri wa nishati, basi sawa... heshima ya kipekee kwake JPM kwa kushusha gharama za kuunganishiwa umeme vijijini hadi kufikia Sh. 27,000!
 
Back
Top Bottom