Rais Samia ikiwezekana kwepa kuwalenga Wasukuma moja kwa moja kwenye hotuba zako

Tulieni dawa iwaingie vyema na hamna mamlaka ya kumkosoa mh rais wa nchi.
Ha ha haaaa! Yamekuwa hayo tena? Tukirudi kwa kesi ya mwenzetu nadhani lugha itabadilika, siyo? Ha ha haaaa
 
Mikoa ya kanda ya ziwa ni kama ifuatavo Mwanza kiongozi wa kanda, Geita, shinyanga, simiyu, tabora, kigoma, mara na kagera yaani litakaloanzia mwanza kisiasa ujue mikoa tajwa italifuata kwa nguvu moja kabisa,
Tabora tangu lini ni kanda ya Ziwa Victoria? Weka orodha ya mikoa ya kanda ya kati.
 
Hiyo2025 yenyewe sijui kama atafika maana anazidi kuchafua nchi na umoja umepotea tumaini limeondoka katika kila kitu
Katoka Mwanza huyooo Zanzibar. Yaani tokea awe Rais hajatembea kijiji hata kimoja. Yeye ni.mijini na nchi za nje tu.Anachua tu anga na moshi wa ndege.
 
Sasa ni wakati muafaka wa Kutenga maeneo ili wafugaji wasizurure hovyo na mifugo kuharibu mazingira na mashamba.
 
Kwa kweli mama ameteleza mno kuwananga tena kwa kuwataja kabisa huku akiwa amezungukwa na Maaskofu Wasukuma zaidi ya Saba 🤔 tena wakatoliki!
Wasukuma waharibifu wa mazingira,wameharibu kwao Sasa wapo rukwa huko wanachunga ng'ombe,wanakata Sana miti bila sababu
 
Katoka Mwanza huyooo Zanzibar. Yaani tokea awe Rais hajatembea kijiji hata kimoja. Yeye ni.mijini na nchi za nje tu.Anachua tu anga na moshi wa ndege.
Rais ni taasisi,hasafiri bila sababu za msingi,na hawajibiki kukuambia kwa nini anasafiri
 
Mjomba wako alipokuwa anataja makabila mengine ulikenyua meno, tulieni sindano iwaingie
 
Bila shaka angezungumzia wafugaji! Maana kauli hii inaweza kupelelea wakuu wa mikoa na askari wanyama pori kuanza kudhulu wafugaji bila sababu za msingi! Ukweli anaujua ni uzembe wa utawala wake ndo maana haya yanatokea!
Mjinga wewe, ng'ombe anaswaga yeye, au walianza kuswaga wakati wake?
 
Hahahhaa nchi hii watu kweli wamegawanyika sana! Yaani siku wakikutana watauana maana chuki imetanda si mchezo kuna mda mtu hajui hata adui yake ni nani!
CCM, ilidhani inafanya mzaha tu, kumbe inapanda, inaweka mbolea, inamwagilia maji na kupalilia mbegu ya ubaguzi, bila gharama yake ni kubwa. Tunalo hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…