Tetesi: Rais Samia kubadilisha Baraza la Mawaziri hivi punde

Huu ni moja ya mikakati yake mkuu. Mama amedhamiria kulala mbele na wezi wa rasilimali za taifa.
Safi sana ila wapo wengi sana inahitaji wasaidizi wengi maana huwa hawana huruma washenzi hao
Atajaribu kuwamaliza ila mmh
 
Tumekusikia dada mbadhirifu
 
Ikitokea akabadilisha jambo ambalo nahisi halitatokea, atabadilisha kwa sababu zake wala sio kwa sababu ya ripoti ya CAG ripoti ya CAG huko serikalini imeshatupwa kwenye kaburi la sahau.
 
Kama ni kweli basi itakuwa ni hatua moja nzuri mbele.
 
Mama anayagwaya mafisadi kinoma...au labda tatizo ni mshika rimoti??.
 
Utakuwa mmoja wao. Endelea kulamba asali. Wazuri hawafi mapema.God is good.
 
Hana Option zaidi ya Kurudi kuteua kutoka Bunge la Mchongo, akina Babu Tale, Msukuma, Kishimba, Kibajaji na Vilaza wengine
 
Naamini kikubwa alichofanya ni kusema "Stupid".. Hapo ndipo nguvu yake ilipoishia.

So far Watanzania tumeshasahau na tunaendelea na Maisha....
 
Nilitamani kuandika kitu serious, lakini nimekuja ku learn kuwa you are a child ! Ulicho andika unakijua mwenyewe.
 
HIlo haliwezekani kabisa sababu baadhi ya mafisadi papa ni watu wanamhusi yeye binafsi na ni watu wake karibu. Ikumbukwe pia CCM kama taasisi huwa inahusika katika ufisadi mkubwa hasa unapokaribia uchaguzi
 
Hilo ni jizi lililobobea mkuu. Haya ndiyo mjitu yanayotafutwa na Samia yafungwe jela ili liwe fundisho kwa wengine.
 
Nakula kwa urefu wa kamba,kamba yangu sio ndefu sana

Hata wewe ukipewa nafasi utakula ,Shida ndio zinakufanya upige kelele

Lakini pesa inaleta comfortability fulani na kujiamini mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee punguza wizi wa fedha za umma utakupeleka jehanamu. Hupendi kufika mbinguni?
 
Kwahiyo wale walioongeza bei kwenye manunuzi ya ndege nao ni makosa ya kihasibu


Wale walioongeza bei kwenye mabehewa ya treni ya sgr nao ni issue ya makosa ya kihasibu


Wale wanaokopeshana nhif hela zote za members WA mfuko Hadi mfuko unakaribia kucollapse ?


Wale walioongeza cha juu kwenye ujenzi WA treni ya mwendokasi (sgr) phase 3?


Una ujinga Sana wewe

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…