Hata huku makazini tuliko utaona kabisa kijana mchapa kazi, shupavu tusio na maringo. Weledi.
Ukiuliza vizuri utaambiwa yule jamaa ni CHADEMA.
Niliwahi kuandika humu kuwa hata Ukisikia Wakili au Mwanasheria Mbabe na Kichwa kikali basi hutakuta mahali pengine bali ni CHADEMA.
Hotuba ya Mh Rais Samia imedhihirisha kuwa kikao cha leo cha baraza la vyama vya siasa na wadau wa demokrasi hakihitaji Zitto, Lipumba wala Chongola na Chalamila bali kilihitaji Watu wazito wenye weledi na hoja kuntu kama Mh Mbowe na Mh Tundu Lissu.
Sikiliza Hotuba ya Rais Samia utaona Njaa ya kuikosa CHADEMA kwenye jambo lao.